Wamiliki wa Mabasi ya Dar Lux, ujumbe wenu huu

mushongokle

Member
Sep 23, 2014
95
113
Wamiliki wa Dar Lux jitahidini kuyafanyia mabus yenu service. Leo bus lenu namba T345 DNX, hili bus la Kutoka Mwanza kwenda DSM limetusababishia na kutuharibia ratiba.

Tangu tunaanza Safari saa 12 katika ofisi zenu gari lilianza kusumbua mpaka muda huu saa nne usiku tumekwama hapa Kongwa; gari linasumbua hakuna suluhisho lolote hakuna basi mbadala.

Hii sio sahihi kabisa; unasababisha hasara na usumbufu sana.
 
Hii inaelekea ukingoni tyr inapumulia mirija, basi tu inajikaza kwasababu ina vitendea kazi, ila account zao hamna kitu, its a matter of time.
Kampuni nyingi za mabasi zinapumulia mashine hasa kutokana na ile kashkashi ya Corona, ni wachache mno wenye pumzi.
 
Tatizo la wafanyabiashara wa Tanzania Ni consistence ya standard huanza vizuri Sana Tena mno Hadi wanakuwa na Monopoly lakini ku maintain standard Ni shida wakisha grow na kuwa na customer base kubwa

kampuni nyingi za watanzania hufa zikiwa kubwa kwa kutoelewa maintain standard ya service

Dar Lux alishakuwa na Monopoly ya route kibao kukosa kumaintain service standard Kuna mgarimu watu wanahamia mabasi mengine
Scandinavia alifunga virago sokoni sababu hiyo hiyo

Mabasi kibao ya route ya Moshi Arusha yamehamwa na wateja sababu hiyo hiyo ya kuto maintain customer service standard
 
...Scandinavia alifunga virago sokoni sababu hiyo hiyo...
Umeongea mujarabu kote ila hapo nakukata kama mjumbe, (kama jambo ulijui kaa kimya mkuu) Scandinavia haikuondoka kwa sababu uliyotaja asee..!

Yote kwa yote Dar lux ndiyo safari ya kumupulia machine imeanza, nikipita pale mianzini arusha naona ofisi yao imebaki kijiwe tu kukatia abilia noah na coaster za magazeti zinazorusi Dar.
 
Upo sahihi mkuu. Scandinavia mpaka wakati inafunga biashara yake haikuwahi ku compromise na standards za huduma zake! Siku zote walitoa huduma nzuri consistently.

Inawezekana miongoni mwa sababu za mambo yao kwenda kombo ni pamoja na mivutano ya mikataba kati ya wenye shares, gharama kubwa za uendeshaji, hujuma kwa sababu za kisiasa na pengine mikopo ya bank. Hivyo ndio vilikua vyanzo vya Scandinavia kuondoka kwenye biashara

Kwa maoni yangu aina ya kiwango cha huduma kilichokua kinatolewa na Scandinavia Express ndio ilikua ni standard inayotakiwa kwa watoa huduma ya usafirishaji abiria na yeyote atakayeweza kufanya vile atachukua asilimia kubwa ya soko
 
We ujui chochote bora ungekaa kimya hii serikali inawahujumi wafanyabiashara at the great extent.
 
We ujui chochote bora ungekaa kimya hii serikali inawahujumi wafanyabiashara at the great extent.
Sii Kweli madeni na matumizi mabaya ya mikopo nje ya biashara aliyokopea
Mtu.Unakopa kwa ajili ya biashara unaenda Jenga ghorofa la kuishi mikopo italipikaje?
 
Upo sahihi mkuu. Scandinavia mpaka wakati inafunga biashara yake haikuwahi ku compromise na standards za huduma zake! Siku zote walitoa huduma nzuri consistently.

Inawezekana miongoni mwa sababu za mambo yao kwenda kombo ni pamoja na mivutano ya mikataba kati ya wenye shares, gharama kubwa za uendeshaji, hujuma kwa sababu za kisiasa na pengine mikopo ya bank. Hivyo ndio vilikua vyanzo vya Scandinavia kuondoka kwenye biashara

Kwa maoni yangu aina ya kiwango cha huduma kilichokua kinatolewa na Scandinavia Express ndio ilikua ni standard inayotakiwa kwa watoa huduma ya usafirishaji abiria na yeyote atakayeweza kufanya vile atachukua asilimia kubwa ya soko
Scandinavia alijiingiza kwenye siasa wakati anamadeni, alidhani CCM itamlinda.
 
Scandinavia alijiingiza kwenye siasa wakati anamadeni, alidhani CCM itamlinda.
Nilizisikia hizo tetesi kwamba wanasiasa kadhaa walikua na magari yao kwenye ile kampuni. Minyukano ya kuwania Urais 2005 ilianza kutoa cheche za mifarakano na hatimaye miaka michache baadaye wakashindwa kuhimili misukosuko hiyo

Pia kwa watu waliokua karibu na Management ya Scandinavia Express wanasema ilifika wakati MD wao akaacha kufuata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wabobezi wa hiyo biashara waliyowaajiri kama ilivyokua awali na akawa yeye ndio anafanya kila kitu
 
Vile ni mjadala tu.

Scandinavia ibaki kuwa Scandinavia kuanza kuweka mawazo yetu au ya kusikia haiwezi kuleta uhalisia na kusaidia Dar Lux ikawa giant in transportation.
 
Hivi bado wapo?

Walinilisha kwenye kihoteli chao kiko pale Dodoma kabla ya Manyoni nikaharisha tumbo ikauma sina hamu nikawahama.

Huduma zilishaanza kua mbaya toka mwaka jana. Watu walikua wanasubiri basi stend safari ya sa 12 mnaanza sa 5.

Wale ndio biashara imefikia ukingoni.
 
Nilikuwa na mpango wa kwenda Mwanza kwa Dar Lux achanibadili mawazo nikwee Allys.
 
Back
Top Bottom