Wamiliki wa Kupatana na Zoomtanzania wanapataje faida

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,129
4,469
Hili swali nimekuwa najiuliza kuhusu hii biashara ya online market Tanzania baada kupatana kuingia kwenye hii biashara kuna vijana wengi nao wakaingia huku wengi zaidi kuishindwa hii biashara ukiingia huko playstore utajionea wewe mwenyewe wengi 'wamedondokea pua'

Tuachanae na hilo nachojiuliza mimi hawa Kupatana na Zoomtanzania pamoja nakufanikisha wazo hili wanapataje faida sababu naona gharama wanazotumia kufanya matangazo yao ni kubwa kuliko faida.

Je, na wao ni madalali?
 
Kuna matangazo yapo kwenye kundi la premium ambapo wewe muweka bidhaa unalipia kuweka tangazo lako, pia kwenye website zao kuna advertisement za kampuni mbalimbali ambapo hizo kampuni hulipia matangazo yao kuwekwa
 
Nimejaribu kuangalia hilo lakini nimegundua gharama za kufanya promotion bidhaa za wateja ni kubwa kuliko mapato wanayopata sababu ukiangalia hapo kwa makadilio wanayotumia kwa siku ni zaidi ya dollar 50
Watumiaji wanaotangaza bidhaa zao premium kuna matangazo kumi mwezi mzima bei ni elfu 30
sijui matangazo ya google wanaingiza kiasi gani
 
Mimi kwa mwez tu nilikuwa nawalipa 270,000 kila mwezi. Na sio mm pekee nna washakji zangu zaid ya 10. Hao ni wachache nnaowajua. Kuna watu zaid ya 100 wanalipa kama sisi upande wa zoom tanzania. Hapo hujaweka matangazo ya Google na mashirika.
 
Mfano kupatana wanala njia nyingi za kupata faida mfano wewe ukipost bidhaa yako ukiupgrade to primium unalipia pia kuna google AdSense unakuta kwenye app yako kuna matangazo mbalimbali kupitia watembeleaji hao wanalipwa na google kwa sabab google wanaweka matangazo yao
 
Back
Top Bottom