Wamiliki wa Hotel zilizoko ufukweni, marufuku kulipisha kiingilio

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
ee37b72ca3182652846a470a68bdee80.jpg
http://
Wamiliki wa Hotel za kitalii zilizoko katika fukwe mbalimbali nchini wamepigwa marufuku kutoza wananchi kiingilio wanapoenda kupumzika na kuogelea katika fukwe hizo.

Marufuku hiyo imetolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Mwanasheria wa NEMC, Manchari Heche alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, fukwe zote ni mali ya umma hivyo hakuna anayepaswa kuzitumia kwa biashara akiwatoza fedha wananchi.

“Fukwe zote ni mali ya umma kwa sababu kuna mipaka yake, hivyo kitendo cha kuwatoza wananchi fedha kuingia katika fukwe hizo ni kosa kisheria na wanaofanya hivo wanapaswa kuacha mara moja,” alisema Heche.

Baadhi ya hotel zilizoko katika fukwe hususan jijini Dar es Salaam zimekuwa zikitoza wananchi kiingilio cha kati ya shilingi 10,000 na 40,000 kwa kutembelea fukwe hizo kupunga upepo na kuogelea.

Katika hatua nyingine, Heche aliwataka wawekezaji wote waliojenga katika fukwe za bahari kuhakikisha wako umbali wa mita 60 kutoka Baharini, kinyume cha hapo nyumba na hotel zao zilizo chini ya umbali huo zitabomolewa.

Chanzo: Dar24
 
huu usanii wa viongoz wetu cjuh utaisha lin, mikwara kibao wakiitwa chemba tu, wakitoka watakwambia wapo kwenye mchakato mpk muda wa kupiga kura ufike.
 
Nimeweka habari hii asubuhi Moderator wakafuta.Siku hizi wamekuwa wapiga ramli.Habari niliileta ya moto toka jikoni kwenyewe.Aibu yenu,Futa na hiii
 
Huuu ni upuuzi mwingine wa CCM wameanza kutoza Leo hicho kiingilio??? Na huo ujenzi wa umbali wa mita sitini hamkuuona??? muwe mnafikiria japo kidogo nyie mawazir wa CCM,
 
NEMC acheni kutubomolea nyumba, hizo fukwe wala hatuna haja ya kuzitumia
 
Hamna kitu hilo tamko, utaingilia wapi kufika hizo bichi zao wakati wameweka mageti
 
Mimi sidhani kama ni hivyo...hutozwi kuogelea unatozwa kutumia huduma za hoteli hiyo. Kwa mfano ukiweza kupaa angani ukatua baharini usawa na hiyo hoteli ya whitesands na kuendelea na mambo yako na baada ya hapo ukapaa ukaondoka zako hakuna mtu anayetakiwa kukuchaji. Ukitumia huduma nyingine zozote zilizowekwa na hoteli hiyo ni lazima ugharamie.

Mfano hai: Kule kigamboni kuna beach kama tatu zinafuatana..Kipepeo, Sunrise na South Beach..ukiweza kupita vichochoroni ukaingia baharini ukaogelea hadi usawa wa South beach hakuna mtu atakudai..na kwa kuwa zinapakana waweza kuendelea kuogelea usawa wa hoteli yoyote hapo.

Utakapotoka majini na kwenda kukaa umbali wa hizo mita 60 nje ya bahari (kisheria) au kutumia viti au chochote ambacho kiliwekwa na hoteli hiyo kwa ajili ya watu wake ni lazima utadaiwa.

Huo ni mtazamo wangu!
 
kutoa amri ni rahisi sana sasa kwenye utekelezaji ni ziro kabisa.
Hawa jamaa wanavyoongea utadhani wakati haya makosa yanafanyika wao walikuwa kwenye sayari nyingine na sasa wamerejea. Ukweli ni kwamba ndio hawa hawa waliotoa vibali na ndio leo wanatoa hizi amri, nchi haijawahi kuwa nje ya system iliyopo sasa!
Haya, kuna hekalu pale mbezi beach la Mbunge mmoja mwanamama (mch), kuna golden tulip, kuna sea cliff nk. Mbali na hizo hebu tupe mrejesho kama ile hoteli ya pale Msamvu Morogoro uvunjaji umefikia wapi.
Tanzania imeshaharibika na imeharibiwa na kikundi kidogo sana cha wafanya maamuzi (watwala na sio viongozi), yatakuwa ni makosa makubwa zaidi kuwaamini walioiharibu eti ndio wairudishe kwenye mstari. Kuiinusuru Tanzani inatakiwa ushirikiano wa wananchi wote kwa kupima uhalisia wa hoja husika na sio haya matamko na vitisho.
Kama ni fukwe basi serikali iimarishe ulinzi ili vibaka wasijipenyeze kwa maana hao wamiliki wa sasa ndio wanashughulikia usalama hivyo kuamua kudhibita wanaoingia na kutoka, mfano Yatch Club Masaki ambapo membership ni sehemu ya maisha.
 
Last edited:
...golden tulip, sea cliff, the bay, slipway, double tree by hilton...wote hawa wana either a garden o r bar just a few metres from the ocean.., velisas, mediterannio, giraffe ndio mpaka wana pier, newly built Ramada pa kulipia 40, belinda , jangwani sea breeze, landmark mbezi beach , ernomous white sands, beachcomber, kunduchi beach hotel and ledger plaza hotel.... Hii streach ya fukwe ni zaidi ya km 20.. Yetu macho kwenu NEMC na mamlaka husika.
 
Back
Top Bottom