Wamiliki wa Bajaji Dodoma, dereva nipo hapa. Natafuta kazi

Mzaleee

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
1,616
3,029
Wakuu kwema?

Baada ya ajira serikalini kuwa ngumu hasa kwa sisi wahitimu wa vyuo vikuu,niliamua kuingia veta kutafuta ujuzi mbadala na nimefanikiwa kupata leseni yenye madaraja yayoniwezesha kuendesha pikipiki,bajaji na magari chini ya tani tatu.

Nimekuja kwenu wanajamii forum hasa wakazi wa Dodoma na wamiliki wa bajaji nikiomba kazi ya udereva,nimependelea zaidi bajaji kwamaana katika kufuatilia nimeona inalipa vizuri kwa tajiri yaan mwenye chombo na pia mm dereva.

Hesabu kwa siku ni elf 20000 lakn pia inaweza kupungua kutengemeana na hali ya uchakavu wa chombo husika, lakn hata chombo kiwe kichakavu vipi haitapungua hesabu ya elf 10000 kwa siku ili mradi kiwe kinaweza kuingia barabarani bila shida.

Hii in fursa kwa wote si tu walio na bajaji kwa sasa lakn pia kwa waliokuwa wakitafuta namna au wazo bora la kuwekeza jijini Dodoma.

Asanteni sana..
 
Back
Top Bottom