Wamiliki majengo Posta itakula kwenu bila haya sasa

MIGUGO

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
2,131
3,912
Nimeona majengo mengi maeneo ya Posta yakiwa tupu hayana wapangaji yale ya NHC na watu binafsi kwa sababu kuu hizi nilizoziona;

1.Serikali kuhamia Dodoma hili kila mtu analijua

2."Old buildings" Majengo mengi yamekuwa chakavu ya miaka mingi hakuna renovation, Yanavuja (unatembea na mwavuli ndani ya ghorofa), umeme kukatika kila wakati na elevators mbovu.

3. Parking imekuwa janga kubwa sana.

4. Ongezeko la wilaya mbili Ubungo na Kigamboni

5. New buildings za Bagamoyo Road wengine huita "Silicon valley" ya Tanzania ambapo makampuni mengi ya IT na simu yamejichimbia huko.

6. Kila mtu Posta notion inaanza kupotea. Maana siku hizi watu binafsi na serikali wanawekeza nje ya Posta kama matawi ya banks, hospitals, na shopping malls.

7. Technology: E-business imefanya watu wasione umuhimu wa kurun premises ili watu waone bidhaa au wakutane.Tigo pesa M-pesa, Jumia, Alibaba, Kupatana, Simbanking.

Nini kifanyike?
i) Wamiliki wa majengo Posta punguzeni kodi. Nani aje kupanga jengo lina giza na ukungu kibao halafu unamtoza kwa dollars kadhaa kwa square metres na ni miezi sita Hadi mwaka.

ii) Modify majengo wekeni parking ground floor. (I am not engineer). Ili kuvutia wateja.

iii) Pangisheni makazi si lazima ofisi. Piga luku za kutosha kama jengo lina storeys 5 haina haja ya elevators. Msiweke bei za apartment za kutosha hela ya kawaida ya class flani. Chini mnaweka warden wa kusimamia.

iv) Ingieni ubia watu wamiliki vyumba au storeys.

v) OSHA na Fire brigade haya majengo hasa ya NHC hayana safety yaangaliwe. Unaweza kuta yana entry/exit moja na hakuna assembly point.

vi) Vunja vyumba tengenezeni kumbi watu wafanye sherehe na mikutano.

vii) Weka automatic back up generator

NB: Kuna majengo yale ya kabla ya Uhuru ni hazina naona yaendelee kuwepo.

Karibuni.

Screenshot_20191202-180904~2.jpeg
 
Hapo kwenye kumbi za harusi nimekubali mkuu kama kuna sehemu iliobaki watu wanapiga hela ni hapo yani kumbi za harusi mfano unataka uoe mwakani mwezi wa 6 unaweza usipate hadi hivi tunavyoongea...
 
Nimeshangaa weekend hii ilopita Mhe.Majaliwa anawaambia NHC,Watumishi Housing wawapangishe wanafunzi majengo ya kijichi na Kigamboni kama sikosei wakati Posta karibu tu kuna majengo chungu zima tupu.

Land ladies and lords are not creative enough.
Its constructive ideal kwa kweli
 
Ishu hapo ni kupunguza kodi...makampuni mengi ya kati wanakodi nyumba za chini mikocheni, kijitonyama, sinza na mbezi karibu na mji na bei ni rahisi nyumba kwa mwezi laki 8 mpaka milioni moja na nusu hamna kampuni inataka kulipa dola 3000 kodi kipindi hichi
 
Aisee nimetafuta fremu Posta nikapata ila ilihitajika milioni 12 kwa miezi sita na mie ningeweza kulipa kwa miezi miwili nikashindwa. Cha kushangaza mpaka leo zile fremu mbili karibu na mtaa wa imala seko supermarket ziko tupu na ni zaidi ya miezi tisa sasa

Kuna nyingine hapa karibu na askari monument imepakana na S H Amoni na nimeifatilia nayo board ya hilo jengo wameshikilia million 3 per month. Na aliyekodi hiyo fremu ya duka la vitabu ambayo imefungwa zaidi ya mwaka sasa kaishindwa na wanasubiri eti waje au aje kuilipia ile kodi anayodaiwa, wakati ni zaidi ya mwaka sasa imekaa tupu


Kuna fremu karibu na I & M Bank pale maktaba square imeandikwa for rent, sasa almost a year now. Kwa kweli hata ma bank yameshindwsa kurent ile space

Posta biashara yenyewe imekuwa changamoto na mzunguko umepungua kwani ofisi nyingi zimehamishwa. Kwa kweli inapendeza kuwa kuna watu wanaona haya matatizo, Posta imechoka
 
Ishu hapo ni kupunguza kodi...makampuni mengi ya kati wanakodi nyumba za chini mikocheni, kijitonyama, sinza na mbezi karibu na mji na bei ni rahisi nyumba kwa mwezi laki 8 mpaka milioni moja na nusu hamna kampuni inataka kulipa dola 3000 kodi kipindi hichi
Yaani real estate agents hawaoni fursa hii.Mfano majengo kama
Agip hotel ya zamani,
Peacock hotel
wizara ya katiba na Sheria(Lina ocean view nzuri Kwa hotel)
kitega uchumi,
sukari house,
JM mall,
NSSF house

nimetaja machache.
 
Kuna jamaa namfahamu Ana ofisi opposite na cbe mitaa Ile alikuwa anapangisha 1.5m kwa mwezi Ila Sahv amekaa sana frame yake bila kupata mpangaji nkamwambia ashushe bei juzi juzi katoka kuniambia Sahv hata mtu akija na laki 7 anapangisha

Ova
 
Gily, Wazee wanataka hela kubwa wakidhani Posta inalipa kama zamani.Pale IPS building pakopako Tu.
 
Dar sasa Hivi itarudia jina lake la mzizima maana panaanza kuwa zzzzz Posta lakini.
Kuna jamaa namfahamu Ana ofisi opposite na cbe mitaa Ile alikuwa anapangisha 1.5m kwa mwezi Ila Sahv amekaa sana frame yake bila kupata mpangaji nkamwambia ashushe bei juzi juzi katoka kuniambia Sahv hata mtu akija na laki 7 anapangisha

Ova
 
Back
Top Bottom