Wamiliki gazeti Tanzanite wafungua kesi kudai wamedukuliwa na kuchapisha habari zisizo na maadili, sio wao walichapisha

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Yaani mmoja wa wamiliki wa jarida hili ni Musiba wa ccm, ili kukwepa adhabu naona wameshauriwa wafanye ivyo kwa kuandika ujinga.

Hii imekuja muda mfupi baada ya Ofisi ya Habari Maelezo kuwaita gazeti la Tanzanite kwa kuandika habari inayokinzana na maadili ya uandishi. Soma =>Gazeti la Tanzanite kitanzani kwa habari zisizo na ueledi. Waitwa ofisi ya Habari Maelezo kujieleza


IMG-20180304-WA0020.jpg
 
Hahaha....lingekuwa ni tz daima hata kama lingedukuliwa na kutoa taarifa police.. Sasa hvi ofisi zingekuwa chini ya ulinzi na upekuzi kufatia huku laptomp na vitendea kazi vikibebwa kw ajili ya uchunguzi... Ila kwa kuwa mali ya mtu mwenye mamlaka ya kutangaza watu hatari wa nchi nadhani ndio imetoka hivyo.
 
Kushadadua vituko vya mtu mwenye mtindio Wa ubongo kama msiba ni kupoteza muda. Mtu ambaye mume wake mwenyewe amemchoka kwa upuuzi Wake (Anajua namaanisha nini).
 
Hawa bado wana makosa tu hata kama wamedukuliwa, ni kwamba hiyo habari ni kweli wao ndiyo wameaiandika (maana hawajakanusha kwamba hawahusiki nayo) ila usambazaji wake mtandaoni ndiyo umefanyika bila kibali cha wahusika. Sasa kwanza lazima wapambane na kujibu kuhusu maudhui ya gazeti ndipo hapo habari ya kudukuliwa ianze kusikilizwa. Mwisho wa siku huyu Musiba ni kwamba kashajikatia tamaa na maisha, kaingiwa na frustrations za maisha, anatafuta kuwa sawa kwa kufanya haya anayoyafanya akifikiri ndiyo dawa ya ugonjwa wake. Amekuwa fedheha na aibu kwa familia yake na jamii ya watu wangwana. Hawa ni aina na watu walio radhi kuua hata mtu kwa ajili ya kupata vyeo au pesa ni matokeo mabaya ya frustrations .
 
Back
Top Bottom