Wamewafungulia Kesi ya Uhujumu Uchumi Wenzao, Kwa nini na sisi tusiwafungulie na wao pia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamewafungulia Kesi ya Uhujumu Uchumi Wenzao, Kwa nini na sisi tusiwafungulie na wao pia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gagurito, Apr 23, 2012.

 1. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Taarifa ya Waziri wa Kilimo ndg. Maghembe inasema kuwa wale waliochakachuwa mbolea kwa kuchanganya na chumvi wamechukuliwa hatua, kesi zipo mahakamani na wanatuhumiwa kwa kuhujumu uchumi.
  Kifupi nimeshangazwa sana, kwani Maghembe ni mmoja kati ya Mawaziri waliopo kikaangoni kwa tuhuma za kutokuwajibika na ufisadi pia. Sasa kama wameweza kuwachukulia hatua wenzao kwa kesi ya kuhujumu uchumi kwa nini na sisi tusiwafungulie kesi ya kuhujumu uchumi wetu Mawaziri wote wanaotajwa kuhusika kwa ufisadi wao endapo watathibitishwa?
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa makini nimetega sikio kumsikiliza Pinda, macho kideoni!
   
Loading...