Wametusaidia fedha, sera, utaalamu: Tumeshindwa sasa wanatekeleza wenyewe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wametusaidia fedha, sera, utaalamu: Tumeshindwa sasa wanatekeleza wenyewe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, May 9, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Uchafu, yaani namaanisha UCHAFU kweli kweli

  Yaani binadamu kufurahia maisha, kula na kulala katikati ya takataka, uozo, harufu mbaya, maji yenye kinyesi na mikojo na wadudu kama inzi bila wasiwasi!

  Tumeshindwa, tena tumeshindwa halafu tukashindwa kusema kwamba tumeshindwa. Tumeshindwa kufikiri, tukashindwa kupanga na kutekeleza. Yaani tumeshindwa kabisa, anayebisha anyooshe mkono.

  Kwanza wahisani wanatupatia pesa kupitia mfuko mkuu wa bajeti ya serikali na miradi mbali mbali. Tunazitafuna kama mchwa!

  Kisha wanatusaidia ushauri wa kisera na hata utaalamu wa hapa na pale. Hata kama ushauri wao ni mbovu basi mipango yetu wenyewe mizuri yenye tija ni ipi?

  Yote yakashindikana bado hata mazingira tunamoishi ni hatari kutokana na uchafu unaotishia afya zetu na kuongeza gharama ya huduma za afya. Uchafu ambao pia unatishia maisha ya wahisani wanaoishi humu.

  wakaamua basi bora wasafishe wenyewe, kama ilivyo kwenye hii picha hapa chini, na wataendelea kufanya hivyo

   

  Attached Files:

 2. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Kwa sababu viongozi wetu hawana aibu watalichukulia tukio hili kama la kawaida na maisha yataendelea kama kawa, lakini kusema ukweli hii ni aibu tosha kwa meya wa Dsm na watu wake... wangekuwa wanafanya kazi kwa vitendo namna hii tusingeweza kufedheheshwa namna hii!
   
 3. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu Mtemi Kazwile kunisaidia kuongeza ukubwa wa picha
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kinachokera zaidi ni pale viongozi wetu wanapokwenda kuwashukuru kwa kusafisha mitaa wakiwa na suti za dubai na wanatumia VX V8

  Kinyaa kabisa wallahi.....

  Waweza kuta waziri anakwenda kufungua kisima cha milioni saba akiwa na magari saba yenye thaman ya mamia ya mamilioni na allowances tu za timu hiyo kuzidi milioni sitini

  tena kinyaa zaidi ni pale ambapo wanatuandikia sera, wanatekeleza, wanatathmini na kisha wanaturipotia, sie tuko bize na makongamano
   
 5. m

  mkulimamwema Senior Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ndio uozo wa CCM na serikali yake eti MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA-UJUHA MTUPU
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwenye tv nilimuona mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni akiwashukuru wahisani hawa kwa kuwasaidia kusafisha maeneo! Pia akatupiwa swali ni kwa nini Manispaa imeshindwa kusimamia usafi akajiumauma tu habari ikaisha na waandishia hapo
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ndio bongo hiyo.... yeye anashukuru badala ya kufanya nao kazi na kuwaambia next month tutafanya wenyewe hata kwa bakora
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hali inatisha!
   
 9. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hao mabalozi wamekosea, wangeenda kuanza kazi ya usafishaji pale magogoni. Mkuu wa nchi mwenyewe anaishi kwenye uchafu titiri
   
 10. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  dah hii ni aibu sasa!! thanx media kwa hili..!!labda inaweza ondoa tongotongo
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu ukifuatilia nyuuzi zote kuhusu hii inshu, media haikuripoti kama aibu bali kama sifa kwamba maagizo ya Makamu wa rais kufanya usafi jumamosi ya kwanza ya mwezi yametekelezwa, hata wahisani nao wamejitokeza. Ndiyo maana leo nikaona nililete hapa janvini
   
 12. m

  mob JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Samahani tuliowapa dhamana wanafanya kazi kwa mazoea ndo maana kazi na shughuli za maendeleo hazifanyiki,mathalani tumuulize afisa afya wa manispaa anafanya kazi gani au amekaa tu ofisini na kwenda kukamata akina mama lishe apate hapo fedha za kujikimi au
  hawa viongozi yaani tuliowachagua na watendaji wa kuajiriwa wameshinda kufikiria kuhusu kesho wao wajikita tuu katika kudai posho za vikao na makongamano ambayo hayaishi ili tu wajichumie kodi zetu. Ivi zile harufu pale magogoni zitaisha lini au wenzetu wa usafi na mazingira hawazioni au wenzetu wa afya walioko takribani hatua 300 hawazisikii
  ushauri wangu WENYE DHAMANA WAache semina na makongamano yanayomaliza fedha na fedha zielekezwe kwenye vitu vitakavyoleta tija kwa taifa letu, WApunguze kujifungia kwenye viyoyozi bali twende mitaani WAkafanye kazi zenye tija kwa jamii
  asante
   
 13. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Hawa viongozi wetu sijui kama wako sawa,mtu uliye sawa huwezi kufurahia ujinga wa hali hii
   
 14. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  CHADEMA wasusiwa uchafu Sinza B  na Efracia Massawe
  BAADA ya Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda, kuwataka wakazi wa Manispaa hiyo kutunza mazingira, jitihada hizo zimepingwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sinza (B) kwa kile kinachodaiwa sababu za kisiasa.

  Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti wakazi hao walisema Aprili 9 mwaka huu walihimizana kufanya usafi wakiongozwa na viongozi wa mtaa huo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiunga mkono jitihda za serikali kutunza mazingira.

  Kwa mujibu wa wakazi hao, taratibu zote za kuufahamisha uongozi wa serikali ya mtaa huo juu ya azma yao zilifanyika lakini uongozi huo wa mtaa uliwanyima mifuko ya kuhifadhi taka watakazokusanya ili kuzipeleka maeneo husika kwa taratibu za kila siku.

  "Tumekusanya uchafu huu unaouona hapa na maeneo mengine lakini gari lilipofika uongozi wa serikali ya mtaa ulituambia tuwaambie CHADEMA watutafutie gari la kuzolea taka hizi kwa kuwa wao ndio walioratibu suala hili la usafi… kwa kweli inatusikitisha sisi wananchi kuona mambo ya msingi yanashindwa kutekelezwa kwa sababu za kisiasa," walisema wakazi hao.

  Katika maelezo yao walisema fedha za kuchangia kwa ajili ya usafirishaji wa taka hizo zilikataliwa na uongozi wa mtaa na kuwaacha katika hali ya kutofahamu siku uchafu huo utakapoondolewa.

  Aidha Tanzania Daima ilimtafuta kwa njia ya simu mwenyekiti wa mtaa huo Dk. Kessy ambaye alikataaa kulizungumzia suala hilo kwa madai kuwa suala hilo ni la watu binafsi lakini taka zitaondolewa wakati wowote.

  Naye Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mwenda alikiri kufahamu juu ya kadhia ya uchafu na kusema endapo suala hilo linafanywa kisiasa wahusika hawawatendei haki wananchi.
   
 15. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Ndio hao hao ila sisi tumo tunahimiza kupenda biadhaa zetu za nyumbani a lakini hakuna anayediriki kushonesha japo nguo ya kulalia kwa fundi wa mtaani au kwa desinger wa tazania. Hakuna aliyetari kuchongesha japo pair pair moja ya kiatu kutoka kwa fundi wa mtaani. teh teh teh

  Waulize wabunge kama suti wanazovaa japo zimechangia ajira maimboni mwaoooo.......... Kwa hili wapinzani na wana CCM wote sawa tu.

   
 16. k

  kimandolo Member

  #16
  May 9, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uchizi mtupu, HATA KUFAGIA NA KUZIBUA MITARO TUNASUBIRI MABALAOZI? Kweli hawa watu wanahaki ya kutuona cc na WEHU, I WISH WAFUNGUE KLINIC MAALUM YA KUPIMA AKILI ZA VIONGOZI WETU
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu umetoa wazo zuri sana. Wasimamishe misaada ya bajeti serikali watusaidie kutibu akili za viongozi wetu kwanza. Wakipona ndo waendelee kuwapa misaada
   
 18. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  kUMBE WENYEWE-SIRIKALI ILIONA HII KITU KAMA SIFA ....OMG!!IMPLICATION NA IMPACT YAKE NI KUBWA KULIKO WANAVYOFIKIRIA..!!
   
 19. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Eti balozi anatuma picha na ripoti kwa rais wake kuonesha anazibua mifereji ya maji machafu tz. Mawaziri wetu wako nchini kwake wanakula bata. Kwa nini kikwete hana mshipa wa aibu?
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  Mbona hii rahisi sana, Wapeleke Nyumbani kwa viongozi wa mtaa zitakazo baki wapeleke ofisi ya mtaa na zingine hivyohivyo kwa meya nyumbani na ofisini.
   
Loading...