Wameru na wazee waandamana wataka sioyi sumari mgombea wa ccm akatiwe rufaa tume ili ang'olewe

Sasa, hawa wazee wako upande gani? Cdm au ccm A? Kama siyoi ni kyasaka na ni mteremko kwa nini cdm wanataka kumuondoa? Wanataka kupambana na kina sarakikya na kaaya ili iweje sasa? Chochote cdm mnachofanya muwe makini kuhusiana na huo uchaguzi. Na kama hao wameru wanaomuwekea siyoi pingamizi ni ccm, basi muwe makini maana mtajikuta mnasaidia ccm
 
Comrades plan A ni kwa sanduku la Kura then hiyo ya pingamizi ifuate kama mjuavyo tena maamuzi mengi huwa ya kuibaka Haki toka kwa Vibaraka wa CCM Vinginevyo hii ni Vita Takatifu tusiwe na Shaka tujiandae tu kuirith pepo
VIVA CDM
 
Sasa, hawa wazee wako upande gani? Cdm au ccm A? Kama siyoi ni kyasaka na ni mteremko kwa nini cdm wanataka kumuondoa? Wanataka kupambana na kina sarakikya na kaaya ili iweje sasa? Chochote cdm mnachofanya muwe makini kuhusiana na huo uchaguzi. Na kama hao wameru wanaomuwekea siyoi pingamizi ni ccm, basi muwe makini maana mtajikuta mnasaidia ccm

ccm kupitia mwigulu hawakawii kuwa na tindikali, hatutaki tufike huko, sioi analizwa msiba mwingine mapemaaaa kabla hajasahau wa baba yake.
 
EL hajapata taharifa tu, maana yawezekana akacha matibabu huko aliko ili arudi kuokoa jahazi la mkwe wake.
 
Amini nawaambieni hili lina mkono wa CCM wenyewe!! Sioyi achomoki!!!
 
mimi hapa mbona sielewi...yaani hawa wazee(wa ccm) wanataka cdm wakate rufaa ili sioi sumari asigombee...na asipogombea sioi agombee sarakiya kwa manufaa ya chadema au kundi la sarakiya ? hapa cdm wanatakiwa watulize bolu, ccm wenyewe wachinjane...!
 
Afu mambo yakiwa moto kutishia Sioyi kuchomolewa kuna Plan B baada ya mtu kusarenda.CDM be SMART not CLEVER!!
 
Simtetei Sioi, lakini nadhani inabidi tujiulize na tuangalie katiba ama sheria za kenya zinasemaje juu ya mtu aliyezaliwa katika ardhi yao huku wazazi wake wote wakiwa sio Raia kama ilivyo kwa Sioi ambaye amezaliwa Kenya lakini wazazi wake sio wakenya. From there tutakuwa na ground nzuri ya ku-judge
Mkuu, unaandika mwenyewe haya madudu? Hivi kuna haja gani sasa ya kuwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iwapo kuna katiba za nchi nyingine?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania

(67 1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtuyeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwakuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wamiaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma nakuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa nachama cha siasa;
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe yaUchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakamayoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyoteya Serikali.

(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwakuwa Mbunge-
(a) ikiwa mtu huyo anao au kwa hiari yake amejipatia uraia wa nchi nyingine yote; au
(b) ikiwa kwa mujibu wa sheria inayotumika katikaJamhuri ya Muungano imethibitishwa rasmi kwambamtu huyo ana ugonjwa wa akili; au
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyotekatika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu yakifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidimiezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote,vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wauaminifu; au
(d) ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tareheya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewaadhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovuwa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya Maadili yaViongozi wa Umma;
(e) bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoniyake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wenginena kushiriki shughuli za umma kwa mujibu wa sheriaza nchi, ikiwa mtu huyo si mwanachama na mgombeaaliyependekezwa na chama cha siasa;
(f) ikiwa mtu huyo ana masilahi yoyote katika mkataba waSerikali wa aina yoyote aliyowekewa miiko maalumkwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na iwapoamekiuka miiko hiyo;
(g) ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisamwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri yaMuungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais awezaau anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu waKatiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;​
(h) ikiwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge
 
Ngoja tuone hii move mwisho wake..lakini nadhani ni mwanzo mzuri sana kwa CHADEMA na wananchi wapenda haki wa taifa hili.
 
Hapo kwenye RED nona ngoma sasa nzito wala si maatani tena.

Wazee wa Meru na kundi linalodhaniwa kuwa na la KAMBI YA SARAKIKYA na ELISHILIA KAAYA wamesema hakuna ubishi SIOI SUMARI amebebwa kwa nguvu ya hela. Watu wake wengi tu wameshikwa katika kuhusishwa na rushwa kwenye kura ya maoni.

Wazee hao ambao ndio wasemaji wa kundi hilo wamesema haya mara baada ya viongozi wa chadema kumaliza press conference huko usa river na wamewataka viongozi wa chadema wasimlazie damu huyo mtoto wamuwekee pingamizi na wao wako tayari kutoa ushahidi wa rushwa hizo maana ni kweli hela imetembea hakuna ubishi maana hata ndani ya ccm wanajua hivyo.

Wazee wamesema na wameapa kamwe MGENI WA MERU hawezi kuongoza. Wamewataka chadema wakate rufaa haraka atolewe maana kumpambanisha SIOI na Joshua Nassari ni kupoteza muda bure.
 
Simtetei Sioi, lakini nadhani inabidi tujiulize na tuangalie katiba ama sheria za kenya zinasemaje juu ya mtu aliyezaliwa katika ardhi yao huku wazazi wake wote wakiwa sio Raia kama ilivyo kwa Sioi ambaye amezaliwa Kenya lakini wazazi wake sio wakenya. From there tutakuwa na ground nzuri ya ku-judge
mkuu
binafsi si mwanasheria si ifahamu katiba ya kenya ila kuna mdau kesha tueleza kuya yetu inamtaka mtu aliyezaliwa pengine aukane uraia wa huko alikozaliwa kitu ambacho sioi hajafanya je huone kwa vyovyote hata kama ya kenya itatamka wazi kutomtambua mtu aliyezaliwa kwao na wazazi wasio raia bado yeye alipaswa kutii hii yetu?nipo tayari kukosolewa
 
Leo Mgombea wa CHADEMA Joshua Nasari,amewasilisha pingamizi kwa Mkurugenzi wa uchaguzi,dhidi ya mgombea wa CCM.Pingamizi hilo ni kuhusu uraia wa Sioi,katika fomu zake Sioi aliandika kuwa alizaliwa Thika nchini Kenya.Kwa mujibu wa sheria za uhamiaji kuna urai wa aina tatu,1.Wa kuzaliwa,2.Kujiandikisha,na 3,ni kupata uraia kwa kurithi kwa aliezaliwa nje nchi,na wazazi wote kuwa raia wa Tanzania.Kifungua cha 6 cha sheria ya uhamiaji,kinamtaka aliezaliwa nje ya nchi kuukana nchi aliyozaliwa na kukiri uraia wa Tanzania.
Sioi hakuwahi kuukana uraia huo,kwa mujibu wa barua ya Ofisi ya uhamiaji Arusha,kwenda kwa Mkuu wa mkoa,afisa uhamiaji aliyefahamika kwa jina la Namomba anamtaarifu RC kuwa wao kama uhamiaji hawana taarifa wala rekodi yeyote ya Sioi kuukana uraia wa Kenya

Mkuu, kumbe Sioyi Sumari, ni mkuki kwa Chadema, si mnasema kuwa mgombea wa Chadema anakubalika Arumeru, sasa kwa nini mnapoteza muda wenu?
 
Simtetei Sioi, lakini nadhani inabidi tujiulize na tuangalie katiba ama sheria za kenya zinasemaje juu ya mtu aliyezaliwa katika ardhi yao huku wazazi wake wote wakiwa sio Raia kama ilivyo kwa Sioi ambaye amezaliwa Kenya lakini wazazi wake sio wakenya. From there tutakuwa na ground nzuri ya ku-judge

Mkuu mbona unataka kutupigisha kwata hapa? Kwa nini tufanye mambo yetu kwa kuangalia sheria za Kenya zinasema nini? Je hiyo itatusaidiaje kujua uraia wa huyu jamaa? Tuangalie sheria zetu zinasemaje tu, period!!!!

Tiba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom