Wameru na wazee waandamana wataka sioyi sumari mgombea wa ccm akatiwe rufaa tume ili ang'olewe

chachana

Member
Aug 4, 2011
57
92
Wazee wa Meru na kundi linalodhaniwa kuwa na la KAMBI YA SARAKIKYA na ELISHILIA KAAYA wamesema hakuna ubishi SIOI SUMARI amebebwa kwa nguvu ya hela. Watu wake wengi tu wameshikwa katika kuhusishwa na rushwa kwenye kura ya maoni.

Wazee hao ambao ndio wasemaji wa kundi hilo wamesema haya mara baada ya viongozi wa chadema kumaliza press conference huko usa river na wamewataka viongozi wa chadema wasimlazie damu huyo mtoto wamuwekee pingamizi na wao wako tayari kutoa ushahidi wa rushwa hizo maana ni kweli hela imetembea hakuna ubishi maana hata ndani ya ccm wanajua hivyo.

Wazee wamesema na wameapa kamwe MGENI WA MERU hawezi kuongoza. Wamewataka chadema wakate rufaa haraka atolewe maana kumpambanisha SIOI na Joshua Nassari ni kupoteza muda bure.
 
Leo Mgombea wa CHADEMA Joshua Nasari,amewasilisha pingamizi kwa Mkurugenzi wa uchaguzi,dhidi ya mgombea wa CCM.Pingamizi hilo ni kuhusu uraia wa Sioi,katika fomu zake Sioi aliandika kuwa alizaliwa Thika nchini Kenya.Kwa mujibu wa sheria za uhamiaji kuna urai wa aina tatu,1.Wa kuzaliwa,2.Kujiandikisha,na 3,ni kupata uraia kwa kurithi kwa aliezaliwa nje nchi,na wazazi wote kuwa raia wa Tanzania.Kifungua cha 6 cha sheria ya uhamiaji,kinamtaka aliezaliwa nje ya nchi kuukana nchi aliyozaliwa na kukiri uraia wa Tanzania.
Sioi hakuwahi kuukana uraia huo,kwa mujibu wa barua ya Ofisi ya uhamiaji Arusha,kwenda kwa Mkuu wa mkoa,afisa uhamiaji aliyefahamika kwa jina la Namomba anamtaarifu RC kuwa wao kama uhamiaji hawana taarifa wala rekodi yeyote ya Sioi kuukana uraia wa Kenya
 
Wameshindwa kuyatoa Magamba,sasa CDM tunawaonyesha jinsi yanavyoweza kutolewa bila kutumia kelele nyiingi kama za Vuvuzela.
 
KIMENUKA kwa Siyoi. Sababu za msingi kabisa kuweka pingamizi, tusubiri kuona sheria za nchi zikibakwa kwa mara nyingine kumlinda mwana CCM. Pia tuna records za ishu ya Hussein Bashe kujazilizia ushahidi

Bahati mbaya Kamanda Nanyaro wachangiaji wengi wako busy na thread ya ufuska wa Malima wamesahau kabisa Arumeru, ahsante kwa taarifa narudi tena kule kwa Malima
 
Mi napenda pingamizi lishindwe ili atolewe jasho uwanjani. Ili siku nyingine afikirie mara mbili kabla ya 'kurithi vya baba'.
Yatima hadhulumiwi, ila anafunzwa!
 
Tatizo hawa jamaa kwa kuwa 'serikali ni yao' hawakosi kuyachakachua mambo kwa kadri wanavyotaka, kesho tutaambiwa alishaukana uraia wa Kenya siku nyingi!Maana hufanya mambo yao kulingana na upepo unavyowatuma-eg kama Masauni wakat ule walimwambia agombee, na akashinda uenyekiti wa UVCCM na umri wake mkubwa; then walipooana ni tatizo wakaibuka na kusema ana umri usio halali kwa uognozi huo..hawakosi kuchakachukua na hio la huyo Sioi-kama ni kweli hajawahi kukana uraia wa kENYA (Thika)!
 
Leo Mgombea wa CHADEMA Joshua Nasari,amewasilisha pingamizi kwa Mkurugenzi wa uchaguzi,dhidi ya mgombea wa CCM.Pingamizi hilo ni kuhusu uraia wa Sioi,katika fomu zake Sioi aliandika kuwa alizaliwa Thika nchini Kenya.Kwa mujibu wa sheria za uhamiaji kuna urai wa aina tatu,1.Wa kuzaliwa,2.Kujiandikisha,na 3,ni kupata uraia kwa kurithi kwa aliezaliwa nje nchi,na wazazi wote kuwa raia wa Tanzania.Kifungua cha 6 cha sheria ya uhamiaji,kinamtaka aliezaliwa nje ya nchi kuukana nchi aliyozaliwa na kukiri uraia wa Tanzania.
Sioi hakuwahi kuukana uraia huo,kwa mujibu wa barua ya Ofisi ya uhamiaji Arusha,kwenda kwa Mkuu wa mkoa,afisa uhamiaji aliyefahamika kwa jina la Namomba anamtaarifu RC kuwa wao kama uhamiaji hawana taarifa wala rekodi yeyote ya Sioi kuukana uraia wa Kenya

Simtetei Sioi, lakini nadhani inabidi tujiulize na tuangalie katiba ama sheria za kenya zinasemaje juu ya mtu aliyezaliwa katika ardhi yao huku wazazi wake wote wakiwa sio Raia kama ilivyo kwa Sioi ambaye amezaliwa Kenya lakini wazazi wake sio wakenya. From there tutakuwa na ground nzuri ya ku-judge
 
Mzee Mwana Mpotevu sisi hatuendeshwi na sheria za Kenya.
 
Simtetei Sioi, lakini nadhani inabidi tujiulize na tuangalie katiba ama sheria za kenya zinasemaje juu ya mtu aliyezaliwa katika ardhi yao huku wazazi wake wote wakiwa sio Raia kama ilivyo kwa Sioi ambaye amezaliwa Kenya lakini wazazi wake sio wakenya. From there tutakuwa na ground nzuri ya ku-judge

sisi hatuongozwi kwa sheria za kenya, anatakiwa afate sheria za nchi. Bado mi napenda rufaa ishindwe ili huyu jamaa aone utamu wa 'mirathi ya hatari'.
 
Wazee,wamama,wababa,vijana wa ARUMERU simameni kidete msije mkaweka kiongozi alitumia pesa kushinda kula za maoni,itawagharimu baadaye mkimpa kula huyu mtu sio mwingine ni SIOI, Mtoseni hatawatetea mbali atanza kurudisha pesa yake aliyotoa kwa njia za RUSHWA kupata ubunge,MDHITHUBUTU kumchagua.
 
Labda mmeru wewe ndio umeandamana kichwani kwako. kama wameandamana na wewe ulikuwa shuhuda toa picha. propaganda kama hizi haziwezi kuwa ushindi. Ujue kila mnavyojipa moyo mkishindwa ndio nguvu zinawapotea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom