Wamegundua hawatashinda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamegundua hawatashinda?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 22, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,602
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  SERIKALI imehamanika. Vijana wanasema imepaniki! Nawatazama usoni, nasikiliza kauli zao; nachunguza matendo yao.Ni hamaniko la kisiasa. Linatokana na mkanganyiko unaoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho kinapita katika wakati mgumu kuliko wowote tangu kiasisiwe.

  Hamaniko hili la CCM na serikali linawafanya watawala na wapambe wao wawe wakali mithili ya dume la ng'ombe lililojeruhiwa. Wanataka kufa na mtu.

  CCM hakijawahi kujeruhiwa kisiasa kwa viwango hivi. Hakina uzoefu wa kuona watu wakichukua fomu kugombea uongozi wa ndani ya chama, halafu wanaingia mitini – hawarudishi fomu. Inatokea sasa!

  Hakina uzoefu wa kuona baadhi ya viongozi wanaotumainiwa wakiachia ngazi na kutangaza kutogombea tena nafasi hizo, huku wakijua kuwa wana uwezo wa kushinda. Inatokea vijijini.
  Ni wakati mgumu kwao, kwa maana kwamba viongozi wengi wa kuchaguliwa katika nafasi za uwakilishi, wanahesabu siku wamalize "wajivue gamba." Na wanasema wazi; wanasikika juu ya mipango yao hiyo.

  Haijawahi kutokea viongozi wa juu wa CCM kulalama kila mara mikutanoni na kwenye vyombo vya habari, kwamba "hata wakihama wanachama wote, nitabaki peke yangu, na CCM haitakufa." Imetokea sasa.

  Mambo haya yanayotokea kwa CCM sasa, tumekuwa tunasikia yakiwatokea wapinzani. Wamekuwa wakiumana na kuumizana, CCM inapita katikati yao.
  Sasa hivi wana CCM wanaumana na kuumizana, wapinzani wanapita katikati. Ni wakati mgumu kwa CCM; na hawawezi kuficha hili.

  Ndiyo maana unakuta viongozi wa serikali wanaungana na viongozi wa Bunge kutukana wapinzani, na kutetea matusi hayo. Hasira za viongozi wa Bunge dhidi ya wabunge wa upinzani, hasa wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi, ni ishara ya uchovu wa watawala.

  Hoja zimefika kikomo. Sasa wameamua kutumia mabavu. Lakini naona na Mungu hayuko upande wao. Maana wakifunika hili, linazuka lile.

  Kwa wanaoona mbali, hasira hizi za serikali zinajenga hasira kubwa zaidi kutoka kwa wananchi. Iwapo wananchi wataamua kuonesha hasira hizo, kwa wakati wao, serikali itabaki kujilaumu kwa kuwapatia wapinzani wake silaha nzito.

  Si mimi tu ninayeliona hili. Hata baadhi ya wana CCM makini wanaona. Na baadhi yao wanasema. Majuzi tu, nimekutana na wanachama na viongozi wengi wa CCM ambao wanaamini kwamba chama chao kipo njia panda. Wanaona nyuma. Hawaoni mbele.

  Mmoja aliyeniambia kwamba anaona mbele, amesema anaona damu! Ana nafasi nzito katika mfumo wa utawala wa sasa wa nchi. Ameshiriki kuusimika mfumo huu; na amekuwa akiulinda.

  Lakini sasa amefika mahali naye amepoteza imani na mfumo ule ule aliouzaa. Anasema, kwa jinsi anavyoona mambo, zamu ya CCM kushinda uchaguzi na kutawala nchi hii kwa ridhaa ya wananchi imepita.

  Anaona kama wapinzani wanakaribia kuiondoa CCM madarakani. Hata hivyo, anadhani kwamba CCM hawako tayari kuwapisha watawala wapya.

  Anasisitiza: "Naona kama hatutaweza kushinda uchaguzi. Nguvu ya CHADEMA inazidi kuongezeka; wanaweza kushinda. Lakini sioni kama sisi tupo tayari kuondoka na kuwaachia nchi. Na kama hili litatokea, CHADEMA nao hawatakubali; damu itamwagika..."

  Ana wasiwasi wa ziada. Hajui kama CHADEMA wamejiandaa vya kutosha kuziba ombwe la uongozi linaloonekana sasa. Anakiri kwamba hawajui vema viongozi na wataalamu wa mikakati katika CHADEMA.

  Anajua chama kinakubalika kwa wananchi; hivyo kinaweza kushinda kwa kura. Hofu yake ni kwamba iwapo CHADEMA hawatakuwa wamejiweka tayari mapema kuongoza nchi, CCM inaweza kushindwa ikakubali kuachia madaraka, lakini wao wakaingia kwenye giza nene.

  Silazimiki kukubaliana na kila hoja yake. Lakini dalili zote zinaonesha kwamba watawala wameshajua kwamba mambo si mazuri kwao, na sasa wanagombana na ukweli kwamba inawezekana wakaweka mgombea urais ambaye ndiye atakuwa wa kwanza kushindwa.

  Wanagombana na hisia kwamba huenda Rais Jakaya Kikwete akakabidhi nchi kwa kiongozi asiye wa CCM. Wanaumizwa na ukweli kwamba hadi sasa hawajakubaliana kimkakati ni nani ateuliwe na chama chao kupeperusha bendera ya CCM 2015.

  Wanasukumwa na tetesi zilizozagaa kwamba Rais Kikwete anaona ni heri aikabidhi nchi kwa wapinzani kuliko kwa wagombea wa CCM asiowaamini wala kuwakubali. Kama atafanikiwa au la, ni suala jingine.

  Na hisia zao zinachochewa na hali ya mgawanyiko mkubwa wa makundi ndani ya CCM, unaozidi kupanuka kadiri wanavyopiga hatua katika uchaguzi wa ndani.
  Kinachowachoma zaidi ni habari kwamba wanachama wengi wa CCM, wakiwamo viongozi wao, wanajipanga kuhamia upinzani.

  Nimeshuhudia katika baadhi ya maeneo, wanaondolewa mabalozi wa nyumba 10 wa CCM, wanasimikwa wa CHADEMA. Nimeshuhudia katika baadhi ya vitongoji, uongozi mzima unahamia CHADEMA.

  Nimezungumza na baadhi ya viongozi wa CCM ambao wanasema walishaacha siku nyingi kuzungumzia "imani, ilani na maadili ya CCM." Wanachofanya ni kuzungumzia matatizo ya wananchi, si kusifia au kujibanza kwa CCM na serikali.

  Wanaona aibu, maana wanajua kwamba wananchi wana uelewa mpana wa mambo hayo kwa kutazama matendo ya viongozi wa CCM katika maeneo yao.
  Wana CCM wa vijijini wanatambua kwamba kwa sehemu kubwa, sifa mbaya ya chama chao haitokani na wao, bali viongozi wa CCM wanaoitwa vigogo; ambao wamepewa dhamana ya uongozi wakaitumia vibaya kujinufaisha na kuumiza wananchi.

  Na katika mazingira ya Katiba mpya inayoandaliwa, kama kweli itakuwa kama wananchi wanavyotaka, hakuna dalili za CCM kubaki madarakani.

  Ndiyo maana baadhi ya wana CCM wanaojua maana ya madai ya Katiba mpya wamekuwa wakigoma kuunga mkono mchakato huu, kwa kuhofia kwamba ukifanikiwa ndiyo utakuwa mwisho wa utawala CCM.

  Na kwa kuliona hili, CCM ambao kwa miaka zaidi ya 15 wamekuwa wakipinga hoja ya wapinzani kuhoji matokeo ya kura za urais mahakamani, sasa nao wameibuka na pendekezo hilo.

  Walianza wakikataa Katiba mpya. Baadaye wakalazimishwa na rais, wakakubali kwa shingo upande. Sasa wametafakari na kukubaliana kwamba Katiba mpya iseme wazi kwamba mgombea urais atakayeshinda apingwe mahakamani.

  Mtu mmoja akaniuliza: "Ina maana wamegundua kwamba hawatashinda urais?"


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,225
  Trophy Points: 280
  ccm inajimaliza yenyewe, saa nnyingine ukisikiliza maneno yao viongozi na wanachama unaweza kudhani wanajimaliza makusudi......sijui ndo kulewa madaraka?????
   
 3. s

  sangija Senior Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu kwa uchambizi wa kina na kutoa picha ya hali halisi,ni ukweli usiopingika kuwa CCM siku zako zinahesabika iwe isiwe kuna kila dalili ya kunyang'anywa dhamana 2015!
   
 4. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Ushauri wa bure kwa wana ccm, watanganyika hatudanganyiki tena!
   
 5. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Kalamu ya Ngurumo daima huwa naiheshimu. Hongera sana Mpiganaji makini.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,602
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,796
  Likes Received: 36,818
  Trophy Points: 280
  wamegundua hali ni tete
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,419
  Trophy Points: 280
  Mimi bado napigania CCM imsimamishe EL na kama afya yake itaendelea kuwa mgogoro kama ilivyo sasa, hataweza kuhimili mikiki mikiki ya 2015, hivyo basi wamsimamishe Membe, ili upatikane ushindi laini safi na very clear bila migogoro, kuumizana wala kusuguana, ikulu ni njia nyeupe, safi na iliyoonyooka bila kona kona zozote, cha muhimu ni kujipanga kutoka sasa!.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,602
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  Bado tu unamfagilia Lowassa ili mafuta uzuri yakupate nawe. Huyu Lowassa ni fisadi tu. Sijui kwa kipi alichokifanya Lowassa kwa Tanzania au Watanzania uone anastahili kusimamishwa kama mgombea wa magamba 2015.


   
 10. N

  Nonda JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  CCM wanaweza kubaki madarakani kama wanapenda, tena kwa uhalali. Muda wanao wa kujipanga lakini Mkuu Pasco, sikio la kufa.......
  Litakalowaepusha CCM kuenguliwa madarakani ni :
  1.Kuifufua serikali ya Tanganyika, litokee G55 kutoka CCM na lifanikiwe katika kuileta Tanganyika na serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano. Mpaka sasa hakuna Chama ila DP(Rev.Mtikila) ambaye amedaka huu upenyo wa hali tete ya muungano ambayo imepelekea watu kutaka Tanganyika na serikali yake irudi.

  2. Kupitisha sheria ya ufisadi, rushwa na kuitekeleza kama vile wanavyofanya China.

  3. Kuacha usanii na siasa za ahadi hewa badala yake watatue shida za wananchi na kuwawezesha wazawa.

  4. Kupiga U-turn katika kusimamia rasilimali za taifa( kuingia mikataba yenye maslahi kwa nchi na kufuta ile inayotoa %3 kwa nchi yetu na wawekezaji kujichukulia watakavyo.

  5. CCM wamsimamishe Salim A. Salim. au mgombea wa kike mwenye uwezo wa uongozi.

  6.Wasimsimamishe mtu mwenye Afya mgogoro kama huyo ulimtaja( mgogoro wa Afya unaongezeka na umri, usitegemee mtu wako atatengemaa kiafya kuhimili marathon ya uchaguzi mkuu), lakini zaidi wamsimamishe mtu ambaye anaonekana katika macho ya wananchi kuwa ni mtu safi, ambaye hajaandamwa na kashfa za ufisadi na utumiaji mbaya wa madaraka.

  Je kuna katika CCM mwenye nia na uwezo wa kutenda hayo?

  Nitafurahi kuona CCM na wao wanaonja joto ya kuwa chama cha upinzani.
   
 11. Collins

  Collins Senior Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  never hawataweza kutekeleza hizo points,hawana huo ubavu
   
 12. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  7. Wabadirishe jina la chama CCM. Hili linatuchefua watafute jingine na kubadirisha safu nzima ya uongozi wa juu, wa kati na wa chini na kuweka ule wa CHADEMA.
   
 13. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Kwa jicho la mbali sana swali kubwa ni JE CHADEMA WAMEJIANDAA KIMKAKATI NA KIUWEZO KUITAWALA NCHI... Kwa wengi wetu msisimko na matarajio ni makubwa kiasi hatuna nafasi ya kujiuliza swali hili, lakini wako wengi walioko kwenye limbi (kuichoka CCM vs kutoiamini CDM) na kuna haja ya jibu la swali hili kupatikana...
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,602
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  ...Ni kweli hilo usemalo lakini kwa jinsi walivyolewa na madaraka watakuwa tayari kufanya lolote lile ili kubaki madarakani. Si umeshasikia kauli za "CHADEMA ni Wahuni hatuwezi kuwakabidhi nchi."

   
 15. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2016
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Well said Mkuu.
   
 16. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2016
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Unajua siku hizi kuna slight difference ambayo ni almost negligible, baina ya chama tawala na chama shindani. Mbinu ni zile zile zinazofanywa na watu wale wale ambao zamani walikuwa watawala wakageuka kuwa washindani. Kwetu sisi tusio wafia vyama tumeshawapuuza nyote.
   
 17. THOMASS SANKARA

  THOMASS SANKARA JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2016
  Joined: Nov 13, 2014
  Messages: 456
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 180
  Mkuu BAK pitia huku uone unafiki wako
   
 18. m

  mwasu JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2016
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 8,259
  Likes Received: 6,138
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi alieteuliwa mpaka sasa hajafika kituo chake cha kazi huko moshi, alietolea kazini bado anasubiri kukabidhi mtu kazi lakini jamaa huko aliko anajua mwenyewe kimyaaaaa, haijawahi kutokea kabla ya awamu hii.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2016
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,602
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  Hakuna unafiki hapo hebu onyesha nilipoandika tofauti na nilivyoandika hapa. Kama utaweka huo ushahidi wa kuonyesha bandiko la kugeuka hiki nilichoandika hapa naam huo utakuwa ni unafiki, vinginevyo umekurupuka bila kujua nini maana ya UNAFIKI.

   
 20. Japkas

  Japkas JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2016
  Joined: Mar 12, 2014
  Messages: 762
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 80
  Hizi hasira za ufisadi wa Lowassa zinaendelea bado?
   
Loading...