Wamechezea hela zetu vyakutosha na sasa wameanza kuchezea miili yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamechezea hela zetu vyakutosha na sasa wameanza kuchezea miili yetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlangaja, Feb 2, 2011.

 1. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tukio lililotokea katika Hospitali ya mwananyamala ni la kusikitisha sana, hasa katika wakati huu ambapo fedha zinaibiwa kiholela, bei za umeme na mafuta zimepandishwa na kuidhinishwa kwa malipo kwa makampuni hewa. Mimi ningependa kuwapa changamoto, kwamba fedha na mali zetu wanaweza kuchezea lakini si miili yetu. Naomba wawe makini, kuna vitu visivyovumilika katika ulimwengu huu. Kuchezea miili ya watu waliokufa ni jambo la kuzimu, binafsi sipendi na sitaki kusikia katika nchi yangu.
  Serikali iwe makini! Naomba iwe makini. Yote fanyeni lakini dhambi inayotendwa katika mwili wa mwanadamu haisameheki.
   
 2. S

  Sukya New Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :deadhorse: Huu ni ushirikina mkubwa ambao hauvumiliki, kuua vichanga ambao ni taifa la kesho kweli haivumiliki. Vyombo vya sheria vichukue mkondo wake bila kubania bania mambo. Mara nyingi utasikia uchunguzi unaendelea, lakini mwisho wa uchunguzi hatuusikii, hapo inakaa vipi, au ndo ule moto wa mabua, yakipita basi inabaki historia iliyosahaulika.
   
Loading...