Wambura namfananisha na Giwa na maalim seif anajipotezea muda tu

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,471
4,424
Leo mahakama imetoa hukumu ya rufaa aliyokataa Michael Richard Wambura juu ya kufungiwa kwake na kamati ya maadili ya Tff.Mahakama imetoa pingamizi hilo na kumrudisha Wambura kwenye nafasi yake ya zamani ya umakamu wa rais wa Tff.

Turudi nyuma kidogo mwezi june mwaka huu Chama cha soka cha nchini Nigeria Nff kulikuwa na mtarufuku kwenye uongozi ndipo Mr Giwa akaenda mahakama kuu na mahakama kuu ikamtawaza kama rais wa NFF na kumfukuzia mbali Pinnick kisha waziri wa michezo kutoa amri pinnick aondoke.Papo hapo Fifa ikaingilia kati na kutoa onyo kali na kisha ikaomba ipewe maelezo kwanini masuala ya soka yanaenda kuhukumiwa nje na third party kilichotokea huyo waziri akaomba radhi ili wasifungiwe na FIFA.sheria ya Fifa inasema kila mwanachama wa fifa ikitokea any disputes ni haramu na dhambi kubwa kwenda kuyasuluhisha kwenye mahakama za kiraia.

Huyu bwana Giwa mpaka leo hii tarehe 30 Nov yupo kwake tu licha ya mahakama kumpa uongozi NFF na bwana Pinnick anazidi kutesa tu na NFF yake.

Kila federation zina courts zake bwana wambura baada ya kufungiwa na mahakama ya Tff ilibidi akate rufaa hapo au aende CAS.

Pia August mwaka huu rais wa chama cha soka nchini Gambia bwana Lamin Bajo na wenzake walipandishwa kizimbani na mpinzani wao mahakamani .Fifa wakatoa onyo kali na kuwakumbusha Gambia na mahakama hio vifungu vya sheria vya Fifa..naomba mjisomee hapo chini

Namkumbusha bwana Wambura juzi rais wa chama cha soka nchini Spain bwana Villar alifukuzwa na mahakama ya michezo katulia zake sababu anajua sheria ila hawa wa KiAfrika kama huyu wa Gambia na Nigeria walivyokimbilia mahakama za kiraia Fifa wakaingilia na kutoa onyo na mpaka leo hawajagusa kuingia kwenye federation za michezo.

Ina maana Wambura hajui Cas ilipo na hajui kuwa any dispute za uongozi ni mahakama za federation au CAS ndio wenye mamlaka ya kutatua tu.

Wambura namfananisha na bwana Giwa na Maalim seif.Atajikalia kwake soon tu na hio hukumu ya mahakama kama itamrudisha.
Screenshot_2018-11-30-20-43-03-1.jpg
Screenshot_2018-11-30-20-43-12-1.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_2018-11-30-20-43-12-1.jpg
    Screenshot_2018-11-30-20-43-12-1.jpg
    63.2 KB · Views: 29
Leo mahakama imetoa hukumu ya rufaa aliyokataa Michael Richard Wambura juu ya kufungiwa kwake na kamati ya maadili ya Tff.Mahakama imetoa pingamizi hilo na kumrudisha Wambura kwenye nafasi yake ya zamani ya umakamu wa rais wa Tff.

Turudi nyuma kidogo mwezi june mwaka huu Chama cha soka cha nchini Nigeria Nff kulikuwa na mtarufuku kwenye uongozi ndipo Mr Giwa akaenda mahakama kuu na mahakama kuu ikamtawaza kama rais wa NFF na kumfukuzia mbali Pinnick kisha waziri wa michezo kutoa amri pinnick aondoke.Papo hapo Fifa ikaingilia kati na kutoa onyo kali na kisha ikaomba ipewe maelezo kwanini masuala ya soka yanaenda kuhukumiwa nje na third party kilichotokea huyo waziri akaomba radhi ili wasifungiwe na FIFA.sheria ya Fifa inasema kila mwanachama wa fifa ikitokea any disputes ni haramu na dhambi kubwa kwenda kuyasuluhisha kwenye mahakama za kiraia.

Huyu bwana Giwa mpaka leo hii tarehe 30 Nov yupo kwake tu licha ya mahakama kumpa uongozi NFF na bwana Pinnick anazidi kutesa tu na NFF yake.

Kila federation zina courts zake bwana wambura baada ya kufungiwa na mahakama ya Tff ilibidi akate rufaa hapo au aende CAS.

Pia August mwaka huu rais wa chama cha soka nchini Gambia bwana Lamin Bajo na wenzake walipandishwa kizimbani na mpinzani wao mahakamani .Fifa wakatoa onyo kali na kuwakumbusha Gambia na mahakama hio vifungu vya sheria vya Fifa..naomba mjisomee hapo chini

Namkumbusha bwana Wambura juzi rais wa chama cha soka nchini Spain bwana Villar alifukuzwa na mahakama ya michezo katulia zake sababu anajua sheria ila hawa wa KiAfrika kama huyu wa Gambia na Nigeria walivyokimbilia mahakama za kiraia Fifa wakaingilia na kutoa onyo na mpaka leo hawajagusa kuingia kwenye federation za michezo.

Ina maana Wambura hajui Cas ilipo na hajui kuwa any dispute za uongozi ni mahakama za federation au CAS ndio wenye mamlaka ya kutatua tu.

Wambura namfananisha na bwana Giwa na Maalim seif.Atajikalia kwake soon tu na hio hukumu ya mahakama kama itamrudisha.View attachment 951774View attachment 951776
Mmmmh sikubaliana na wewe inamaaaana wewe unaonesha na wewe ni wale wale wanaopambana na wambura maana umejieleza kweli kweli ,kimsingi nikuwa huyu jamaa kuna watu na wewe ni moja wao ambao hutumia huo ujanja ujanja wa kimtandao kutaka kuumiza wenzao kisa hutakiwi kwenda huko mahakamani
 
Hapana ninachoshangaa kwanini Wambura kama intellectual asiende kabisa CAS au hata CAF kisha aende mahakamani wakati wambura amekaa muda mrefu kwenye sekta hii ya mpira na asiyajue haya yote hata mifano ya juzi tu ndani ya mwaka huu asiyaone...unaweza kuta hata CAS hajaenda hapo

Mie namkumbusha tu, hata sina chuki wala kinyongo nae
 
Unahisi ni mara ya kwanza jamaa kwenda mahakamani na kesi zote katoboa tulia awanyooshe ninyi tiefu tiefu kichefu chefu
 
Mbona hawakupindua uamuzi wa FBI ilipotinga FIFA na kuwatawanya akina Jerome na Joseph
Mkuu FBI haikutoa maamuzi yeyote bali ma agent wa fbi walitoa siri na ubadhilifu wa Blatter wa $10 Million walioufanya..Blatter aliweza kuendelea na urais asijiuzulu ila kwa kashfa ile alijiuzulu lkn hakuna popote fifa iliingiliwa kimaamuzi na Fbi au taasisi yeyote.
 
Kila mbabe ana mbabe wake

Kwa taarifa zilizovuja ni kwamba wao viongozi wa fifa waliwachoka wakubwa zao wakina sepp bletter walikuwa wanapiga hela sana walichofanya hili genge la raisi wa sasa wa fifa walisuka zengwe kwenda fbi kwa madai ya rushwa na kweli rushwa ilikuwepo ukizingatia usa walikuwa na hasira na bwana bletter haikuwa kazi ngumu kuisambaratisha fifa nani wakupingana na marekani?
 
Mkuu FBI haikutoa maamuzi yeyote bali ma agent wa fbi walitoa siri na ubadhilifu wa Blatter wa $10 Million walioufanya..Blatter aliweza kuendelea na urais asijiuzulu ila kwa kashfa ile alijiuzulu lkn hakuna popote fifa iliingiliwa kimaamuzi na Fbi au taasisi yeyote.
Jerome alishitakiwa na account zake zilikuwa frozen. Wambura alikuwa anatuhumiwa kwa jinai, TFF ilitakiwa wamsimamishe na kuiomba JAMHURI imfungulie mashitaka.
 
Unahisi ni mara ya kwanza jamaa kwenda mahakamani na kesi zote katoboa tulia awanyooshe ninyi tiefu tiefu kichefu chefu
Hao FIFA na hao FA zao, wamejijengea ufalme fulani, ambao hawataki kuingiliwa. Utaona maonevu ya wazi kabisa, mwathirika hana kwa kukimbilia.
We ufamfungiaje mtu maisha yake yote, asijihusishe na mchezo aupendao?
 
Wambura namsikia tokea kitambo Fat wenzie akina Tenga,ndolanga na rage washastaafu
 
wambura namfananisha na marehemu mtikila kwenye siasa ni wabishi dunia nzima hakuna
 
Mmmmh sikubaliana na wewe inamaaaana wewe unaonesha na wewe ni wale wale wanaopambana na wambura maana umejieleza kweli kweli ,kimsingi nikuwa huyu jamaa kuna watu na wewe ni moja wao ambao hutumia huo ujanja ujanja wa kimtandao kutaka kuumiza wenzao kisa hutakiwi kwenda huko mahakamani
vp unasemaje sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom