Wambura awekewa pingamizi

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,192
25,493
Mgombea wa nafasi ya Rais ya Klabu ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam,Michael Wambura amewekewa pingamizi dhidi ya ugombea wake.Pingamizi hilo limewekwa na aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Simba,Seydou Rubeya.Rubeya amedai kuwa pingamizi lake linajikita katika hoja ya kwamba Wambura aliwahi kupeleka masuala ya soka mahakamani na pia aliwahi kufisidi TFF.

Mwisho wa mapingamizi ulikuwa leo saa kumi jioni.

Chanzo: Radio One Stereo, Sports
 
simba wasirudie makosa waliyofanya kwa rage Wambura alikuwa kiongozi tff ni jambo gani la maana alilofanya tff ambalo atakuja kulifanyia simba yule akichaguliwa sana sana atarudisha migogoro na hiyo imejitokeza hata kwenye maneno yake
 
ni vyema kujiuliza kwanini kuna watu ni hao hao tu ndio wamekuwa wakitaka uongozi wa mpira siku zote, je hakuna wengine wenye uwezo wa kuongoza? wanachama wawe na fikra mpya ili timu yao ipate mafanikio ya kimataifa.
 
simba still in limbo; akiingia wambura friends wataweka zengwe, akiingia aveva taliban.....................
 
ni vyema kujiuliza kwanini kuna watu ni hao hao tu ndio wamekuwa wakitaka uongozi wa mpira siku zote, je hakuna wengine wenye uwezo wa kuongoza? wanachama wawe na fikra mpya ili timu yao ipate mafanikio ya kimataifa.

mtu anayetaka uongozi kwa kutumia pesa ni wa kuogopa sana
 
Wambura anatosha, hizo tuhuma zote alishakuwa cleared, tafuteni hoja zingine!
wachumia tumbo wote mwisho wenu umefika
 
Wambura anatosha, hizo tuhuma zote alishakuwa cleared, tafuteni hoja zingine!
wachumia tumbo wote mwisho wenu umefika

Haka ka sarakasi kaendelee hivi hivi hadi wachague viongozi bomu ili Jangwani tuendelee kukaa kwa amani bila ya kuwa na hofu na Mnyama, tuelekeze nguvu kumdhibiti Azam peke yake.
 
Back
Top Bottom