Wambura awajibu TFF, asema anasubiri barua ya maamuzi ya Kamati ya Maadili

Mar 5, 2018
28
25
MAKAMU Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Michael Wambura ameeleza suala Kamati ya Maadili ya shirikisho ni la kimkakati zaidi na si la kisheria.

WAMBURA.jpg

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Wambura amesema suala hilo lilianza miaka 14 iliyopita akiwa raia wa kawaida tuu.Wambura anatuhumiwa kufoji barua na kupokea malipo yasiyo halali kutoka Kampuni ya JICK System Ltd,pia kushusha hadhi ya TFF.

Akizungumzia zaidi suala hilo Wambura ameeleza tatizo lililopo ni uenyekiti wa TFF, fedha na ajira za TFF hasa nafasi ya Katibu Mkuu.Pia Wambura amesema kuwa kama Makamu Mwenyekiti wa TFF ataendelea kufanya kazi kama kawaida na lawama hizo zishindwe kabisa.

Ameongeza, kuwa kuna tatizo kubwa sana ndani ya Shirikisho hilo na wananchi watalijua mapema na ameitaka kamati tendaji kufikiri tena kabla ya kufanya maamuzi.Hata hivyo amesema anasubiri barua rasmi ya kamati hiyo na ndipo atakuwa na cha kuzungumza,hivyo anasubiri maana kwa sasa amesikia tu taarifa kuhusu kusimamishwa kujihusisha na soka.

Kwa upande wa Wakili wa Wambura Emmanuel Muga amesema, kikao hakikufuata sheria hali iliyompelekea kushindwa kufanya kazi yake, amesema barua ya mwito ilicheleweshwa na ilipelekwa nyumbani kwake ili hali Wambura yupo TFF.

Pia ameeleza kanuni ya 48 ya maadili ya TFF inayoeleza kuna siku 3 za kuitikia mwito haikuzingatiwa na pia kamati haikuzingatia kanuni ya 58 inayoeleza kuhusu kesi na kupanga siku ya kuleta vielelezo na mashahidi haikuzingatiwa kwa mteja wake.

Pia Muga ameeleza kuwa kikao hicho hakikutoa majibu ya moja kwa moja na walieleza watatoa uamuzi siku nyingine.
 
Karia ni Simba damu.
Wambura ni Simba damu.

Walifanya kila njama kuhakikisha wana Simba wanakamata nafasi zote za juu. Walisaidiwa na mkubwa mmoja serikalini ambaye ziara zake nyingi ni kwao tu.

Sasa mafuta yameanza kujitenga na maji.
 
Wambura si wamwache aisee...
Viongozi wa Tff uroho wa madaraka unawaponza..

Yule kapata ( na mimi nataka km yy)
 
Inawezekana kweli kavuta mkwanja lakini kwanini asisikilizwe? Kwa ushahidi wa forgery na kuchukua pesa si kesi ya nusu saa hii? Wangempa nafasi apangue ushahidi wao then wamhukumu fairly.
 
Wambura si wamwache aisee...
Viongozi wa Tff uroho wa madaraka unawaponza..

Yule kapata ( na mimi nataka km yy)
Uongozi unapaswa kuendana na uaminifu. Haitoshi kiongozi kuwa mwaminifu/mwadilifu. Ni lazima aonekane kuwa mwaminifu. Kwa bahati mbaya Wambura haonekani kuwa mwaminifu/mwadilifu. Kila alipopata fursa ya kuwa kiongozi, aliandamwa na tuhuma zinazomnyima sura ya uadilifu. Alipokuwa Katibu Mkuu FAT alituhumiwa kutowasilisha majina ya Wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la CAF (Mlandege ya Zanzibar) lakini ya Mwakilishi wa Klabu Bingwa (Simba ya Dar-es-salaam) aliyapeleka. Mlandege haikushiriki. Uenyekiti wa Chama cha Mpira Mkoani Mara, alishauriwa kuachana nao mara tu baada ya kushinda U-makamu Mwenyekiti wa TFF kwa kuepuka mgongano wa kimaslahi. Akakataa. Baadaye akatuhumiwa kushiriki katika jaribio la kuzibeba timu za Mkoa wake kwenye Ligi ya Daraja la Kwanza. Simba wanajua zaidi alichotuhumiwa nacho alipowahi kuwa Katibu Mkuu wao, na kwa nini hawapendi apate nafasi ya kuiongoza tena. TFF ya Tenga inaonekana haikupenda apate nafasi ya kuongoza kandanda nchini, labda baada ya kuona kumbukumbu za aliyoyafanya alipowahi kuwa kiongozi wa ngazi hiyo. TFF ya Karia nayo imemhukumu kwa iliyomtuhumu.
Nadhani wakati umefika wa Wambura kusafisha jina lake. Kwanza kwa kukata rufaa kama alivyoahidi. Na baada ya hapo - iwe ameshinda au la - kuachia ngazi kabisa katika uongozi wa kandanda wa ngazi za juu - Taifa, Mkoa, Wilaya. Kuna njia nyingi za kuchangia maendeleo ya soka nchini bila ya kuwa kiongozi.

Akina Manyoto Ndimbo, Mansour Magram, Ahmed Jongo, Mbaraka Mwinshehe, Juma Kilaza, Charles Hillary, Mwamoyo Hamza, Edo Kumwembe, Mwalim Kashasha na wengi wengine walichangia na wanachangia sana mchezo huo kwa namna mbalimbali, bila ya kuwa ni viongozi wa FAT au TFF. Raia mwema anaweza sana kuchangia maendeleo ya nchi yake bila ya kuwa Rais wala Mbunge. Seuze mpenzi wa kweli kuchangia maendeleo ya kandanda ya nchi yake bila ya kuwa kiongozi.
 
Kula like mkuu
 
Back
Top Bottom