Wamasai Waliokamatwa Ngorongoro wafunguliwa Kesi ya Mauaji

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,620
218,041
Hii ndio Taarifa mpya kutokana na Sakata la Ngorongoro , ambapo Serikali leo imeamua kuwafungulia Kesi ya mauaji wahanga hao waliogoma kuhama kwa hiyari.

Taarifa zaidi zinaonyesha kwamba wamasai hao waliswekwa rumande siku moja kabla ya Uvamizi wa Polisi , na kwamba wakati Askari akipigwa Mshale wao walikuwa tayari selo , inakuwaje wanahusishwa na mauaji hayo?

Tutaweka hapa orodha kamili ya walioshitakiwa kwa mauaji na kama kutakuwa na mashitaka mengine tutayaweka wazi hapa hapa.

Usiondoke.
 
Duh, hata kabla ya update, uzushi wa aina hii sio mzuri hata kidogo, huwezi kudai waliogoma kuhama ndio wamebambikiwa kesi ya mauaji.

Ukweli ni kuwa kuna askari wetu mmoja amekufa baada ya kuchomwa mshale wenye sumu kali na mmoja wa morani hao.

Kwa vile lilikuwa kundi, wanakikukindi hao, wanamjua aliyemchoma mshale uliomuua askari wetu ila wameamua wasimtaje, hivyo wanasombwa wote na kushitakiwa as accessories after the fact.

Hivyo sii kweli kuwa wamebambikiwa kesi ya mauaji kwa kukataa kuhama!

Hata hivyo baada ya kesi kutajwa, polisi wetu hutumia mbinu za kipolisi za mahojiano ili wawataje wahusika halisi na wale wasio husika hugeuka mashahidi wa Jamhuri.

Kutokana na mafunzo ya ukakamavu ya morani wa the Maasai people, they would rather die mikononi mwa polisi kuliko kumtaja mwenzao.

Ila pia ma Laigwanan wa the Maasai people wakiamua, DPP anafuta kesi na morani wote wanaachiwa bila masharti yoyote.

Kwa ndio wajua the Maasai people walivyo na umoja, soma hiki kisa cha huko Arusha, hao morani wa kimasai waliwahi kufanya nini na wakafanywa nini, ndio maana nawaambia Ma Laigwanan wakiamua hakuna kesi hapo!.

P
 
Sasa askari achomwee mkuki halafu bado waendelee kuishi kwa Aman kingekua kipindi cha ngosha huu upuuzi usingekuwepo kabisa Kimara watu wamevunjiwa magorofa bila hata kupewa hela hata ya maji na wakaufyata wewe mmasai ni nani na zile tembe zako eti uuwe Askari uendelee kuchekewa mara zote nipo against polisi ila sio kwa hili
 
Sasa askari achomwee mkuki halafu bado waendelee kuishi kwa Aman kingekua kipindi cha ngosha huu upuuzi usingekuwepo kabisa Kimara watu wamevunjiwa magorofa bila hata kupewa hela hata ya maji na wakaufyata wewe mmasai ni nani na zile tembe zako eti uuwe Askari uendelee kuchekewa mara zote nipo against polisi ila sio kwa hili
Akili zako na Hugo shetwaani ngosha hazijapishana
 
Hii ndio Taarifa mpya kutokana na Sakata la Ngorongoro , ambapo Serikali leo imeamua kuwafungulia Kesi ya mauaji wahanga hao waliogoma kuhama kwa hiyari...
Mkuu usitufanye wajinga.

Thibitisha uliloandika.

Walikamatwa watu takribn 10 baada ya askari kuuwawa, kulingana na kmanda Sabas.

Hao waliokamatwa jana yake watahusikaje tena na mauaji kama walikuwa selo?

Mwaga data zako
 
Hii ndio Taarifa mpya kutokana na Sakata la Ngorongoro , ambapo Serikali leo imeamua kuwafungulia Kesi ya mauaji wahanga hao waliogoma kuhama kwa hiyari...
wamegoma kuhama kwa hiari, wameua polisi. ulitaka wasifunguliwe kesi ya mauaji? hapo hadi upelelezi ukamilike washakula mvua ya mwaka. watatia adabu. hivi wakishika ile mikuki yao na panga zao huwa wanajiona wanaweza kutetemesha serikali? pyuuuuu
 
Kwenye sakata la wamasai wewe unafahamika upande uliopo , hakuna anayekushangaa , zipo tetesi kwamba umelipwa ( Tukithibitisha tutaanika hadharani bila kuogopa )
Mkuu Erythrocyte , mimi siku zote I'm always side with the truth. Naomba nikuhakikishie mimi ni an independent journalist, silipwi na yeyote kwasababu sina bei, yaani ni priceless. Hivyo don't waste your precious time kusubiria uthibitisho wa hizo tetesi Pasco Mayalla halipwi na yeyote, na anafanya uandishi wa habari kwa mapenzi tuu and sio kwaajili ya malipo!.
P
 
Back
Top Bottom