Wamasai wakataa kuondoka katika ardhi ya Serengeti Tanzania

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mgogoro wa ardhi wilayani Loliondo, Kaskazini mwa Tanzania umeendelea kukua baada ya mamlaka za uhifadhi wilayani humo kuendelea kuchoma nyumba za watu wa jamii ya Kimaasai. Viongozi wa kijiji wa eneo hilo wameiambia BBC kwamba zaidi ya familia 500 zimeachwa bila makazi.

Wakati serikali ikisisitiza kwamba zoezi la kuwaondoa watu karibu na hifadhi ya Serengeti lazima liendelee, jamii ya Wamaasaia wa eneo hilo wameiambia BBC kwamba wako tayari kutoa uhai wao wakiilinda ardhi yao.

Mwandishi Sammy Awami alitembelea eneo hilo na kutuandalia taarifa

Chanzo: BBC
 
Hakuna tatizo kubwa linalotukabili wahifadhi na jamii nzima ya uhifadhi kama hili la ongezeko la makazi katika maeneo ya uhifadhi, hawa ndugu zetu inabidi waelewe kitu, mambo yamebadilika siku hizi kuendelea kuwaacha hawa watu kwa kigezo cha uwenyeji ni kuamua kuitokomeza kabisa hii rasilimali na hazina ya taifa na dunia kwa ujumla (serengeti) , mind you enzi hizo namba ya hawa wamasai ilivyokuwa ndani ya hifadhi na sasa ni tofauti kabisa, watu wanazidi kuzaliana jamii inazidi kukua na mahitaji yanazidi kuongezeka , leo hii si ajabu kusikia mmasai nae ameingia kwenye shughuli za kilimo kwaajili ya kujipatia kipato na chakula kitu ambacho hakikuepo mwanzoni, sasa ukishaanzisha shughuli za kilimo hifadhini nambie kuna nini tena hapo?

Mi nadhani ifike kipindi lazima tukubali kuwa flexible na kwenda na mabadiliko.

Conservation.
 
Hili la kuongezeka halikuonekana toka awali,,, are we that myopic!!
 
mbona ngoro ngoro wanaishi bila shida?wakae watatue tatizo na sio kuchoma Nyumba za wamasai!
 
Magufuli huyu asiye na huruma bora mjiondokee maana watawaletea polisi kutoka Dar ambao hamzungumzi lugha moja na hamna undugu au watawaletea wakurya mliokua mkiwaibia mgombe
 
Back
Top Bottom