Wamasai wadai hawaondoki Ngorongoro kwa sababu wanalindwa na UTATU wa kikatiba yaani Wenyeji - Hifadhi - Utalii

Issue ya Ngorongoro ni Suala nyeti sana kitaifa na siyo masilahi ya wamasai. Kwa maana kiualisia hawakuzaliwa maeneo hayo by nature kwa maana hiyo walikwa hapo kulingani na historia inavyo sema.

Sasa kama kuna impacts yake ni kubwa kiikologia , basi tuache utasi ifanye kazi pasipo hisia.

Nashauri wamasai waangalizie namna bora ya wao kwenda kuisi maeneo mengine au wawatenge maeneo yao hapo pasipo ku-interacts na wanyama moja kwa moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kwamba wamasai hawataki kuondoka,ila hawana uhakika huko wanakotaka kupelekwa kutakuwa na malisho, na maji ya kutosha na eneo la kutosha, Kama ngorongoro! Wasije wakawahamishia Oysterbay .
 
Tanzania masikini wa akili ni wengi sana
We jifurahishe kwa statement za kijinga, kawashauri wana ukoo wako mhame mbugani tafuteni hata kazi ya ulinzi bado mnafaa ikishindikana semeni tuwauze maana si mmesema nyie ni kivutio Cha utalii???
 
Wamasai waishio kwenye vijiji vya hifadhini Ngorongoro wamesema kamwe hawatahama kwani Ngorongoro ni mafiga matatu ya Wenyeji, Hifadhi na Watalii na ukiondoa figa moja Ngorongoro inakufa.
Kwahiyo yule mwandishi mwenye kofia ya adidasi alikuwa kimbelembele kuwapigania wapewe huduma muhimu, wao wanatamani waendelee kuliwa na simba
 
Inapelekwa jeshi kule ukitaka kusikia wamasai wameuwawa Kama kuku wajifanye wanaleta Vita ya kinjekitile watafurahi maaaanina.
Kila Msimu/Awamu ya Rais haikosi laana. wabunge wanapanga kwenda kuua wamasai ili wapamgishe wazungu!

Karma hii haitatuacha salama!
 
Hifadhi ya Ngorongoro ina nia kuu tatu(1) Hifadhi (2) Utalii (3) Makazi ya binadamu yasiyodumu. Pamoja na kuwa na nia nzuri lakini sisi binadamu tumekiuka taratibu hizi. Kwanza kumekuwa na ongezeko la kutisha kwa watu na kumekuwa na ujenzi wa makazi ya kudumu.

Nashauri sheria inayohusu Hifadhi ya Ngorogoro ipitiwe upya na kama itaonekana kuwa hapahitajiki binadamu kukaa pale basi wakazi wote waliopo kwenye Hifadhi wahame. Tanzania bado tuna ardhi ya kutosha wanaweza kutafutiwa mahala pa kuishi na siyo Ngorongoro peke yake.
 
Acha utoto wewe unahisi kila mtu hapa ana umri wako? Kwamba wao ndio watashinda risasi kwa Ile mikuki kisa wanaishi na Simba kwanza hawaishi na simba ni kwamba Simba ndio anaishi na Masai baada ya Masai kujisoheza kwenye himaya ya Simba.

Simba hapendi nyama ya binadamu sababu Ina chumvi na ng'ombe pia hapendi labda Simba mzee ambaye ametengwa na wenzie anakuwa hana nguvu ya kuwinda ndio husogea kwenye makazi ya binadamu avamie mbwa, mbuzi au binadamu wenyewe Ila Simba na chui hana muda na binadamu.

Pia Simba akiwa na watoto na akiwa na njaa anaweza kuvamia group ya ng'ombe na hii inatokea sana hapo ngorongoro sio kwamba haya matukio hayapo sema ndio maana nasema sio Masai ndio anaishi na Simba Ila ni Simba ndio huamua kuishi na Masai kwa maana anakaa mbali nao sababu anaona pale chakula kipo Cha kutosha Ila akikosa menu atakula ng'ombe hata watano in case ukatokea group ya Simba dume watupu.
Hata Simba wakiwala hupo porini hawawezi kusema maana wataulizwa kwanini waishi huko? Kikubwa sasa wameona watu wengi wanapenda wabadilike waishia maisha ya mtu mwenye utashi wa kujenga kizazi cha baadaye na siyo kuishi kama wanyama bila huduma za msingi na kujenga kizazi cha baadaye kwa kuishi tu porini na kuchunga wanyama bila mipango yao ya maisha itakayoletea jamii maendeleo.
 
sio kwamba wamasai hawataki kuondoka,ila hawana uhakika huko wanakotaka kupelekwa kutakuwa na malisho ,na maji ya kutosha na eneo la kutosha ,Kama ngorongoro!?, wasije wakawahamishia osterbay .
Ndo maana wanatakiwa kufuga kisasa na maisha ya kutangatanga wawaachie wanyama wa porini, wao ni watu na ndugu zetu maisha ya kale wote babu zetu waliishi ila Sasa tunatakiwa tuishi tofauti na kizazi cha kale kwa kuishi kisasa kwa Kila jambo Ili ajira zipatikane na utu wa Kila mtu uwe salama Sasa huko kushinda kutafuta malisho sehemu isiyo shamba lako huo ni uchokozi maana hiyo ruhusa wamepewa wanyama peke yake ila binadamu anatakiwa atengeneze miliki yake ya kufanya mambo katika mpangilio mzuri, imagine hawaoni wafugaji wa kuku jinsi wanafuga kisasa katika maeneo yao na mifugo yao imeleta viwanda vya kuzalisha chakula cha kuku Sasa wao wamenyima hata viwanda vya kuzalisha chakula cha ngo'mbe na wanyama wa kufuga kwa kuzunguka na mifugo, wamenyima ajira zinazoeleweka kwa vijana wao maana kama Kila mtu angekuwa na farm ya wanyama kama wafuga kuku ni ajira ngapi zingepatikana kuanzia daktari wa mifugo, viwanda vya chakula cha mifugo, wahudumu wa kusimamia farm, boss mwenye mfugo kuwa wa kisasa, kuishi kwenye maeneo yao nakuacha kugombana na wakulima na wanyama wa porini.
 
Inapelekwa jeshi kule ukitaka kusikia wamasai wameuwawa Kama kuku wajifanye wanaleta Vita ya kinjekitile watafurahi maaaanina.
Wanalindwa na sheria za umoja wa mataifa wale.Jeshi usiku watakula mishale hadi wachakae pili hatujafikia huko.
 
Wanalindwa na sheria za umoja wa mataifa wale.Jeshi usiku watakula mishale hadi wachakae pili hatujafikia huko.
Masai hajawahi kupigana vita labda ndio iitwe mishale war against modern army tactics tuone mabushmen watakavyochakaa.

Usicheze na mtu ana googles zenye night vision na ana rada anakutupia risasi mita Mia tano kutoka kwenye sniper rifle hiyo mishale utaishia kujichoma kalio
 
Wamasai waishio kwenye vijiji vya hifadhini Ngorongoro wamesema kamwe hawatahama kwani Ngorongoro ni mafiga matatu ya Wenyeji, Hifadhi na Watalii na ukiondoa figa moja Ngorongoro inakufa.

Wamedai wao wanaishi vijiji vya hifadhini kwa mujibu wa sheria.

===
Wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza wabunge kuelimishwa kuhusu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Jamii ya wafugaji wanaoishi kwenye bonde hilo wamesema wataendelea kuishi kwa kufuata sheria na kanuni za uanzishwaji wa mamlaka hiyo na si vinginevyo.

Source: Star tv!

View attachment 2115445
Mungu wabariki Wamasai .
 
Back
Top Bottom