Wamarekani weusi wana ushindani mkubwa wa kiharakati ukilinganisha na Waafrika

wazanaki

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
1,092
804
Wakuu, leo tugusie hawa watu wanaitwa Wamarekani weusi, hawa jamaa bana wanahistoria ndefu sana na yenye mateso, ila Mungu si athumani pamoja na kupitia mateso yote still wapo wana exist.

Tunajua kwamba wamarekani weusi ni ndugu zetu waliochukiuliwa utumwani miaka 400 iliyopita, waliuzwa kama bidhaa kwa matajiri waliuokua wameweka kambi huko, walifanyishwa kazi usiku na mchana. Kwasababu hawa jamaa waliwekwa kwenye pressure ya Maisha kwa mda mrefu huku wakijaribu kuwa huru, walifanikiwa kujifunza mengi sana, hali hiyo iliwafanya wakomae licha ya kwamba kila walipokua wanajaribu kua free walikua wana kanyagiwa.

Pia wale jamaa wameishi na watesi wao kwa mda mrefu, so wanawajua nje ndani, lakini mnatakiwa mkumbuke kitu kimoja, kinachoendelea kwa wamarekani weusi ndo kilichokua kinaendelea Afrika, ila kwa sababu Afrika majority ni weusi ni ngumu sana kugundua, mara nyingi unaweza ona ni mtu mweusi mwenzako ndo anakuonea, kumbe huyo unae muona ni kibaraka.

So, kwa kifupi, wamarekani weusi wamefika mbali sana kisiasa, wameanza harakati za kupigania uhuru hata kabla ya kina Kwame Nkurumah, Nyerere na Lumumba. ni watu waliokomaa Zaidi katika kuelewa siasa na uchumi unavofanya kazi, kusema kweli, kielimu na kichangamoto, wametuzidi mbali sana, kama tukipima kwa ratio ya asilimia wale jamaa wanaweza kua na ratio ya 100:5, yani wao tunawapa asilimia 100 alafu sisi ni 5 kutoka kwenye mia zao.

Wamarekani weusi ukiwaleta Afrika na kuwapa nafasi za uongozi wanaweza kuibadili Afrika kwa speed kali sana, wana uwezo mkubwa wa kufikiria solution kwa haraka sana na wanauelewa mpana wa dunia inavokwenda. hebu imagine mamtu kama kina Malcom X na Marcus Garvey, yalikua ni mamtu hatari sana, Marcus Garvey huwezi linganisha na Nyerere au Nkurumah, yale majamaa yamefanikiwa katika mazingira magumu sana na yakapata popularity kipindi ambacho kulikua hakuna hata media, imagine mtu kama Marcus Garvey angeishi kipindi cha media, mmh, labda angetawala dunia. :p

Wale ni ndugu zetu tuwapende na tuwakaribishe, pia tusisahau wazungu kama kina John Brown, sio wazungu wote walipenda ile hali, John Brown ni mwanaharakati wa kizungu aliesalitiwa na mtu mweusi, lengo la John Brown ni kupinga utumwa. It's all about evil and good. Kuna watu weusi pia ni evil vile vile, so msiwe blinded na issue ya rangi japokua rangi pia ni factor sometimes, so umakini ni muhimu.
 
Black Americans hawajawahi kupewa chochote kwenye silver plate. Wamezaliwa kwenye mapambano.

Kuanzia kina Martin Luther, etc

Sisi tulipewa Uhuru kwenye sahani, bure bure tu.

Tumekuwa kama wacongo, kazi kukata mauno, na kuwasifia wenye pesa na madaraka ili tuishi.
 
wamarekani weusi ukiwaleta afrika na kuwapa nafasi za uongozi wanaweza kuibadili afrika kwa speed kali sana,
Kwa bahati mbaya historia inasema vingine.

Baada ya Wamarekani Weusi kurengenezewa Nchi yao ya Liberia kwenye Bara la Afrika walikuja na 'Ustaarabu' wa kibaguzi kama Ile waioukmbia.

Wakaanza kuwadharau Wenyeji na kuwatia Savages na kuwatenga na kuwaondoa.

Soma kisa cha Samuel Doe na Americo Liberians.
 
Black Americans hawajawahi kupewa chochote kwenye silver plate. Wamezaliwa kwenye mapambano.

Kuanzia kina Martin Luther, etc

Sisi tulipewa Uhuru kwenye sahani, bure bure tu.

Tumekuwa kama wacongo, kazi kukata mauno, na kuwasifia wenye pesa na madaraka ili tuishi.
hao jamaa wana akili kinyama, yani kiushiundani, unavokua unalinganisha viongozi wa afrika na watu kama malcom, au garvey, au martin unakua unawaonea, kichangamoto bado ni watoto sana, sisi tunahitaji pressure kali sana ya matatizo kama yao kufikia walipo, viongozi wa afrika wanaweza wakawa wazuri ila nafikiri hawajajengeka kichangamoto. wale jamaa wako mbali sana kiharakati and very very very very competitive. wamepigana vita vingi sana hadi kuwaona hapo walipo, ni ma legendary ambao wamepitia pressure ya Maisha kwa miaka 400, achana na hawa watu, hebu watafute afu usikie wanavochambua economics zao na siasa, ni noma wazee, ni hatari hawa watu. na unapowasikiliza usiwe blinded na jinsi wanavoongea, focus kwenye topic. maana unaweza sema kwa sababu kapiga tattoo simsikilizi, ndo tunapokosea.
 
Kwa bahati mbaya historia inasema vingine.

Baada ya Wamarekani Weusi kurengenezewa Nchi yao ya Liberia kwenye Bara la Afrika walikuja na 'Ustaarabu' wa kibaguzi kama Ile waioukmbia.

Wakaanza kuwadharau Wenyeji na kuwatia Savages na kuwatenga na kuwaondoa.

Soma kisa cha Samuel Doe na Americo Liberians.
unaambiwa wale waliopelekwa Liberia walitumika tu, we hujiulizi, yani mkoloni akutoe sehemu anayokufaidi na kukutumia akurudishe tu Liberia eti kisa uwe huru, kwani wenyewe walikua hawaitaki liberia
 
Nimekujibu hoja yako ya kwamba Wamarekani Weusi wakiletwa Afrika wanaweza kuwa Viongozi wazuri.

Sasa Ghafla unakuja na hoja nyingine kumbuka ni sisi wenyewe ndio tulikuwa tukiuzana Utumwa hao Waarabu walikuwa wakiwaletea Machifu wetu Ushanga na Bunduki ili wapewe Watumwa
 
Nimemjibu hoja yako ya kwamba Wamarekani Weusi wakiletwa Afrika wanaweza kuwa Viongozi

Sasa Ghafla unakuja na hoja nyingine kumbuka ni sisi wenyewe ndio tulikuwa tukiuzana Utumwa hao Waarabu walikuwa wakiwaletea Machifu wetu Ushanga na Bunduki ili wapewe Watumwa
poa mkuu
 
Marcus Garvey alitaka kuwarudisha awo jamaa afrika sema wazungu bado wakaona bila mtu mweusi america mambo hayataenda wakamuua.
 
Ukisikia hotuba za kina Martin Luther King Jr ,Malcom X nk ndo unatajua hawa jamaa ni moto wa kuotea mbali

Sio hawa wakina prof Lumumba ambao wamekuwa wapiga kelele hovyo hovyo
hayo majitu yalikua sooooooooooooo faaaaaaaaaar aheaaaaaaad of time, hata sasa wapo wengi tu, sema wanaminywa sauti.
 
Mazingira yanawafanya wawe juu kwetu kwa kila kitu.Uzaliwe USA halaf uwe kilaza kama upo timamu.
America ni developed nation hivyo raia wake wote lazima wawe na weledi mkubwa kulinganisha na mataifa mengine tukiwemo Africa.
Hata China imemepiga hatua kwa kuwatumia diaspora wa kichina waliokuwa USA.
Viongozi wa Africa wanahofia sana diadpora kwa sababu wanaweledi na exposure ya kutosha kuliko sisi waafrica.
USA inachota na kutumia maarifa ya waafrika( diaspora) kwa kiasi kikubwa sana huku sisi hatuna habari nao.
Nilishangaa kusoma kuwa MOSFET TRANSISTOR,security codes pamoja na teknolojia mbalimbali iligunduliwa na mmisiri.
Waafrika sasa tuamke tutumie damu zetu za nje kuleta maendeleo barani kwetu.
 
Mkuu umeliona na ww.
 
Sio hivo tu. Misri kuna technology zimevumbuliwa na mweusi ambazo sa hv tunazitumia. Wazungu walichofanya ni kwenda kufanya research tu. Kama kawaida empire zina rise na kufall. Egypt empire ilakaa mda mrefu kuliko empire zote duniani lakini ilikufa.
 
These people are very useful. Na viongozi wetu wa afrika wanawaogopa kama ukoma. Coz wanajua kwamba wakiwapa nafasi za ushindani watapoteza nafasi zao za utawala

Back
Top Bottom