Wamarekani wapoteza Dola Milioni 143 mwaka 2018 kutokana na ulaghai wa Kimapenzi Mtandaoni. Wanaijeria 167 na Wamarekani 74 ni miongoni mwa Watuhumiwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Maafisa wa FBI wamewashtaki watu 80 huku wengi wakiwa ni raia wa Nigeria wanaoishi Los Angeles kwa kujihusisha na biashara za udanganyifu wa kimapenzi ulimwenguni

FBI imeonya kuwa kashfa na udanganyifu huo wa kimapenzi mtandaoni zimewagharimu Wamarekani fedha nyingi kuliko kosa lolote la udanganyifu lililoripotiwa kwao mwaka jana

Shirikisho hilo la Uchunguzi limebainisha kuwa zaidi ya watu 21,000 walidanganywa na kutuma jumla ya Dola Milioni 143 (zaidi ya Tsh. Bilioni 328.8) kwenye miradi hiyo kwa mwaka 2018

Ripoti zinaonesha Walaghai hao wapo zaidi kwenye 'Dating Apps', lakini pia kwenye mitandao ya kijamii ambayo sio maalumu kwa kuunganisha wapenzi (Dating) kama Facebook

Mkurugenzi Msaidizi wa FBI, Paul Delacourt amesema Waathiriwa wanatumika kama wasafirisha fedha wa awali kwa kuruhusu akaunti zao kusafirisha fedha zilizoibwa

Washtakiwa wote watakabiliwa na mashtaka dhidi ya kula njama kutaka kulaghai, kula njama za kutakatisha fedha na wizi wa utambulisho

1.jpg

UPDATE
Oparesheni iliyofanyika Ulimwenguni kote imefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao wanatoka katika mataifa 12

Watuhumiwa 167 wanatoka nchi ya Nigeria, 74 kutoka Marekani, 18 Uturuki na 15 kutoka Ghana. Katika oparesheni kiasi cha Tsh. 8,506,300,000 zimerudishwa

Waliokamatwa wengi ni wanachama wa makundi ya kihalifu kupitia mtandao ambayo mengi yanatokea nchini Nigeria. Kwa muda mrefu raia wa Nigeria wamekuwa vinara wa wizi kwenye mitandao

Zoezi hilo limeendeshwa na Idara ya Sheria ya Marekani na Kamisheni ya uchunguzi wa uhalifu unaohusiana na masuala ya fedha na uchumi
********

Online romance scammers are busy stealing money and hearts across the United States.

Just this week, federal officials announced that they charged 80 people -- including Nigerians based in Los Angeles -- in businesses and romance scams worldwide.

The Federal Trade Commission has warned that scams that prey on vulnerable people cost Americans more money than any other fraud reported to the agency last year. More than 21,000 people were conned into sending $143 million in such schemes in 2018 alone, it reported.

2.PNG

And that number has skyrocketed in recent years, with losses that are almost quadruple 2015 figures.

"Reports indicate the scammers are active on dating apps, but also on social media sites that aren't generally used for dating. For example, many people say the scam started with a Facebook message," the FTC says.

As online dating becomes more popular and romance scams increase, the FTC warns people to become suspicious of any online relationship if:
  • The person wants to leave the dating site immediately and use personal email or messaging
  • The person is fast to claim love
  • They say they're traveling or working internationally
  • He or she says they want to visit but don't have the money because, for example, a business deal went sour
  • They ask for money without meeting face-to-face​
 
Back
Top Bottom