lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,147
- 33,302
Kauli hii Ni maarufu Sana kwa VIONGOZi wa awamu hii ya tano muhula wa pili."Mabeberu wasituingilie katika mambo yetu ya ndani, kwani sisi ni Taifa huru, uchaguzi ulikua huru na wa haki, Kama mtu hajaridhika aende Mahakamani"
Haya maneno yanasemwa Sana na Watawala kutoka CCM ya kizazi hiki.
Ila kwa kumbukumbu zangu na kwa kupitia maandiko mengi niliyosoma Ni kwamba, Wakati wa Utawala wa awamu ya kwanza ya Akina Nyerere Tanzania ilikua mstari wa mbele kuwapinga wakoloni na makaburu na Mabeberu waliokua wakiwatesa Waafrika na wanyonge wengine duniani.
Tanzania ilikua kiongozi wa nchi zilizoitwa nchi tano za mstari wa mbele kupigania ukombozi wa Afrika.
Nchi hizo Ni
Tanzania
Zambia
Angola
Msumbiji
Na
Zimbabwe.
Kinara alikua Ni Tanzania.
Kilichokua kinapiganiwa na Tanzania Ni kupinga uonevu wote dhidi ya Binadamu Kama Ubaguzi wa rangi na na ubaguzi wa Aina yoyote, Ukoloni, uonevu au ukandamizaji wa ndani uliokua ukifanywa na Marais au Watawala madikteta,wakoloni,Mabeberu na Makaburu wa Afrika kusini.
Watawala madikteta walikua Ni
Makaburu wa Kusini waliwabagua wazalendo weusi wa Afrika kusini,
Wakoloni waliwatawala bila ridhaa yao Waafrika na kwingineko,
Mabeberu walikua Ni Kama Mataifa yenye nguvu kuzitawala,kuzikandamiza na kizinyonya nchi changa
Madikteta walikua Ni kama kina Iddi Amini wa Uganda,Bokassa wa Afrika ya Kati,Mobutu seseseko wa Zaire,Kamuzu Banda wa Malawi,Watawala wa Sudani dhidi ya Wasudani Kusini Weusi na wababe wengine.
Hawa Ni baadhi.
Lakini wote Hawa kiboko yao alikua Ni Julius K Nyerere.
Aliwasaidi na kuwaunga mkono kwa Hali na Mali wale wote waliokua wakionewa,wakikandamizwa,kudhulumiwa,kubaguliwa,kuteswa na kila Aina ya manyanayaso hapa duniani.
Nyerere na CCM yake waliwasaidia kwa Hali na Mali.
Alitoa misaada kiserikali na kibinafsi.
Hata Hivyo Watawala wa nchi zote hizo walikua wakimpinga Nyerere kwa kauli zinazofanana na kauli zitolewazo Leo na Watawala wa Sasa kuwa,
"Nyerere asiingilie mambo yao ya ndani,kwani wao ni nchi huru".
Malalamiko ya wananchi wengi wa nchi hizo Ni kwamba walikua wanaonewa sawasawa kabisa na Wafanyiwavyo CHADEMA leo,ndipo Mwalimu na CCM ya wakati huo ikamuuma akajitolea kuwasaidi hai waliokua wanateswa.
Baadhi ya waliosaidiwa Ni,
Yoweri Museven wa Uganda
Raurel Kabila wa Zaire
Sam Nujoma wa Namibia
Wazalendo wa Afrika kusini na Namibia
John Garang wa Sudan
Kanyama Chiume wa Malawi
Na wengine wengi.
Watawala wa nchi KandamiI walimuona Nyerere anaingilia Mambo yao ya Ndani na wao Ni nchi huru.
Walimchukia Nyerere.
Leo hii,miongo mingi imepita na mambo yemekua kinyume, waliokua watetezi wa haki wamekua wakandamizaji,leo hii Wazungu wamekua watetezi wa haki na wakandamizaji leo wanadai wao Ni nchi huru wasiingiliwe katika mambo yao.
Wapinzani wanasulubiwa mchana kweupe,wanabaguliwa,wanateswa,wanafungwa nakila Aina ya uonevu na dhuluma Kama jinsi makaburu na madikteta walivyowafanyia wazalendo katika nchi zao.
Tanzania ilikua kimbilio la wanyonge,Sasa inakimbiwa na wanyonge.