Wamanyema wa Dar es Salaam katika TANU na siasa za kudai uhuru

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,796
31,809
Iddi Faiz Mafongo TANU Card No. 24
Iddi Tosiri TANU Card No. 25
Ndugu Wawili Katika Kupigania Uhuru wa Tanganyika, 1954

8lS-bGcfJLi-US4KM0clKL332ZwGi0MysIEH5ffaAkw=w680-h510-no

ushoto Kwenda Kulia: Idd Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere,
Saadan Abdu kandoro na Haruna Taratibu, Dodoma Railway Station, 1956

Wamanyema wanajulikana kama watu wenye harara na ya ushujaa. Mmanyema anaweza kuulipia fedha ugomvi ili na yeye awemo, na kadri mpinzani anavyokuwa na nguvu na hodari, ndivyo Mmanyema anavyofaidi ugomvi wake. Katika siku hizo Wamanyema walikuwa wameshikwa katika magomvi. Katika mwaka wa1941 ilibidi serikali, maimamu na masheikh wa msikiti mingine mjini Dar es Salaam kuingilia kati ili kuamua ugomvi uliowakumba Wamanyema kuhusu msikiti wa Manyema. Wamanyema hawakumstahi mtu yeyote, waligombana hata wenyewe kwa wenyewe. Hamaki hizi zilipoelekezwa kwa serikali ya kikoloni zilikuja kuwa na manufaa sana. Kwa kuwa walikuwa ni kabila la Waislam watupu, Wamanyema hawakuweza kufaidika na elimu iliyokuwa ipo mokononi mwa wamishionari. Hata hivyo Wamanyema walipiga hatua kubwa katika elimu ya dini yao na hii ndiyo sababu kuwa hadi leo utamaduni wa Kiislamu umeenea katika kila familia ya Mmanyema iwe nyumbani Kigoma au huko pwani. Mmanyema hayupo mbali sana na utamaduni wa Kiislam. Wamanyema, Warufiji na Wadigo ni katika makabila ambayo ni tabu sana kumpata Mkristo.
Idd Faiz alikuwa Mmanyema. Hadhi yake iliongezeka zaidi kwa kuwa alikuwa mweka hazina wa TANU. Vilevile aliifanyia kampeni TANU, akifuatana na Nyerere katika safari za awali za kukitangaza chama, akihutubia mikutano jukwaa moja na Nyerere. Ilikuwa ni Idd Faiz na kaka yake Idd Tosiri ndiyo waliompeleka na kumtambulisha Nyerere kwa binamu yao Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo. Ilikuwa ni baada ya utambulisho huu kwa Sheikh Ramia ndipo urafiki ukajengeka kati ya Sheikh Ramia na Nyerere na ndiyo Nyerere akakubalika Bagamoyo. Sheikh Ramia akiwa khalifa wa tariqa ya Qadiriya alikuwa na murid wengi waliomfuata kama kiongozi wao. Juu ya hayo alikuwa miongoni mwa wanachuoni walioheshimiwa sana. Hakuna kilichoweza kusimama na kuota mizizi Bagamoyo bila kupata ridhaa ya Sheikh Mohamed Ramia. Akiwa khalifa wa tariqa ya Qadiriya ambayo ilianzishwa na kustawishwa Bagamoya na baba yake, Sheikh Yahya Ramia, mwanzoni mwa karne ya ishirini, nguvu za Sheikh Ramia zilikuwa hazisemeki. Alichosema sheikh ndicho hicho kilichofuatwa.

upload_2016-4-21_0-4-45.gif

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Idd Faiz Mafongo alihudhuria mkutano wa uzinduzi wa TANU katika Ukumbi wa Arnautoglu. Haifahamiki kwa hakika hasa ni lini Idd Faiz alijiunga na TANU kwa sababu kadi yake ya kwanza ya uanachama ilipotea na akapewa kadi nyingine iliyokuwa na namba 915 iliyotolewa tarehe 28 Agosti, 1954. Lakini kwa kukisia tu kutokana na kadi ambayo Idd Faiz mwenyewe aliitoa kwa kaka yake Idd Tosiri ambayo ilikuwa kadi namba 25 na yenye saini yake kama afisa aliyetoa kadi hiyo, inaweza kuchukuliwa kwa uhakika kuwa Idd Faiz alikuwa miongoni mwa wale watu wa mwanzo kabisa kuingia TANU na huenda akawa miongoni mwa wanachama ishirini wa mwanzo. Ukichukua katika fikra ukweli kwamba Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya aliingizwa TANU na Mtemvu katikati ya mwezi Agosti, 1955, huenda Ally Mwinyi kama katibu wa Al Jamiatul Islamiyya na Idd Faiz akiwa mweka hazina, wote wawili waliingia TANU wakati mmoja.

Idd Faiz na nduguye Idd Tosiri, muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, walikuwa Wakusu, moja ya makabila ya Kimanyema, kwa upande wa baba yao; na Wabwali kwa upande wa mama yao. Wote wawili walikuwa katika Batetera Union (Congo Association), chama kilichokuwa kikiwaunganisha Wamanyema wa Tanganyika. Mzee bin Sudi alikuwa rais muasisi wa chama hicho na baada ya kifo chake Sheikh Hussein Juma alichaguliwa kushika nafasi hiyo. Batetera Union kilikuwa chama kilichoshikamana na chenye nguvu sana miongoni mwa vyama vya kikabila. Wamanyema ni kabila la Waislam watupu na kwa sababu hii hakukuwa na pingamizi katika kuunga mkono TANU. Batetera Union kilikuwa na nguvu sana kiuchumi kwa kuwa kilikuwa katika wafuasi wake, watu waliomiliki majumba na walihodhi takriban nusu ya nyumba zilizojengwa mjini Dar es Salaam kati ya vita kuu mbili za dunia. Uwezo huu wa kiuchumu uliwafanya Wamanyema kuwa wapinzani wagumu wa serikali ya kikoloni na uliwanyanyua hadi kufikia kuwa mbele katika siasa mjini Dar es Salaam na katika miji mingine ya Tanganyika. Umoja wa Wamanyema ndiyo uliojenga msikiti maarufu wa Wamanyema mwaka wa 1912 uliokuwa karibu na makao makuu ya African Association.

nyerere_departing_for_UNO.jpg

Iddi Faizi Mafongo Aliyevaa Kanzu Koti na Tarbush Uwanja wa Ndege
Dar es Salaam Akimsindikiza Nyerere Kwenda New York, UNO 1955
Wengine kuanzia kushoto ni Rashid Sisso, Robert Makange, Iddi Faizi Mfongo
Julius Nyerere, John Rupia na Bi. Titi Mohamed

Habari zaidi za Iddi Faiz Mafongo ingia:
Mohamed Said: Idd Faiz Mafongo Mweka Hazina wa Safari ya Nyerere UNO 1955

Mapacha Wawili Sheikh Hassan na Hussein Juma, 1958

2016%2B-%2B1

Kushoto: Sheikh Hassan Juma na pacha mwenzake Sheikh Hussein Juma

Katika kipindi hiki mashambulizi kwa wale Waislam walionekana wanaipinga TANU na Nyerere yalizidishwa. Sheikh Hussein Juma makamu wa rais wa UTP alikuwa na pacha mwenzake, Sheikh Hassan Juma. Sheikh Hassan Juma alikuwa akiendesha madrasa pamoja na shule ikiitwa Al Hassanein Muslim School, moja ya majaribio ingawa hafifu ya Waislam kujiendeleza katika elimu. Shule nyingi zilikuwa mikononi mwa wamisionari. Watoto wengi waliozaliwa mjini Dar es Salaam baada ya vita ya pili walisomeshwa Qur'an katika Al Hassanein chini ya Sheikh Hassan Juma. Wazazi waliwatoa watoto wao katika shule hii kwa sababu waliihusisha madrasa hii na upinzani dhidi ya TANU. Watoto hawa hawakuishia katika kuacha kuhudhuria madrasa bali walitunga nyimbo za kebehi ambazo waliziimba kwa sauti kubwa walipokuwa wakipita katika shule yao ya zamani ili kuwakebehi, Sheikh Hussein Juma na nduguye pacha Sheikh Hassan. Wazee wao hawakuona haja ya kuwakataza watoto wao tabia hii isiyofaa. Kwa kawaida ilionekana kwamba yeyote aliyekuwa anaipinga au hakujinasibisha na TANU, alikuwa adui.

Baada ya vumbi la kutafuta uhuru kutulia Sheikh Hussein Juma alibaki nyumbani kwake akisomesha dini na alikuwa Imam Namba Moja Msikiti wa Manyema ingawa alikuwa hafiki pale kusalisha. Lakini kwa heshima ya ilm yake Wamanyema waliona Sheikh Hussen Juma awe kwenye nafasi hiyo. Sheikh Hussein Juma alibakia katika nafasi hiyo ya Imam wa Kwanza hadi kufa kwake.​
 
View attachment 341210

Ben,
Inasikitish sana kuwa kwenye jengo la CCM Lumumba hakuna hata
kumbukumbu ya picha za wazalendo hawa.
 
Guasa...
Sheikh Hussein Juma
ni mtoto wa Sheikh Hassan.

Lakini Sheikh Yahya alichukua ubini wa baba yake
mdogo hivyo akajulikana kama Yahya Hussein.
Shukran jazillah nilikuwa kama nakumbuka historia hiyo ila sikuwa na uhakika sana ndio ikabidi nikuulize jazakallah lkheir maalim wangu.
 
Ilikuwaje Wamanyema wakawa wengi Dar es salaam ambako si asili yao?
Pia naomba unijibu kwanini pale Gerezani panaitwa jina hilo kuliwahi kuwa na gereza?
 
Kitulo,
Hata mimi sijui kwa nini Wamanyema ni wengi Dar es Salaam.
Na hata jina la Gerezani sijui kwa nini pakaitwa hivyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom