Wamachinga wote walioko kwenye hifadhi ya barabara, mbele ya taasisi za Umma, mbele ya maduka wapewa mwezi 1 kuondoka

RC Makalla ametoa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo wamachinga walio katika maeneo yafuatayo kuhama:

1. Kwenye hifadhi ya barabara

2. Waliojenga vibanda juu ya mifereji ya maji machafu

3. Mbele ya maduka

4. Mbele ya taasisi za umma

5. Mbele ya shule za msingi na sekondari

Jumaa kareem!
Waondoke waondoke
 
Hawa wachafuzi na waharibifu waondolewe, jiji limekuwa kama danguro
Nikweli unacho sema ila napenda kukumbusha wengi wao kwa sasa machinga ni wasomi waliokosa ajira hivyo wameingia mtaani kubuni ajira. Kwa bahati mbaya serikali imewachukua poa na sasa ndio jeshi hatari lenye nguvu ambapo akipatikana mtu wakuwasha moto serikali itasema pooo. Yani ni hatari ya noma.... Wewe huwenda una ajira ila wao hawana ajira na wana akili kuliko wewe. End
 
Kweli waondolewe, ila nguvu lazima! Tuache kujidanganya eti wapangwe vyema. Hapo ni mwendo wa vunja, mwaga, buruza vilungu faini, ndio itawezekana, na Hangaya aambiwe mapema, asije shtuka haya mambo, serikali lazima ipata lawama kidogo ila ni lazima, tofauti anataka kazi bila lawama!
 
Huyo ana akili timamu sio mkuu wa wilaya anayelazimisha benki kumkopesha mamilioni eti ya wamachinga wakati hajui idadi yao isitoshe hajui ataurudisha vipi mkopo..

Ataifanya serikali kuingia madeni yasiyo ya lazima na mbadala ni makodi kupanda.
Ni DC gani huyo mkuu, nilipitwa kidogo na udambwi udambwi wa matukio mjini kwa muda wa wiki mbili
 
Siyo wao bali ni uchumi wa nchi umefeli kutoa ajira.

Bidhaa huuzwa kwenye wateja siyo " kajificheni"

Kinachotakiwa ni kuwawekea utaratibu wa kisheria kule kule kwenye wateja!
Ingekuwa kajificheni hakupati wateja basi soko la Mbuzi loliondo kibaha lingekosa kabisa wateja.Maana lipo kajificheni lakini watu wanasafiri kutuata nyamachoma kajificheni hukohuko.Wamachinga wameachiwa ndo tumefika hapa.Hata ukijenga soko hawataki kuja.Kigogo Kuna soko,kisutu Kuna soko,Magomeni Kuna soko Lkn Wamachinga hawataki kwenda
 
Hawa wajinga sio wakuwachekea kabisa,ni waharibifu na wauaji. Nishashuhudia wakimuua jamaa mmoja akiwa kwenye Gari lake pale Mtaa wa Narung'ombe kisa kakanya bidhaa zao walizopanga njiani.
Yaani .wameziba barabara halafu Tena wanamdhuru anayetakiwa kutumia barabara.Matukio Kama hayo ndo yangetumika kuhalalisha kuwatoa
 
Kura gani maneno tu kwanza wengi hata vitambulisho hawana kelele tu. Makala safisha mji huo watu watakuelewa tu. tumia ustaarabu hawataki nguvu unazo hapa shida ni Rais na PM wako very weak kauli zao hata hujui wanataka nini. very sad
Exactly Wamachinga huwa hawapigi kura.Wanachoweza Ni kupiga tu miluzi Wakati wa kampeni msafara wa wagombea ukipita lakini kwenye kupiga kura usimtegemee machinga
 
Yaani vijana wadogo wenye ndevu mpya, nguvu mpya na ari mpya badala ya kwenda kufanya uzalishaji wanazunguka na saa, mikufu, spana n.k kutoka china eti unajenga uchumi wa nchi? Mkifuata kauli ya mama eti kuwatoa kiustaarabu mtakesha. Mzuka alioanza nao sasa hivi wangeshaondoka lakini naona kama anakatishwa tamaa.
Kuna machinga nilimuona pale mbezi mwisho anauza tambi za taa za chemli
 
Back
Top Bottom