Wamachinga wote walioko kwenye hifadhi ya barabara, mbele ya taasisi za Umma, mbele ya maduka wapewa mwezi 1 kuondoka

Sidhani kama itakuwa kazi nyepesi Kama anavyodhani na kuichukulia. Machinga limeshakuwa jeshi kubwa hivyo kuwaondoa kwenye maeneo yao kazi ipo.

Serikali ikiamua watatoka tu. Itakachofanya Serikali ni kufanya overnight operation Chingas wakiamka asubuhi wanakuta njia nyeupe vibanda na takataka zao nyingine vimeondolewa. Atakayeleta vurugu atadhibitiwa vilivyo. Hawa jamaa ni kero sana.
 
Kosa lote hilo ni la magufuli na ccm yake waliowaruhusu machinga wafanye biashara popote wanavyopenda kwa gharama ya kupinga mkono ccm kwenye chaguzi feki za 2020 sasa mshawatumia ndio mnajuwa sheria sasa hivi wachieni tu waweke biashara zao mpaka mbele ya ikulu.
Na kweli bhana, acha tu wauze mpaka ikulu. Si unajua nchi hii ni ya Watanzania wote, kwa hiyo haina shida. Upo sahihi!
 
Natamani kujua kilichopo kichwani kwa huyo Muheshimiwa.

Yaani kabisa kwa akili zake anaamini kuwa wataondoka kwa kuwa tu yeye kasema?.

Mkubwa wake keshaagiza 'wasisukumwe' sasa kama wasipoondoka atatumia mbinu gani mbadala kuwaondoa?.
hii nchi ni yetu sote sisi tunaganga njaa wenyewe wanatembelea V8 tena kwa gharama za kodi zetu,nasema mama ajiandae kama anadhani 2025 ni rahisi anapotea sana,maaanake kwasasa tumechoka sana kupita kiasi si kwa ugumu huu wa maisha na tozo gandamizi ,watanzania wengi tunatafuta hela ya kula sio kama wengine wanajilimbikizia,haki imepote sana kwenye taifa
 
Waungane,wakodishe ferem,kwa mfano wanne,wanaweza wakaungana,na kukodisha Frem,wakalipa kodi kwa kuchanga,wakalipa leseni kwa pamoja,wakalipa mapato kwa pamoja,na mwenye Frem akalipa kodi ya zuio(withholding tax).
Ni wazo zuri sana
Lipo mikononi mwao na sio Serikali
 
Hii ngoma ni ngumu. Kama serikali ipo serious na hili swala basi sio la kuwaachia wakuu wa mikoa na wilaya pekee.
ukweli ni kwamba wamachinga hawawezi kuondoka kiustaarabu.
ikiwezekana wizara ya ulinzi wanajeshi watumike kuwaondoa hawa mabwana
 
Wacha tusubiri mkuu, ila zoezi linaonekana ni gumu sana kwasababu wamachinga wamepewa kichwa sana, wakiguswa kidogo tu kilioo. Ni eidha serikali kuziba maskio au kuwaacha waendelee na biashara zao.
Mkuu hili zoezi wala sio gumu kabisa. Tatizo letu ni kufanya kazi bila kufuata SHERIA, taratibu na kanuni tulizojiwekea. Kiutawala tuna Serikali mbili: Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Hili suala ni la Serikali za Mitaa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na ina Waziri wa Serikali za Mitaa. Wizara inaendesha shughuli zake kwa kufuata taratibu walizojiwekea zikienda sambamba na Sheria Ndogondogo (by laws). Wakuu wa Mikoa na Wilaya wao kama Mwenyeviti wa Kamati za Ulinzi wao wahakikishe sheria zinafuatwa.

Kwanini wasizitumie sheria hizo kwenye zoezi hili. Aidha hawa wamachinga wapo chini ya Katibu Kata na watendaji wake. Tatizo ni kwamba viongozi wa juu wanapenda kuingilia shughuli za watendaji hawa ili wajulikane kisiasa. Tuwape uwezo, nyenzo na uhuru wa kiutendaji wanaweza kuwapanga wamachinga ndani ya wiki mbili Nchi mzima.
 
Ni muhimu kuwapanga na kuwaondoa taratibu bila vurugu kwasababu makosa yalifanywa na serikali kuwaachia wakajazana kila mahali. Machinga nao watii sheria bila shuruti. Hawana ukubwa wowote wa kuishinda serikali.
Sidhani kama itakuwa kazi nyepesi Kama anavyodhani na kuichukulia. Machinga limeshakuwa jeshi kubwa hivyo kuwaondoa kwenye maeneo yao kazi ipo.
 
Wewe unatembea tembea hapo Ufipa?
Mkuu, ile Gezaulole ya kule Kigamboni ni matokeo ya hawa wamachinga; wakati ule walijulikana kama wazururaji/vijana wasio na kazi maalumu. Ili kutatua tatizo la hawa vijana Serikali ilitenga eneo lile ambalo kwa wakati ule lilikuwa pori sawa na Msitu wa Pande. Kwa maandalizi ya Serikali ya TANU iliwapeleka vijana hao kule na wapatiwa kila kitu kwa mujibu wa sheria. Leo Gezaulole ni mji. Hivyo hawa wamachinga ni suala la kutafuta suluhisho la kudumu. Serikali iache kununua magari ya kifahari, fedha inayobaki itengeneze mkakati wa Kudumu wa hawa wamachinga ili iwe kama wa Gezaulole.
 
Hii ngoma ni ngumu. Kama serikali ipo serious na hili swala basi sio la kuwaachia wakuu wa mikoa na wilaya pekee.
ukweli ni kwamba wamachinga hawawezi kuondoka kiustaarabu.
ikiwezekana wizara ya ulinzi wanajeshi watumike kuwaondoa hawa mabwana
Mkuu, mimi siamini kuwa wamachinga ni wastaarabu. SERIKALI ndio iliyowaweka hapo, na sasa Serikali hiyo hiyo inawataka wapangwe vizuri ili wafanye biashara zao viziri, sasa huo ukaidi wao kwa SERIKALI iliyowapa go ahead ya kufanya biashara zao unaanzia/wanautoa wapi? Watakuwa hawana fadhila.
 
Back
Top Bottom