Wamachinga wote walioko kwenye hifadhi ya barabara, mbele ya taasisi za Umma, mbele ya maduka wapewa mwezi 1 kuondoka

Waondoke kwenda wapi?..

Miaka ya nyuma nasikia Makonda aliwatoa machinga wa Ubungo na kuwaonyesha eneo lingine la Mawasiliano pale.....
Waungane,wakodishe ferem,kwa mfano wanne,wanaweza wakaungana,na kukodisha Frem,wakalipa kodi kwa kuchanga,wakalipa leseni kwa pamoja,wakalipa mapato kwa pamoja,na mwenye Frem akalipa kodi ya zuio(withholding tax).
 
Yaani vijana wadogo wenye ndevu mpya, nguvu mpya na ari mpya badala ya kwenda kufanya uzalishaji wanazunguka na saa, mikufu, spana n.k kutoka china eti unajenga uchumi wa nchi? Mkifuata kauli ya mama eti kuwatoa kiustaarabu mtakesha. Mzuka alioanza nao sasa hivi wangeshaondoka lakini naona kama anakatishwa tamaa.
 
Huyo ana akili timamu sio mkuu wa wilaya anayelazimisha benki kumkopesha mamilioni eti ya wamachinga wakati hajui idadi yao isitoshe hajui ataurudisha vipi mkopo..

Ataifanya serikali kuingia madeni yasiyo ya lazima na mbadala ni makodi kupanda.
Nadhani hukusoma na kuelewa

USSR
 
Sijawahi kupafahamu Ufipa wala sina mpango wa kupafahamu.
Lazima ukubali kuwa machinga ni mtembezi wa kuuza bidhaa ndogo ndogo /duka litembealo, ukijifanya kuganda kodi kama zote wanazolipa wenzako zitakuhusu tu.
Swali lingine!!!?

Wale wa sagura sagura pale karume wanalipa kodi gani sawa na wafanyabiashara wengine. Swala la wamachinga halitofautiani na ufafanuzi wa kuhusu demokrasia alioutoa mh Rais SSH, kila nchi ina aina yake ya wa machinga. Hata USA wanao utaratibu wao wa kimachinga ambao unamgusa karibu kila raia wataifa hilo billionea na fukara/ legendari na odinarii. Utaratibu huo unaitwa street sells na ndio chanzo kikubwa cha hii mitumba tunayoletewa huku ya vitu vya nyumbani na magagulo.
 
Hawa wachafuzi na waharibifu waondolewe, jiji limekuwa kama danguro
Kosa lote hilo ni la magufuli na ccm yake waliowaruhusu machinga wafanye biashara popote wanavyopenda kwa gharama ya kupinga mkono ccm kwenye chaguzi feki za 2020 sasa mshawatumia ndio mnajuwa sheria sasa hivi wachieni tu waweke biashara zao mpaka mbele ya ikulu.
 
Hii ni kero kubwa sana. Sehemu za kutembea kwa miguu zinazibwa, watu wanalazimika kupita kwenye njia za magari.

Vituo karibu vyote vya mabasi sasa hivi ni kero tupu. Matokeo yake maeneo yale foleni haziishi, wanaishia kuhamisha vituo badala ya kuondoa wamachinga wanaoleta misongamano. Yaani kweli mtu anafungua duka la nguo pembeni ya kituo cha daladala?

Juzi nimeona hata pale Ubungo darajani sehemu ya watu kuvuka barabara wapo wanauza miwa.

Ila hakuna nia ya dhati kulitatua hili tatizo.
 
Back
Top Bottom