Wamachinga waomba walipishwe elfu 50 ya kitambulisho ili wasiondolewe mjini

jana nimepita kariakoo, nimekuta watu wanafanya biashara ndani ya barabara. Hawa wanaofanya biashara ndani ya barabara wanatakiwa waondolewe haraka wakati wanaofanya kwenye hifadhi ya barabara watafutiwe sehemu rafiki ila tukiendelea kuwachukulia poa ipo siku maafa yatatokea halafu tuanze kulaumiana.
 
Machinga ni mbinu ya kukwepa kodi
HAWA JAMAA WANAHARIBU KABISA MFUMO WA UKUSANYAJI KODI,MAANA WAFANYABIASHARA WAKUBWA WAO HAWAITAJI DUKA BALI HUITAJI GODAWN TU NA HUGAWA MIZIGO KWA MACHINGA
ushauri baada machinga kuondoka maduka yote yapewe nambari maalumu GPS ya pahala,kitambulisho cha taifa cha muhusika,n.k.
MASHINE ZA EFD ZIONDOLEWE.
UKADIRIAJI UREJESHWE.
 
Unataka kusema kwenye mapato 1.3trillion asilimia kubwa ni wa machinga? Kwa hiz 20 20 ?
Aisee check youe facts, mostly nenda TRA pale wakuambie mchangiaj mkubwa ni nani.
Usikute kampuni hata 20 hazifiki zinachangia hizo nashangaa mtu 1.3 ndio kaona nchi imefika, hii sio nchi ya kukusanya 1.3 sijui 570 billion zinaenda kwenye mishahara tu bado matumiz ya kawaida ya serikali. Hapa sio issue pesa tu ni kuweka mazingira ya kuvutia ya biashara maana kariakoo ni soko la kimataifa biashara zote lazima risiti zitoke serikali ipate na ukaguzi unakuwa rahisi leo hii hujui mmachinga nani na nani kanunua dukani unakuta machinga nje kapanga bidhaa hata duka la nyuma yake kama store na wenye maduka kimyaa wanauzia nje tu ndani supply tu. Wamachinga ni kichaka cha wafanya biashara kukwepa kodi inaweza kuwa sio wote lakini asilimia kubwa.
 
We kiazi, sio kodo zote zinakwepa. Import Duty ya bidhaa hizi imelipwa. VAT kwa kupitia bidhaa za machinga hazillipwi wakati mwenye bidhaa hizo hizo madukani analipa!!

Kujibu swali lako, tufanye TRA walisema ukweli kuwa tumekusanya 1.3m. Nikurejeshw kwa Rais kufuta kesi 147 na kufungulia watu accounts zilizokuwa zimezuiliwa. Kwa kuwe wewe unakula na kulala kwa shemeji yako habari nyingine ni hii - makusanyo mengi yalikuwa ni arrears za kubambikiza za TRA. Enzi hizo hata mikopo ya kibiashara iliitwa “fedha za ndani”. Baada ya arrears kuisha sasa makusanyo ni halisi. Ndio maana wamebanua wigo wa tozo na ushuru kwenda kwenye simu na majengo (na bado mpk kodi ya kichwa itarudi).

Changamoto: mbona hatusikii tena tambo za makusanyo?? Sijui kwanini mnasahau haraka namna hii!
Hizo arrears ilisababishwa na nani
 
Kijijini mnalima wote?!
Hawatalima wote ila hivyo vitu wanavyouza mjini pia vijijini Sasa hivi vinahitajiwa maana maendeleo yamepelekwa vijijini mfano umeme Sasa vifaa vya umeme vitahitajika huko vijijini na ufundi pia, barabara zinatengenezwa Ili iwe rahisi kuchukua vitu mjini na kupeleka kuuza vijijini.
 
HAPANA: wasajili biashara zao waweke sehemu rasmi za kufanyia biashara; wasiwazuie wenzao wenye maduka na wala wasipange bidhaa barabarani.

Kama wanataka mfumo wa kupanga bidhaa barabarani wafanye biashara kuanzia saa 12 jioni na walipe 50000 kwa mwaka.
 
HAPANA: wasajili biashara zao waweke sehemu rasmi za kufanyia biashara; wasiwazuie wenzao wenye maduka na wala wasipange bidhaa barabarani.

Kama wanataka mfumo wa kupanga bidhaa barabarani wafanye biashara kuanzia saa 12 jioni na walipe 50000 kwa mwaka.
Duh
 
Ulime ili ukauze wapi? System ya kilimo ingekuwa na tija hamna mtu ungemuona mjini humu tena mashamba yangekuwa ishu kupatikana yani😅
umejaribu kulima? hebu tuondolee domokaya, jitu zima kchefuchefu, bureee kbisa
 
Ulime ili ukauze wapi? System ya kilimo ingekuwa na tija hamna mtu ungemuona mjini humu tena mashamba yangekuwa ishu kupatikana yani😅
umejaribu kulima? hebu tuondolee domokaya, jitu zima kchefuchefu, bureee kbisa
 
Back
Top Bottom