mkorinto
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 30,703
- 37,313
siku ukiacha upungasese mambo yatakunyookea sana.
Hivi huyu anaeongea hapo kwenye picha nayeye ni machinga?WAMACHINGA WAOMBA KUKUTANA NA RAIS SAMIA
Wamachinga waomba kuonana na Rais Samia kabla ya fedha bil 5 zilizotolewa kwa ajili ya kuboresha maeneo ya kufanyia biashara wamachinga kutumika, wamachinga wa mikoa yote wapo tayari kuonana na Rais na kumueleza Yale hasiyoyajua kuhusu wao View attachment 1980901View attachment 1980902
View attachment 1980905View attachment 1980904View attachment 1980903
Tatizo hili la watu kufanya biashara katika sehemu zisizo rasmi ni lazima lichukuliwe kwa uzito wake kwamba kufanya hivyo ni kuvunja sheria na katu lisivhukuliwe kisiasa. Hawa wamachinga wengi wao kwa kufanya biashara zao wanachafua miji na makazi ya watu na pia huzikosesha halmashauri mapato mengi.Wafuate Utaratibu Wa Kupangwa Kwaanza
TII SHERIA BILA SHURUTII
Mikutano Hapana Kuna COVID ni
Hata haieleweki,mtu anapanga nyanya chungu,mwingine maandazi wote Sasa wanajiita machinga
Mimi kwa tafsiri yangu najuisha wale wote wanaofanya shuhuri zao za biashara za aina zote kwenye sehemu ambayo sio rasmi kuwa ni WAMACHINGA.
Mmmh!Aendelee kupumzika kwa amani🙏
Mkuu hizi ndo mbinu za serikali. KUTENGENEZA TATIZO > KUSOLVE TATIZO > KUJINYAKULIA UMAARUFU.Ni Wamachinga wameomba Kukutana na Rais Samia au ni 'Mkakati' umesukwa vyema na 'System' ili Wamachinga jana wafanye Fujo kisha Mama ( Rais ) ajitokeze Kuwasikiliza na awape Suluhu ya Kudumu ya Maamuzi ya Kuwapendelea Wamachinga na Kuwapoza kisha apate Sifa ya kuonekana kuwa anawapenda na kuwajali Wamachinga?
Acheni Kutufanya Watu wote ni Majuha.
Ni mbinu ya Kipumbavu iliyojaa Unafiki.Mkuu hizi ndo mbinu za serikali. KUTENGENEZA TATIZO > KUSOLVE TATIZO > KUJINYAKULIA UMAARUFU.
Hii picha huwa inakuwasha sana.......
Ili wazibe mitalo nakupanga vitu vikizuia kuona maduka ya wengine?Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (Shiuma) limemuomba Rais Samia Suluhu Hassan akutane nao kumweleze kero walizonazo ili ajue namna ya kuzifanyia kazi.
Hayo yamesemwa leo Jumatano Oktoba 20, 2021 na Makamu Mwenyekiti wa wamachinga Taifa, Steven Lusinde wakati akitoa ufafanuzi kuhusu vurugu za wamachinga zilizotokea jana katika soko la Kariakoo.
Soma hapa:Machinga waanza kuhamishwa Lusinde alisema Samia ndiye Rais wa kwanza kutenga fungu la fedha kwa ajili ya maendeleo ya wamachinga na kwamba mkutano huo utamwezesha kupokea maoni kutoka kwao moja kwa moja nini Sh5 bilioni zifanye kwa manufaa ya wajariamali hao wadogo.
“Tunamshukuru sana Rais ametoa zaidi ya Sh5 bilioni kuhakikisha yanaorodheshwa maeneo hayo kwa ajili ya wamachinga, sisi tupo pamoja na yeye akutane na sisi wamachinga wa mikoa yote tumueleze hata asiyoyajua.
“Yeye mwenyewe apange wapi ili tumweleze changamoto zetu na tushauri fedha hizo zinaweza kutatua changamoto zipi mengi yasiweze kutokea, tunashkuru suala hili amekasimisha kwa wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi hivyo utekelezaji umewezekana,” amesema Lusinde.
Amesisitiza kuwa viongozi wanatakiwa wawashirikishe machinga maeneo wanayotaka kwenda kuwaweka ili kuondoa sintofahamu.
“Watushirikishe sisi changamoto zipo, ukiangalia maeneo mengi waliyoenda bila usumbufu walitushirikisha tunaamini kila kitu kitaenda sawasawa,” amesema Lusinde.
Makamu mwenyekiti Shiuma mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Namoto amesema viongozi wa kundi hilo wana wajibu wa kuishauri Serikali katika kufanya maboresho changamoto zilizopo katika hayo maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wamachinga wanakuwa na mazingira bora ya biashara.
Soma hapa: Machinga Mwanza waanza kuhama, watishia kurejea barabarani
Mmachinga eneo la Shekilango, Mohamed Shaban amesema ameamua kubomoa banda lake kwa kufuata sheria bila shuruti hata hivyo amesema eneo analopelekwa halina biashara za uhakika ikilinganishwa na alipokuwepo.
Chanzo: Mwananchi
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Sasa hili ni jipu.Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (Shiuma) limemuomba Rais Samia Suluhu Hassan akutane nao kumweleze kero walizonazo ili ajue namna ya kuzifanyia kazi.
Hayo yamesemwa leo Jumatano Oktoba 20, 2021 na Makamu Mwenyekiti wa wamachinga Taifa, Steven Lusinde wakati akitoa ufafanuzi kuhusu vurugu za wamachinga zilizotokea jana katika soko la Kariakoo.
Soma hapa:Machinga waanza kuhamishwa Lusinde alisema Samia ndiye Rais wa kwanza kutenga fungu la fedha kwa ajili ya maendeleo ya wamachinga na kwamba mkutano huo utamwezesha kupokea maoni kutoka kwao moja kwa moja nini Sh5 bilioni zifanye kwa manufaa ya wajariamali hao wadogo.
“Tunamshukuru sana Rais ametoa zaidi ya Sh5 bilioni kuhakikisha yanaorodheshwa maeneo hayo kwa ajili ya wamachinga, sisi tupo pamoja na yeye akutane na sisi wamachinga wa mikoa yote tumueleze hata asiyoyajua.
“Yeye mwenyewe apange wapi ili tumweleze changamoto zetu na tushauri fedha hizo zinaweza kutatua changamoto zipi mengi yasiweze kutokea, tunashkuru suala hili amekasimisha kwa wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi hivyo utekelezaji umewezekana,” amesema Lusinde.
Amesisitiza kuwa viongozi wanatakiwa wawashirikishe machinga maeneo wanayotaka kwenda kuwaweka ili kuondoa sintofahamu.
“Watushirikishe sisi changamoto zipo, ukiangalia maeneo mengi waliyoenda bila usumbufu walitushirikisha tunaamini kila kitu kitaenda sawasawa,” amesema Lusinde.
Makamu mwenyekiti Shiuma mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Namoto amesema viongozi wa kundi hilo wana wajibu wa kuishauri Serikali katika kufanya maboresho changamoto zilizopo katika hayo maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wamachinga wanakuwa na mazingira bora ya biashara.
Soma hapa: Machinga Mwanza waanza kuhama, watishia kurejea barabarani
Mmachinga eneo la Shekilango, Mohamed Shaban amesema ameamua kubomoa banda lake kwa kufuata sheria bila shuruti hata hivyo amesema eneo analopelekwa halina biashara za uhakika ikilinganishwa na alipokuwepo.
Chanzo: Mwananchi
Hahaha.Wafuate Utaratibu Wa Kupangwa Kwaanza
TII SHERIA BILA SHURUTII
Mikutano Hapana Kuna COVID 19