Wamachinga wakubaliana na Serikali

blix22

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
213
645
Na. Mwandishi Wetu

Uongozi wa Wanyabiashara Wadogo Wadogo maarufu kama Machinga wamekubaliana na uwamuzi wa serikali wa kuwapanga katika mfumo mpya na rafiki kwenye mikoa yote nchini.

Wakizungumza hayo kwenye mkutano maalum kati ya Shirikisho la Umoja wa Machinga(SHIUMA) na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi zao zilizopo Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, ambapo Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Taifa pia Mwenyekiti wa Wamachinga kwenye Soko la Kariakoo amesema wamekubaliana na mfumo mpya ulioanzishwa na Serikali wa kuwatafutia maeneo rasmi na rafiki kwa biashara zao.

Walipokea maagizo hayo kwenye kikao kilichofanywa na Waziri Mkuu pamoja na wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi na kuwaagiza wahakikishe wanashirikiana na viongozi wa wamachinga ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa vizuri. Hivyo, Uongozi wa wamachinga watahakikisha wanatoa elimu kwa wafanyabiashara hao na kuishauri serikali kutotumia nguvu kuwahamisha kutoka kwenye maeneo yasiyo rasmi,Na wamefanikiwa kwa asilimia 90 ambapo wafanyabiashara hao wamehama bila shuruti na kuiomba serikali kuwafanyia maboresho na kuwapa maeneo rafiki ya kufanyia biashara.

“Changamoto za hapa na pale zipo kwa sababu sisi ni binadamu , lakini ukizingatia mtu ana miezi sita hadi mwaka yupo kwenye eneo hivyo kumuhamisha ni changamoto lakini tunaendele kutoa elimu”alisema Steven Lusinde.

Amesema kuwa kutokana na sintofahamu iliyotokea Octoba 19 kwenye mitaa ya Msimbazi na Uhuru jijini Dar es Salaam Lusinde amesema kwamba walijitokeza watu ambao hawapo kwenye kundi la wafanyabiashara na kuanzisha vurugu kwa lengo la kuharibu utartibu huo uliopangwa na serikali na kuhamasisha mgomo , hivyo walitumia nafasi hiyo kushukuru jeshi la polisi waliojitokeza kuimarisha usalama.

Pia, wametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samuia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha shilingi bil 5/- kwa wamachinga ili kuwasaidia katika kutafuta na kuboresha maeneo mapya ya kufanyia biashara na kumuomba akutane nao kabla ya fedha hizo kuanza kutumika katika maeneo husika ili aweze kujua changamoto zingine zinazowakabili.

“Kwa niaba ya wamachinga wote Tanzania tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuwa na nia njema na wamachinga, pia kwa kutoa fedha shilingi bil 5/- za maboresho ya maeneo ya kufanyia biashara, na inawezekana akawa ni rais wa kwanza kutoa fedha kwa wamachinga, Tulikuwa kukishuhudia Halmashauri na maeneo mingine miaka ya nyuma iliyopita zilikuwa zinatengwa fedha sio kwa ajili ya wamachinga bali zinatengwa ili kuhakikisha machinga haonekani kabisa mjini” ameeleza Lusinde.
 
Back
Top Bottom