Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli wa kutoa vitambulisho kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) nchini, umepongezwa na kufurahiwa na Wafanyabiashara hao kwa madai kuwa, zitasaidia sana kuondokana na kero za kukimbizwa mara kwa mara na Askari wa mgambo.
Wafanyabiashara hao wamedai wanasubiri kwa hamu vitambulisho hivyo na kuipongeza sana hatua hiyo kuwa ni nzuri. "Kama biashara inafanyika bila bugudha, Sh. 20,000 ni kiwango kidogo kuchangia kwa mwaka. Wamachinga wengi hilo liko ndani ya uwezo wao."
Vitambulisho 25,000 vimetolewa kwa kila Mkoa na kitapatikana kwa gharama ya Tsh. 20,000 kila kimoja kwa lengo la kuwatambua Wafanyabiashara hao.