Wamachinga kuwekwa kundi moja na wanawake watoto na walemavu ni matusi kwao

mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
4,113
6,307
Nimesikia kwamba wamachinga wamewekwa kwenye wizara inayoshughulikia wanawake,wazee, watoto na kundi Maalumu (walemavu).

Nafahamu kuna baadhi ya wamachinga wachache ni walemavu na wanaweza kufall kwenye hiyo wizara kusaidiwa.

Nafahamu pia sio walemavu wote hawajiwezi kuna baadhi yao wachache wanajiweza na wala hawahitaji kuwekwa kwenye kundi maalumu.

Ila hii ya kuamua kwamba wamachinga wote kuwekwa kwenye kundi maalumu ni kichekesho cha mwaka , wamachinga wangetakiwa waundiwe idara yao kwenye wizara ya biashara na sio kuwekwa kwenye hiyo wizara inayodili na watu wasiojiweza wanaoonewa.

Wamachinga ni kundi la wapiganaji ambao wanatakiwa wawezeshwe na sio kutetewa kama wanawake,watoto, wazee au walemavu wasiojiweza.

Hao watu waliomshauri rais afanye hivyo wamempotosha kama ni yeye mwenyewe kaamua hivyo basi na awaombe radhi kwa kuwakosea heshima
 
Serikali haija watendea haki wamachinga kwa kuwaweka kwenye hii wizara

Kwa kuwa hii wizara imejikita Hasa kwenye maswala haya:

Jinsia- wanawake, LGBTQ (kulihudumia hili kundi Kwa Mambo mbalimbali)

Wazee - kupewa matunzo na kuishi vizuri.

Makundi Maalumu - kuwapatia mahitaji yao malemavu, hapa hata LGBTQ wanaingia tena kupewa huduma na mahitaji hao mbalimbali

Walitakiwa wa wekwe kwenye wizara ya viwanda na biashara

Kwa sababu wanasaidia kuuza bidhaa mbalimbali zinazalishwa viwandani, zikiwemo bidhaa za nje na ndani ni

SS mumewafanya wamachinga sio tena wafanya biashara, matatizo Yao ya kibiashara ya tatatuliwa kwenye madawati ya jinsia,wazee pamoja na walemavu

Hii inaonyesha jinsi gani serikali (taasisi ya ikulu) haina washauri wazuri
 
... abadili jina la wizara lisomeke Viwanda, Biashara, na Ujasiriamali; neno ujasiriamali linameza kundi kubwa sana hadi wafuga kuku na wachoma chapati wanaingia hapo; ndio de facto standard kwa ukanda huu kuhusiana na jina la wizara hiyo.
 
... abadili jina la wizara lisomeke Viwanda, Biashara, na Ujasiriamali; neno ujasiriamali linameza kundi kubwa sana hadi wafuga kuku na wachoma chapati wanaingia hapo; ndio de facto standard kwa ukanda huu kuhusiana na jina la wizara hiyo.
 
... abadili jina la wizara lisomeke Viwanda, Biashara, na Ujasiriamali; neno ujasiriamali linameza kundi kubwa sana hadi wafuga kuku na wachoma chapati wanaingia hapo; ndio de facto standard kwa ukanda huu kuhusiana na jina la wizara hiyo.
kabisa mkuu hapo angeeleweka ila sio huu upuuzi
 
Huku kuwekana kwenye makundi ni kupoteza tu pesa katika administration..., walete sera zinazoeleweka za kupunguza wabangaizaji mtaani..., haya mengine yote ni majibu rahisi kwa maswali magumu.
 
... abadili jina la wizara lisomeke Viwanda, Biashara, na Ujasiriamali; neno ujasiriamali linameza kundi kubwa sana hadi wafuga kuku na wachoma chapati wanaingia hapo; ndio de facto standard kwa ukanda huu kuhusiana na jina la wizar

Mama yetu anazi kupewa matango Pori
Na hata ashtukii🤣🤣
 
Manchinga ni kundi la wapambanaji wa kijasiriamali! Si kundi dhaifu! Wanavunjiwa vibanda vyao hawakati tamaa wanarudi kwa mkakati mwingine! Wanapambanana mgambo wamo! Wanachomewa maeneo yao kesho wanarudi kama woote! Hawaliilii kwa hasara kesho utawakuta na bidhaa zimejaa! Wamanchinga wanastahili heshim
 
Back
Top Bottom