Wamachinga kando ya kuta za viwanda Mbagala, usiku hutoboa na kuiba

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,590
22,197
Barabara ya Zakhiem Mbagala Rangitatu ina vibanda vingi vya wamachinga kando ya kuta za viwanda, wamachinga hawa wanalindwa na mamlaka kwa hali na mali kwa sababu ndio wapiga kura wetu.

Wapigakura hawa wenye vibanda nyakati za usiku hugeuka nguchiro na kuanza kutoboa kuta za viwanda kwa ajili ya kuiba ndani ya viwanda, huu ndio uwekezaji mkubwa wa wapigakura wetu hawa na kiwanda kilichoathirika sana ni cha Maji Poa.

Tatizo hili si huko tu hata maduka yanayobanwa na wamachinga nayo hukabiliwa na wizi wanaotumia mbanano kuwa kinga.
 
Hili tatizo lililelewa na kayafa

Na Hawa viongozi tuliobaki nao wote wamelemaa na ugonjwa huu wa kuwaacha wamachinga wavunje taratibu zetu bila kuchukuliwa hatua, karibu miji yote na halmashauri nyingi tu zimevamiwa na wahusika Tarula, tanroad, halmashauri, Police, maDiwani , mgambo, ...etc hakuna anayewajibika, angalia leo inchi nzima tatizo la bodaboda Linavyosumbua traffic ambao Sasa Ni wazi kuwa hawana control nao
 
Inatia hasira halafu inaudhi mno
 
Hap TARURA ndio hovyo kabisaa kazi yao kuvizia magari yanayoegesha pembezoni mwa barabara
 
TARURA hawawezi kuwagusa wamachinga na hakuna anayeweza kuwagusa isipokuwa Rais tu, hata Waziri Mkuu hana ubavu wa kuwagusa wamachinga. Tunamsikia Mkuu wa Mkoa akijibaraguza kuhusu wamachinga lakini huishia kuwatuma Wakuu wa Wilaya huku akijua hawawezi kuwafanya kitu, serikali imewajengea jeuri ambayo inahatarisha usalama wa wananchi wengine. Jana nilimsikia Mkuu wa Mkoa Dar. akifikiria uwezekano wa kufunga baadhi ya mitaa ili itumiwe na wamachinga! Nilijiuliza kuhusu wakazi wa mitaa hiyo pamoja na wenye maduka, je, watahamishwa? Ni wazi kauli ile ni ya kutapatapa.
 
Mzaha mzaha litakuja kuleta mapigano makubwa kati yao na polisi, tukumbuke kunasiku walimuua mfanyabiashara wa Kariakoo baada ya gari yake kukanyaga nyanya kwa bahati mbaya na hakuna hatua yoyote ilichukuliwa.
Duh!
Hiyo hatari sasa
 
Katika hali ya udhaifu wa viongozi wetu ni pale wamachinga wanaporuhusiwa kuuza pombe muda wote katikati ya barabara! Wenye baa ambao wanalipa kodi wakiuza pombe mchana wanakamatwa na ukikutwa unakunywa baa saa za kazi unakamatwa lakini kwa wamachinga haukamatwi!
 
Back
Top Bottom