Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,042
- 33,527
Kuna msemo kuwa "uongo ukisemwa sana hugeuka kuwa kweli" ndivyo ninavyoona kwenye jina linalotumiwa na watu wengi kuwatambulisha wafanyabiashara wafanyao biashara kwa kutembeza mitaani ama kutandika barabarani.
Si kweli kwamba jina wamachinga limetokan na neno la Kiingereza la "Marching Guy" bali asili ya neno hilo linatokana wafanyabiashara wa kutembeza biashara mitaani mwanzoni mwa miaka ya themamanini wengi wao kutokea mkoani Mtwara.
Watu waliokuwa wanaishi Dar es salaam miaka ile baada ya hali ngumu ya uchumi kupita, watakumbuka jinsi wamachinga walivyokuwa wanapita mitaani wakiwa na bidhaa mbali mbali hasa za Urembo na vyombo vya Plastiki na bati wakiuza.
Waingereza watu wa aina ya wamachinga wa Tanzania wao wanawaita "Hawkers" . Inakuwaje kwao wawaite "Hawkers" eti hapa waje kuwaita "Marching Guys" na wala hilo neno lenyewe la "Marching Guys" halisadifu hata kidogo aina ya biashara inayofanywa na Machinga wa Tanzania.