Wamachinga haitokani na Marching Guy!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
17,871
33,235
Kuna msemo kuwa "uongo ukisemwa sana hugeuka kuwa kweli" ndivyo ninavyoona kwenye jina linalotumiwa na watu wengi kuwatambulisha wafanyabiashara wafanyao biashara kwa kutembeza mitaani ama kutandika barabarani.

Si kweli kwamba jina wamachinga limetokan na neno la Kiingereza la "Marching Guy" bali asili ya neno hilo linatokana wafanyabiashara wa kutembeza biashara mitaani mwanzoni mwa miaka ya themamanini wengi wao kutokea mkoani Mtwara.

Watu waliokuwa wanaishi Dar es salaam miaka ile baada ya hali ngumu ya uchumi kupita, watakumbuka jinsi wamachinga walivyokuwa wanapita mitaani wakiwa na bidhaa mbali mbali hasa za Urembo na vyombo vya Plastiki na bati wakiuza.

Waingereza watu wa aina ya wamachinga wa Tanzania wao wanawaita "Hawkers" . Inakuwaje kwao wawaite "Hawkers" eti hapa waje kuwaita "Marching Guys" na wala hilo neno lenyewe la "Marching Guys" halisadifu hata kidogo aina ya biashara inayofanywa na Machinga wa Tanzania.
 
Correct!
Kwa kuongezea tu neno 'machinga' limekuwa borrowed to english na lipo kwenye oxford dictionary.
Kwahiyo neno machinga ni kishwahili pia ni kiingereza kama ilivyo kwa maneno 'shamba' ,'matatu' ,'mzee' 'panga' ,'safari' na mengine mengi.
Hii dunia usipotafuta maarifa utadanganywa mpaka unakufa.
 
1546023292662.png
 
Sawa umepinga kuwa sio marching guys bali hujasema hilo neno limetokea wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeelezea kuwa ni kutokana na waliokuwa wanafanya biashara ya kutembeza bidhaa hasa kwenye jiji la Dar es salaam miaka ya mwanzoni mwa themanini kuwa ni watu kutoka mtwara. Kwa ivo watu wakawa wanaulizana "hiyo bakuli umenunua wapi" na mnunuzi hujibu " nimenunua kwa wamachinga" muuliza swali huelewa kwamba imenunuliwa toka kwa watu watembezao bidhaa mitaani.
 
Kwa hiyo watu kutoka Mtwara ndiyo sababu ya kuitwa Wamachinga,kivipi? Hebu unganisha maana ya neno Wamachinga kwa uchuuzi mitaani,ulinganishe watu wa kusini hasa Mtwara,corelation iko wapi hapo? Hujatoa sababu. Kutoka Mtwara hakuwez kuwa ni sababu ya neno Wamachinga. Na kule Mtwara hakuna sehemu au affiliation yoyote na neno Wamachinga. Sababu yako inakosa hoja ya kimantiki. Hoja ile ya Matching Guys ina mashiko kuonyesha uchuuz(literally-Swahili-English direct interpreration)!
Tafuta sababu,hapo umekosa sababu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta sababu,hapo umekosa sababu.
Kwanza sina sababu ya kutafuta sababu kwani huo ndiyo ukweli na uhalisia. Sasa "Correlation" ya "Marching Guys" na "Wamachinga" iko wapi? Au kwa kuwa kimatamshi ni kama yanafanana?

Kwenye kiswahili kuna kundi la maneno "Mwa" ambalo neno "mmachinga" linakuwa "Wamachinga" sasa "marching Guys" iweje iwe "Wamachinga"?

Nimetoa Historia ambayo ni ya kweli wewe unaleta mapokeo ya zama hizi. Unaikumbuka bendi ya "Nchinga Sound" iliyokuwa inaongoza na Muumini Mwinyijuma? Sasa huko Nchinga ndiko wamachinga wanapotoka na wao ndiyo asili ya watembeza vitu mtaani kuitwa wamachinga.

Nimesema kwamba wazungu wamachinga wanawaita "Hawkers" basi ni kwa nini hawa wa huku kwetu waje wawaite "Marching Guys" wakati wanafanya biashara kwa mtindo unaofanana na ule wa "Hawkers" wa kule kwao?
 
Limetokana na watu wanaotoka nachingwea wachinga

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe uko sahihi kabisa kwanza neno machinga halijaanza zamani sana nazani ni miaka ya 90 na hivi wakati huo walioanza kufanya kazi ya umachinga walitokea huko nachingwea na mtu mwingine yeyote akifanya kazi hiyo ilizaniwa ametokea huko na asili Yao hao watu wa nachingwea ni wachinga na ndio kitu ambacho kimezaa jina la machinga leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kinandinandi nikurekebishe kidogo. Ni kuanzia miaka ya 1986 na kuendelea ndiyo wamachinga walipovamia Dar na biashara yao ya kutembeza vitu. Nadhani ni kutokana na kuisha zama za "Hali ngumu ya uchumi" ndiyo na wao walipogundua kutembeza vitu na kuuza mitaani ni biashara kubwa sana!!
 
Kwanza sina sababu ya kutafuta sababu kwani huo ndiyo ukweli na uhalisia. Sasa "Correlation" ya "Marching Guys" na "Wamachinga" iko wapi? Au kwa kuwa kimatamshi ni kama yanafanana?

Kwenye kiswahili kuna kundi la maneno "Mwa" ambalo neno "mmachinga" linakuwa "Wamachinga" sasa "marching Guys" iweje iwe "Wamachinga"?

Nimetoa Historia ambayo ni ya kweli wewe unaleta mapokeo ya zama hizi. Unaikumbuka bendi ya "Nchinga Sound" iliyokuwa inaongoza na Muumini Mwinyijuma? Sasa huko Nchinga ndiko wamachinga wanapotoka na wao ndiyo asili ya watembeza vitu mtaani kuitwa wamachinga.

Nimesema kwamba wazungu wamachinga wanawaita "Hawkers" basi ni kwa nini hawa wa huku kwetu waje wawaite "Marching Guys" wakati wanafanya biashara kwa mtindo unaofanana na ule wa "Hawkers" wa kule kwao?
Hawker = Vendor.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Street hawkers = Street vendors

Yaani "Wamachinga" kama wanavyoitwa Kibongobongo.
 
kinandinandi nikurekebishe kidogo. Ni kuanzia miaka ya 1986 na kuendelea ndiyo wamachinga walipovamia Dar na biashara yao ya kutembeza vitu. Nadhani ni kutokana na kuisha zama za "Hali ngumu ya uchumi" ndiyo na wao walipogundua kutembeza vitu na kuuza mitaani ni biashara kubwa sana!!
Tuko pamoja ndugu hiyo wanayo dai kwamba limetokana neno la kiingeleza wanapotosha na wanawaaminisha watu vibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom