wamachinga DAR wafichua siri ya wanasiasa kuwashirikisha katika maandamano haramu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wamachinga DAR wafichua siri ya wanasiasa kuwashirikisha katika maandamano haramu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mujumba, Mar 11, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WAFANYABIASHARA katika jengo la Machinga Complex, Dar es Salaaa, wamefichua mpango wa baadhi ya wanasiasa kuwashawishi ili washiriki maandamano. Mbali ya hilo, wamewaomba Watanzania wakubali kwamba serikali ya awamu ya nne imefanya na inaendelea kufanya mambo makubwa na mazuri yenye lengo la kuboresha biashara zao, hivyo wasibezwe na kukatishwa tamaa.
  Abubakary Rakesh alisema hayo jana wakati akisoma risala ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyabiashara Ndogo Ndogo ‘Machinga’ katika mkutano maalumu uliofanyika kwenye ukumbi wa Korea. Rakesh alisema kutokutekelezwa na kuzipatia ufumbuzi kero zinazowakabili kunatumiwa na baadhi ya wanasiasa kuwashawishi baadhi ya viongozi wa vikundi vya wafanyabiasahara kutaka kushiriki maandamano na kuleta vurugu.
  Aliwaomba machinga watulie kwani utulivu huo ndiyo utakuwa nyenzo za kumwezesha Rais Jakaya Kikwete kufanya juhudi za utekelezaji wa ahadi yake ya ujenzi wa machinga sita zikiwemo mbili za jijini Dar es Salaam.
  “Tunaomba na kuwasihi baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyabiashara ndogo ndogo na wafanyabiashara wenyewe kuacha kutumiwa na kutumika isivyo halali na wanasiasa kwa ajili ya manufaa ya watu wachache kisiasa,” alisema.
  Rakesh aliwashauri wanasiasa kuacha kuwatumia vibaya baadhi ya viongozi wa wafanyabiashara hao kwa manufaa yao binafsi.
  Alisema wafanyabiashara hao ni moja ya makundi ya wananchi ambao wameathirika na kukosekana kwa umeme na kwamba hawapendezewi na hali hiyo.
  Pia, wameomba wapunguziwe kodi katika jengo la Machinga Complex kutoka sh. 60,000 kwa mwezi hadi sh. 20,000 na wamelaani kitendo kilichofanywa na Manispaa ya Kinondoni, kuwavunjia vibanda wafanyabiashara wa eneo la Big Brother, Urafiki.
  Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo alisema Dar es Salaam ipo imara na inaendelea, hivyo wasiwadanganye kwa kutumia udhaifu wao. Alisema majina ya wanasiasa wanaotaka maandamano hayo wanayo.
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nadhani ma great thinkers wapo makini na wewe,washa kushtukia kama wewe ni kada ,naona leo unapost upupu mwingi sana,mara pinda kapokelewa na mabango yanayowashutumu chadema,kazi unayo lakini watanzania wasasa sio wa enzi zile zako,kashanga=t.hizza=makamba=jk.=upupu.:crutch::crutch::crutch::crutch::crutch::crutch::crutch::crutch::crutch::crutch::crutch::crutch::crutch::crutch::crutch:
   
 3. n

  nndondo JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Cheap politics on the part of Rakesh katokea wapi? na bado watalambwa mpaka mwisho, wanadanganywa kujengewa mabanda big brother mbona hawawataji waliosababisha ushenzi huo na kuwachukulia hatua? wajinga ndio waliwao machinga sio wa Ilala tu kwanza hao wachache ukilinganisha na wa manispaa nyingine, wasitake kujidanganya eti wanasiasa kama wao kwao kuna umeme na hawaumizwi na bei ya daladala wala umeme basi wakae bila maandamano
   
 4. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kaka jamii forum ni jukwaa huru halifungamani na upande wowote? afu isitoshe katiba ya nchi inanuruhushu kutoa maoni yangu bila woga as lon as sivunji sheria! by the way mi sio muumini sana wa vyama vya siasa
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Siku nyingine msoma risala akisema wafanyabiashara wasitumiwe kwa maslahi ya watu, umuulize kama huyo anayemsomea risala hamtumii kinyume chake.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Uzuri wa Mkakasi ndani yake jiwe tupu.....................
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,228
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Ujinga, ujinga, ujinga, ujinga, ujingaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mpaka miaka mitano ipite, nenda machinga complex pale karume uone aibu ya mipango ya kikwete- kule juu ni madangulo tuuuuuuuuuuuu. Sijui akijenga nyingine mbili zitafanyiwa nini. Tuwatafutie vijana wetu tuache upuuzi huu wa kujenga maghorofa bila mpango.
   
 8. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Rakesh naye machinga siyo? Kashaga hivo vitaarifa unavitoa kwenye vyombo gani vya habari? Mbona source huweki? Usipende kutumika mafisadi watakuondolea pingili zako za kwenye ule utumbo unaokusaidia kujisaidia shauli yako...
   
 9. L

  Leornado JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyo Machinga aliesema hayo atakuwa alisoma hotuba ilioandaliwa na mafisadi.

  Hivi kweli na hali ya maisha ilivyo ngumu Machinga unajidai kuwa unalazimishwa na wanasiasa uandamame??

  Wasiandamane waone kama hawajawa machinga for the rest of their lives huku mafisadi wakifaidi kodi ya hilo jengo.
   
 10. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  HAPO KWENYE RED JIBU NI HALIFUNGAMANI NA MAFISADI NA WATUMWA WAO. kawambie!
  .
   
 11. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwanza pale Complex waliojigawia siyo MACHINGA halisia. Pia nakupongeza kwa uhuru wako wa kuripoti ukiwa Bukoma na Mara ushafika Dar ili kutuletea habari za zinazojichanganya. Jaribu kukamilisha habari zako ili ziwe na maana. Mfano hao wanasiasa ni kina nani na wametumwa na nani. Maana inawezekana mtu akatoka chama kingine kwenda kupandikiza zengwe kwa chama kingine. Mfano mdogo wa kubainisha ninachokielezea, ni hivi majuzi (February), TLP walipinga uteuzi wa Udiwani wa viti maalum wa Mwaija Choga wakidai kuwa hakuwa mwanachama wao halali na walishangaa kuteuliwa kwake bila kuwasiliana na uongozi wa TLP. Mchezo mchafu wa siasa tunaujua sana, sijui mtatokea wapi mpaka 2015
   
Loading...