Uchaguzi 2020 Wamachinga, Bodaboda nchi nzima watoa tamko kumuunga mkono Magufuli

jijiletublog

Member
Jul 23, 2020
31
74
IKIWA imebaki siku moja Uchaguzi Mkuu ufanyike, Jumuiya ya wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ na madereva pikipiki ‘bodaboda’ nchini, wametoa msimamo wao kuwa watampigia kura mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.

Wamesema hatua hiyo inatokana na mgombea huyo kubeba agenda za Watanzania na makundi yao ikiwamo kuwapatia vitambulisho vya umachinga ambayo ni sababu kuu inayowafanya wao kumpa kura nyingi na za kishindo kesho.

Wakizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam jana, wamesema lao kuelekea Uchaguzi Mkuu tamko lao ambalo limetolewa na wenzao katika mikoa mitano ikiwamo Simiyu, Mwanza, Iringa, Katavi na Mbeya leo ndiyo msimamo wa wafanya biashara wote kwani wamechoka kutumiwa kama amdaraja na kisha kutelekekzwa.

Lengo mahsusi la kuifanya nchi yetu ifanye uchaguzi wa amani na utulivu. Makamu Mwenyekiti Mwenyekiti wa Machinga Taifa, Steven Lusinde serikali ya awamu ya tano imewafanyia mambo makubwa kwa ujumla na wanamuunga mkono Rais Magufuli haya tunayozungumza yameonekana.

“Tumepewa vitambulisho vina faida kubwa kwetu kwenye maeneo ya mjini, tunapata mikopo, bima ya afya nab ado watu wanafanya biashara bila kusumbuliwa.

“Rais ametutoa utumwani kutupeleka nchi ya ahadi na ndani ya miaka mitano tumepata faida kubwa kuliko wakati mwingine. Kwa hiyo sisi wote nchi nzima lengo letu ni moja tu, ashinde hivyo tutajaza kura za kutosha kwenye debe la kura.

“Alituamini bodaboda, machinga na mama lishe, kwanini sisi leo tusimthamini kwa kumpa kura, bado siku moja tu tutamfanyia jambo zuri tutatia tiki tu pale kwa rais, wabunge na madiwani wote wa CCM,” amesema.

Lusinde amesema hawajawahi kuiunga mkono serikali yoyote tangu nchi hii imepata uhuru na kwamba hii ndiyo serikali ya kwanza.

“Wafanyabiashara wanaenda kuwa matajiri na tunaenda na imani kubwa tusikubali kutumika, tumetumika vya kutosha na wanasiasa wanatufanya madaraja wanatupandia kisha wanatutelekeza.

“Lakini Magufuli ametupelekea sehehemu ambayo hatujawahi kuitegemea tangu nchi ipate uhuru. Wamachinga wote tunakwenda na Magufuli, na wafanyabishara wote kuanzia leo tutafute pesa leo na kesho ili kesho kutwa twende tukapige kura na kwenda nyumbani kula pilau kusubiri rais aapishwe,” amesema.

Kwa upande wake Mweka Hazina wa bodaboda jijini Dar es Salaam, Saidi Chenja amesema wajasiariamali wakiwamo waendesha bodaboda na bajaj lazima wahubiri amani kwani ndiyo tunu ya taifa ambapo Oktoba 28 lazima wafanye maamuzi sahihi.

“Viongozi wa upinzani wamezoea kutupandia sisi kama majukwaa wanatutumia kisasa kisha wanatuelekeza, sasa tumeamua jambo moja, ni bora ule ugali maharage kwa furaha kuliko biriani kuku kwenye machozi.

“Bodaboda ulikuwa nzuio la kuingia mjini tangu sasa tunaingia mjini bila bughudha. Tulikuwa tunaonekana tuna vurugu lakini niwahakikishie Watanzania hakuna atakayevunja amani iwe Dar es Salaam au mkoa mwingine wote tutakwenda kupiga kura,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema wameshuhudia kazi imefanyika ndani ya miaka mitano na kusisitiza waendelee kumchagua Magufuli kwani ni kingozi mzuri ili aendelee kuwatendea mazuri.

“Kiongozi mzuri lazima apate upinzani.
Ametuteteta wanyonge bodaboda, machinga na mama lishe Oktoba 28 tusifanye masikhara ili atakeyesema kura zake zimeibwa aone Magufuli anaongoza kuanzia asilimia 90. Tusifanye makosa, rais anataka mafiga matatu ili akitaka kutoa mikopo kwetu kusiwe na vikwazo ndiyo maana tunataka kumpelekea mafiga matatu,” amesema.

Naye mfanyabiashara Saidi Mrisho, amesema kitambulisho cha wamachinga kwa mara ya kwanza wamekipata baada ya kuhangaika sana lakini kwa busara zake Magufuli aliona kwanini zoezi hilo linasuasua akawapatia.

“Kitambulisho hiki kimetusaidia kupata mikopo, Magufuli katuondolea adha ile ya kukimbizwa kimbizwa mitaani tukifanya biashara leo hiii tusingekuwepo lakini pia nina bima ya afya hii haijawahi kutokea tangu uhuru.

“Tunapata mikopo CRDB na NMB, yaani ni nafasi yako hakuna hati ya nyumba wala kiwanja. Jukumu letu ni kumfurahisha yule eliyetuweka sisi tuwe juu. Hakuna chinga aliyekuwa anakipenda chama chochote isipokuwa yeye ametufanya tuipende CCM, tumeanza pamoja na tutamaliza pamoja.

Mjumbe wa Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Chengula amesema Serikali ya awamu ya tano inatofautiana sana na awamu zilizopita kwani kafanya makubwa sana hususani kwa bodaboda pale aliporidhia kutambua boda kuwa usafiri rasmi kisheria.

“Nasiki kuna miaka mitano tena na miaka mitano kwanza, hakuna sababu ya mitano kuipeleka sehemu nyingine zaidi ya CCM.

“Hakuna asiyemfahamu Farao aliwaua watoto wa kiume lakini Mungu alimvumilia Musa akakua. Lakini tukizungumia Sodoma na Gomora Mungu hakuvumilia, huyu mgombea wa miaka mitano kwanza anatuletea mambo ambayo katiba yetu hairuhusu.

“Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawasiliano siyo mahusiano, nchi yetu hairuhusu mambo hayo,” amesema.

IMG-20201026-WA0394.jpg
 
Mimi nimewauliza wamesema labda alimaanisha wasengerema peke yao.

Mwaka huu mtausimulia maana kwingine hata ukhanithi wenu hawataki kuusikia.
 
Mimi mwenyewe ni dereva wa bodaboda na wala hatujakutana kutoa hilo azimio hao boda boda wenyewe kwanza wana viriba tumbo inaonekana hata hawajawi kuonja viroba. Siku hizi kuna vikundi vya watu fulani vinajifanya vinaweza kusemea wengine
 
IKIWA imebaki siku moja Uchaguzi Mkuu ufanyike, Jumuiya ya wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ na madereva pikipiki ‘bodaboda’ nchini, wametoa msimamo wao kuwa watampigia kura mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli...
CCM kwa kujifariji, bila dhuruma CCM ni sawa na UDP ya John momose Cheyo.
 
Machinga, bodaboda,mama lishe umwaga chakula kila siku biashara hazitoki wateja wanapiga pass ndefu,
Ukisomesha watu namba why uwasumbue kura zao?
Vuna ulichopanda siasa ni akili na sio nguvu.
 
IKIWA imebaki siku moja Uchaguzi Mkuu ufanyike, Jumuiya ya wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ na madereva pikipiki ‘bodaboda’ nchini, wametoa msimamo wao kuwa watampigia kura mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli...
Mungu awabariki Sana wamachinga watu wa Mungu
 
IKIWA imebaki siku moja Uchaguzi Mkuu ufanyike, Jumuiya ya wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ na madereva pikipiki ‘bodaboda’ nchini, wametoa msimamo wao kuwa watampigia kura mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.

Wamesema hatua hiyo inatokana na mgombea huyo kubeba agenda za Watanzania na makundi yao ikiwamo kuwapatia vitambulisho vya umachinga ambayo ni sababu kuu inayowafanya wao kumpa kura nyingi na za kishindo kesho.

Wakizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam jana, wamesema lao kuelekea Uchaguzi Mkuu tamko lao ambalo limetolewa na wenzao katika mikoa mitano ikiwamo Simiyu, Mwanza, Iringa, Katavi na Mbeya leo ndiyo msimamo wa wafanya biashara wote kwani wamechoka kutumiwa kama amdaraja na kisha kutelekekzwa.

Lengo mahsusi la kuifanya nchi yetu ifanye uchaguzi wa amani na utulivu. Makamu Mwenyekiti Mwenyekiti wa Machinga Taifa, Steven Lusinde serikali ya awamu ya tano imewafanyia mambo makubwa kwa ujumla na wanamuunga mkono Rais Magufuli haya tunayozungumza yameonekana.

“Tumepewa vitambulisho vina faida kubwa kwetu kwenye maeneo ya mjini, tunapata mikopo, bima ya afya nab ado watu wanafanya biashara bila kusumbuliwa.

“Rais ametutoa utumwani kutupeleka nchi ya ahadi na ndani ya miaka mitano tumepata faida kubwa kuliko wakati mwingine. Kwa hiyo sisi wote nchi nzima lengo letu ni moja tu, ashinde hivyo tutajaza kura za kutosha kwenye debe la kura.

“Alituamini bodaboda, machinga na mama lishe, kwanini sisi leo tusimthamini kwa kumpa kura, bado siku moja tu tutamfanyia jambo zuri tutatia tiki tu pale kwa rais, wabunge na madiwani wote wa CCM,” amesema.

Lusinde amesema hawajawahi kuiunga mkono serikali yoyote tangu nchi hii imepata uhuru na kwamba hii ndiyo serikali ya kwanza.

“Wafanyabiashara wanaenda kuwa matajiri na tunaenda na imani kubwa tusikubali kutumika, tumetumika vya kutosha na wanasiasa wanatufanya madaraja wanatupandia kisha wanatutelekeza.

“Lakini Magufuli ametupelekea sehehemu ambayo hatujawahi kuitegemea tangu nchi ipate uhuru. Wamachinga wote tunakwenda na Magufuli, na wafanyabishara wote kuanzia leo tutafute pesa leo na kesho ili kesho kutwa twende tukapige kura na kwenda nyumbani kula pilau kusubiri rais aapishwe,” amesema.

Kwa upande wake Mweka Hazina wa bodaboda jijini Dar es Salaam, Saidi Chenja amesema wajasiariamali wakiwamo waendesha bodaboda na bajaj lazima wahubiri amani kwani ndiyo tunu ya taifa ambapo Oktoba 28 lazima wafanye maamuzi sahihi.

“Viongozi wa upinzani wamezoea kutupandia sisi kama majukwaa wanatutumia kisasa kisha wanatuelekeza, sasa tumeamua jambo moja, ni bora ule ugali maharage kwa furaha kuliko biriani kuku kwenye machozi.

“Bodaboda ulikuwa nzuio la kuingia mjini tangu sasa tunaingia mjini bila bughudha. Tulikuwa tunaonekana tuna vurugu lakini niwahakikishie Watanzania hakuna atakayevunja amani iwe Dar es Salaam au mkoa mwingine wote tutakwenda kupiga kura,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema wameshuhudia kazi imefanyika ndani ya miaka mitano na kusisitiza waendelee kumchagua Magufuli kwani ni kingozi mzuri ili aendelee kuwatendea mazuri.

“Kiongozi mzuri lazima apate upinzani.
Ametuteteta wanyonge bodaboda, machinga na mama lishe Oktoba 28 tusifanye masikhara ili atakeyesema kura zake zimeibwa aone Magufuli anaongoza kuanzia asilimia 90. Tusifanye makosa, rais anataka mafiga matatu ili akitaka kutoa mikopo kwetu kusiwe na vikwazo ndiyo maana tunataka kumpelekea mafiga matatu,” amesema.

Naye mfanyabiashara Saidi Mrisho, amesema kitambulisho cha wamachinga kwa mara ya kwanza wamekipata baada ya kuhangaika sana lakini kwa busara zake Magufuli aliona kwanini zoezi hilo linasuasua akawapatia.

“Kitambulisho hiki kimetusaidia kupata mikopo, Magufuli katuondolea adha ile ya kukimbizwa kimbizwa mitaani tukifanya biashara leo hiii tusingekuwepo lakini pia nina bima ya afya hii haijawahi kutokea tangu uhuru.

“Tunapata mikopo CRDB na NMB, yaani ni nafasi yako hakuna hati ya nyumba wala kiwanja. Jukumu letu ni kumfurahisha yule eliyetuweka sisi tuwe juu. Hakuna chinga aliyekuwa anakipenda chama chochote isipokuwa yeye ametufanya tuipende CCM, tumeanza pamoja na tutamaliza pamoja.

Mjumbe wa Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Chengula amesema Serikali ya awamu ya tano inatofautiana sana na awamu zilizopita kwani kafanya makubwa sana hususani kwa bodaboda pale aliporidhia kutambua boda kuwa usafiri rasmi kisheria.

“Nasiki kuna miaka mitano tena na miaka mitano kwanza, hakuna sababu ya mitano kuipeleka sehemu nyingine zaidi ya CCM.

“Hakuna asiyemfahamu Farao aliwaua watoto wa kiume lakini Mungu alimvumilia Musa akakua. Lakini tukizungumia Sodoma na Gomora Mungu hakuvumilia, huyu mgombea wa miaka mitano kwanza anatuletea mambo ambayo katiba yetu hairuhusu.

“Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawasiliano siyo mahusiano, nchi yetu hairuhusu mambo hayo,” amesema.

View attachment 1613076
Na 2025 mtangaze tena kuunga juhudi ndo maana nilisema mpigwe tu
 
...
Viongozi wa upinzani wamezoea kutupandia sisi kama majukwaa wanatutumia kisasa kisha wanatuelekeza, sasa tumeamua jambo moja, ni bora ule ugali maharage kwa furaha kuliko biriani kuku kwenye machozi.
...
... eneo hili la dunia, I mean Tanzania, nadhani ndio eneo lenye binadamu wenye IQ ndogo kuliko eneo lingine lolote! Ni lini hao wapinzani walikamata dola kisha wakawatelekeza? Na kuna "watu" waliokuwa wanamshangilia kwa nderemo na vifijo msoma tamko! Funny!
 
Ndo maana mimi sikuwaonea huruma kabisa waache washughulikiwe sana na hangaya yupo nje anazurura
 
Back
Top Bottom