Wamaasai kudai ardhi yao ya asili bonde la ngorongoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamaasai kudai ardhi yao ya asili bonde la ngorongoro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kowakdengo, Sep 5, 2012.

 1. K

  Kowakdengo Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Waziri Mkuu mstaafu (aliyejiuzulu), Edward Lowassa akinyoosha juu fimbo ya ishara ya uongozi (Laigwanan), kuashiria upigaji kura ya kukubali maazimio yaliyopitishwa baada ya kikao cha siku mbili cha viongozi wa mila wa Kimaasai.
  [​IMG]

  Baadhi ya viongozi wa kimila wa Kimaasai (Malaigwanan), wakinyoosha fimbo zao juu kupiga kura ya kupisha maazimio ikiwemo kudai haki ya ardhi yao ya asili ndani ya bonde la Ngorongoro.

  Jamii ya wafugaji wa Kimaasai imejipanga kudai haki ya kumiliki, kutumia na kuiendeleza ardhi yao ya asili waliyopewa na Mwenyezi Mungu katika bonde la hifadhi ya Ngorongoro na tayari kikao cha viongozi wa mila wa jamii hiyo (malaigwanan), wameunda kamati ya watu 14 itayoongozwa na Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwenda Ikulu kumwona Rais Jakaya Kikwete kuwasilisha madai yao.

  Katika kikao chao cha siku mbili kilichofanyika mjini Monduli hivi karibuni, jamii hiyo imesema imechoka kuonekana wanafanyiwa hisani kuishi ndani ya bonde hilo na wanataka katiba mpya itamke na kutambua uwepo wao ndani ya eneo hilo na kuwapa haki ya kumiliki ardhi kama walivyo makabila na jamii nyingine nchini.

  Pamoja na kutaka haki yao ya kumiliki ardhi itambuliwe kwenye katiba mpya, jamii ya wafugaji pia wanataka sehemu ya ardhi wanazozihifadhi kwa ajili ya malisho kulingana na kipindi cha majira ya mwaka kwa kuzingatia mahitaji yao yasichukuliwe kama maeneo ya wazi na hivyo kuvamiwa au kugawanywa kwa watu/makundi mengine.
   

  Attached Files:

  • za.jpg
   za.jpg
   File size:
   1.8 MB
   Views:
   216
  • aa.jpg
   aa.jpg
   File size:
   1.6 MB
   Views:
   231
 2. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,876
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  nape atasema wametumwa na cdm
   
 3. i

  iMind JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,871
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wahehe wakidai ardhi ya asili pale mafinga na kuondoa shamba la miti la sao hill. Wasukuma wakadai ardhi yao ya asili buzwagi, bulyanhulu , na mwadui. Wachaga wakadai ardhi yao ya asili ya mlima kilimanjaro, Wazaramo wakadai ufukwe wao wa asili na kuondoa bandari, the list goes on. Wamasai waachwe kupotoshwa. Jamii nyingi zime toa ardhi zao za asili kwa manufaa ya Taifa letu
   
 4. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wizi mtupu!!
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,799
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwani ardhi hiyo imehama?Ooops namaanisha inamilikiwa na nani kwa sasa?
   
 6. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Siri hii ni kali, kwanini iwape waarabu na kuwaondoa akina Njere?.....CCM haikubaliki.
   
 7. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 14,416
  Likes Received: 6,088
  Trophy Points: 280
  wawekezeji wa kizungu wamegeuka wanaharakati!


  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 8. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 43,611
  Likes Received: 9,952
  Trophy Points: 280
  ulinzi shirikishi waachiwe ardhi yao watulindie faru na wanyama wengne wanaouliwa na majangili.
   
Loading...