Elections 2010 WAMA ni Chama cha Siasa?

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Majuzi Alhamisi nilikuwa sehemu nyakati za jioni hivi, nikasikia kwenye taarifa ya habari ya Redio Uhuru ikisema kwamba Mwenyekiti wa WAMA (ile Taasisi ya Fisti Ledi wa inji hii ya Bongo) amewaambia wananchi kwamba wakichagua CCM Taasisi ya WAMA itachukua watoto wawili kutoka kila wilaya na kuwagharamia masomo. Sasa mimi nikajiuliza WAMA ni chama cha siasa mpaka kishiriki kwenye kampeni za uchaguzi moja kwa moja bila kificho?. Nakumbuka wakati fulani Prof. Anna Tibaijuka alikuwa anaongoza NGO ya wanawake (jina limenitoka), lakini NGO ile ilipigwa stop kufanya shughuli zake kwa tuhuma za kujishughulisha na shughuli za kisiasa ikiegemea Upinzani. Vipi leo WAMA wanafanya hayo tena kwa uwazi halafu wahusika wanakaa kimya?
 
Hilo swali si la msingi. La kujiuliza ni kwa nini First Lady huyu anatumia fedha na mali ya umma kuendesha shughuli zake binafsi!

Hivi "taasisi" ya First Lady imewekwa kwenye sehemu gani ya sheria za nchi? Mbona Mama Sitti Mwinyi na Mama Maria Nyerere hawakuwa na NGO zao, na wala hawakujulikana kama First Lady?

Mambo ya First Lady yalianza - kimya kimya - wakati wa Che Ben Mkapa! Sasa imekuwa kawaida, na Watanganyika hawana ubavu wa kuhoji, hata kupitia kwa Wabunge wao?

Kama tumeshindwa kuhoji Mama Salma Kikwete (jina lake halisi, na sio First Lady Salma Kikwete) kutumia rasilmali za umma kwa shughuli zake binafsi, tunahoji nini yeye kufanya kampeni moja kwa moja, tena kwa rasilmali hizo hizo za Serikali?

2010 TUSIDANGANYIKE
 
Kama WAMA ni NGO ambayo imeomba usajili kwa ajili ya mambo fulani.. itakuwa ni kiuka katiba ya usajili wake maana inafanya kile ambacho kaikuomba kusajiliwa hivyo inafaa ishtakiwe kama taasisi na ikiwezekana ipewe onyo au kufungwa na sio kutoa promises kama chama cha siasa na wagombea wao katika nafasi mbalimbali...

Inaonekana anatumia mgongo wa kuwa mke wa raisi kufanya hayo anayoyafanya na inaonesha ana baraka zote za mumewe kwani asingefanya hivyo kama mumewe angemwambia kwamba utaniweka katika wakati mugumu kuzuia wasiifungie taasisis yako mpenzi...hebu acha kutoa ahadi ambazo kuzitekeleza itakuwa ni vigumu kama chuma cha pua...
 
Nimemwona kwa macho yangu akimnadi mgombea wa CCM Mafia jana, na kutamka bayana kuwa waichague CCM. Haki Elimu itishiwa na Mkapa kwa kuhamasisha watu kuhusu haki zao. Mama Tibaijuka, japo leo naye yuko CCM alipata kibano kwa sababu ya BAWATA. Iweje Salma anatumia fedha za walipa, na michango yetu kunadi CCM? Nawaombeni mlio ughaibuni mtusaidie kuwaambia wachangiaji wake wajue hilo. Tendwa uko wapi? Makame?
 
WAMA ni mkono mwingine wa kuiibia nchi yetu.

Kwa kifupi ni CCM C baada ya CCM B ya kule Pemba.
 
Back
Top Bottom