Wallah huyu Demu ni Muongo Jamani. Huyu demu ni Muongo!!! Kha!

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,468
2,000
Demu mzuri wa sura na umbo. Ila muongo mpaka akisema kitu unakuwa njia panda. Hujui uamini au usiamini.

Juzi alinambia anaumwa sana hawezi hata amka. Hoi bin taabani nikamwambia nimpeleke Hosp akasema mama yake atampeleka nikamtumia vijicent. Leo namwona kwenye picha ya dada mmoja ofisini walikuwa na party jumamos naye yupo anang'aa ng'aa tu macho. Mzima.

Yaani amekuwa akisema uongo mpaka inafikia hatua jana alisema ni siku ya wanawake. Nlikuwa najua ila aliposema yeye ikabidi nikahakikishe.

Nina waswas hata jina lake alinidanganya. Ingawa nmecheck ndo amesajilia simu hilo hilo. Yaani nashindwa mwamini kabisa. Hata siku akisema amefariki ntamkatalia. Sitomwamini mpaka nione kabisa anazikwa na unapita mwezi hajaomba pesa kwangu.

Hii tabia ya uongo inakera sana.hata unashindwa ongea na mtu wa hivi. Maana akiongea inabid uingie google kuhakiki. Mahusiano na mtu mwongo mwongo ni changamoto sana
 
silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
776
1,000
Sisahau nlimtongoza demu siku ya pili akanambia anaumwa UTI, MALARIA NA TYPHOID. nikamwambia ntumie cheti hana.
 
devor

JF-Expert Member
Oct 15, 2017
1,030
2,000
Upo nastori yamadem Tena inamana ule Uzi wa kutafuta utajir Kongo umesha usahau
 
sibbonnobo

Member
Aug 24, 2019
53
125
Sisahau nlimtongoza demu siku ya pili akanambia anaumwa UTI, MALARIA NA TYPHOID. nikamwambia ntumie cheti hana.
Juzi tu demu wangu aliniambia kaangukiwa na feni kazini ofisini kwake. Nikatuma hela ya matibabu. Machale yakanicheza. Jioni nikamwambia nitumie picha y cheti nipate dawa zaidi ofisini kwangu. Alikasirika eti simuamini. Na cheti hakutuma.
 
johnhance

JF-Expert Member
Jul 9, 2016
1,804
2,000
Juzi tu demu wangu aliniambia kaangukiwa na feni kazini ofisini kwake. Nikatuma hela ya matibabu. Machale yakanicheza. Jioni nikamwambia nitumie picha y cheti nipate dawa zaidi ofisini kwangu. Alikasirika eti simuamini. Na cheti hakutuma.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom