Wallace Karia anaiendesha TFF kihuni, adhabu za vifungo na faini za kibabe zinawaumiza wanamichezo. Karia hafai kwa ustawi wa soka letu

Mti Dawa

Member
Aug 10, 2022
6
20
Hivi karibuni sakata la kufungiwa kwa Msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Sande Manara "Bugati" limeshika kasi katika tasnia ya michezo nchini, lakini mtiriko wa matukio ya kuichafua tasnia ya soka kutoka kwa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) na Rais wake, Wallace Karia umeongezeka kwa kasi.

Hebu tuyatazame matukio yenye kulitia DOA CHAFU TFF tangu Rais Karia aingie madarakani;​
  • KARIA NA MKATABA MBOVU WA GSM KWA KLABU ZA HAPA NCHINI.
Ni Karia ndie aliyeingia mazungumzo na makubaliano na Kampuni ya GSM kudhamini Klabu za nchini kwa miaka miwili kwa thamani ya Tshs. Bilioni 2.1

Mkataba huu uliibua mzozo mkubwa mwanzoni, katikati, na mwishoni ambapo ulikufa.

TFF haikushirikisha Klabu hizi wala kuzipa taarifa, bali Karia na genge lake walijadili peke yao na mdhamini. Walisaini mkataba na kuamuru Klabu zivae nembo za mdhamini kama AMRI, wakidai hayo ni makubaliano ya mdhamini na TFF pekee. Hii inaacha harufu ya ubadhilifu na rushwa kutamalaki lakini pia ubabe wa Karia kwa Klabu za hapa nchini hadi kuingilia afya ya kibiashara kwa Klabu hizo

Karia ameshindwa kulipa fidia ya matangazo Klabu zilizovaa nembo ya GSM (kwa kuogopa vitisho na kupewa adhabu na TFF) kwa miezi mitatu kabla mkataba huo haujavunjika kwa kuonekana ni batili na Klabu zilikua na haki.

Soma: GSM yatangaza kujiondoa kwenye udhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara
  • KARIA NA SAKATA LA BARBARA GONZALEZ
Mara baada ya C.E.O wa Simba SC, Barbara Gonzalez kuugomea hadharani mkataba wa TFF na GSM, yakafuatia matukio mfululizo ya kuitwa na Sekretarieti ya TFF pamoja na Kamati ya maadili kujadili kauli zake mbalimbali.

Tukio kubwa lilikuwa ni C.E.O wa Klabu ya Simba iliyokuwa mwenyeji wa mchezo dhidi ya Yanga SC, kuzuiwa kuingia uwanjani na maafisa wa TFF wakidai hawaruhusu watoto ambao walikuja na C.E.O Barbara kuingia VVIP ilihali wote wana tiketi husika. Hii ni namna ambavyo Karia ambaye alitakiwa kuwa mlezi wa soka ila ameamua kumshughulikia C.E.O wa Klabu Barbara Gonzalez kibabe.
  • KARIA NA FUNUNU ZA KUMFUNGIA BARBARA MIAKA 10
Karia anahusishwa na maneno yaliyotapakaa kwenye jamii kuwa waliketi kikao cha siri nyumbani, jinsi ya kumdhibiti Barbara Gonzalez na kumfungia kwa miaka 10 kutojihusisha na soka nchini.

Taarifa hii ilikanushwa na TFF lakini mtiririko wa matumizi ya vifungo kwa wanafamilia ya soka kama silaha unajionyesha wazi katika awamu ya Karia kama Rais wa TFF.

Wafuatao ni wanamichezo ambao wamefungiwa kujihusisha na soka chini ya Rais Karia

1. Shaffih Dauda
Kosa:
Kuchapisha mtandaoni maudhui yanayodaiwa hayakuwa na utii kwa TFF.

Adhabu: Kifungo miaka mitano kutojihusisha na soka pamoja na faini Tsh. Milioni 2.

Shida za Shaffih zilizidi alipomkosoa sana Karia na maamuzi ya TFF, Shaffih Dauda ambaye alishawahi kugombea nafasi ya u-rais wa TFF amefungiwa miaka mitano kutojihusisha na soka, adhabu zinazotokana na kanuni za kuchomekea, kanuni zisizo na tafsiri inayokubalika kwa wote na kanuni batili ambazo hazijasajiliwa popote na mamlaka za nchi kutumika nchini.

Adhabu ya miaka mitano kwenye familia ya wanamichezo wachache ambao nchi bado inajitafuta kujipambanua kimichezo haina uhalisia wala kuonyesha dhamira ya kukuza soka nchini.

Tathmini inaonyesha miaka mitano ni kifungo cha kuhakikisha Rais Karia anamaliza muhula mmoja madarakani bila kukosolewa na Shaffih Dauda na si kumfundisha mkosaji.

Pili, ni ubabe juu ya kanuni zipi zinatumika kutambua makosa ya machapisho ya kimtandao kupitia akaunti binafsi ya mwanamichezo mwenye maoni na uhuru binafsi.

Tatu, iwapo chombo cha kimtandao (media) cha Shaffih ndicho kilitumika kuweka maudhui mtandaoni, basi kilipaswa kifungiwe chombo chenyewe cha habari (online media) na mamlaka ya TCRA na si TFF kumfungia mtu binafsi kujihusisha na soka nchini.

Hii inadhihirisha Karia anatumia mabavu kuwinda watu asiowataka, na si vinginevyo.

2. Mbwana Makata & David Naftali (Kocha & Meneja Mbeya Kwanza).
Kosa:
Kushawishi wachezaji wasiingie uwanjani dhidi ya Namungo FC.

Adhabu: Kifungo miaka mitano kutojihusisha na soka.

Kocha na Meneja wa Mbeya Kwanza wamefungiwa miaka mitano na Karia, TFF wakidai wamekiuka sheria za FIFA na Kanuni, ilihali hoja ya Mbeya kwanza ni mchezo kutoanza bila kuwepo gari ya wagonjwa ambayo timu ya maandalizi ya mechi ilishindwa kutimiza takwa hilo kwa wakati.

Wakati huohuo, klabu ya Yanga SC iligoma kuingia uwanjani kucheza na Simba SC kwa kile kilichodai ratiba kubadilishwa kinyume na kanuni za ligi, TFF wakaisuluhisha kupitia waziri Bashungwa na Serikali bila kumfungia wala kutoa adhabu kwa mtu yeyote, ila Mbeya Kwanza wako kwa tuhuma hizohizo, japo kutoandaa Ambulance ni makosa ya kimaandalizi ya TFF.

3. Hawaiju Gantala (Biashara United - Mara)
Kosa:
Kupinga uchaguzi Mahakama ya kawaida.

Adhabu: Kifungo cha maisha kutojihusisha na soka.

Gantala amefungiwa maisha kwa sheria za FIFA jumlisha Kanuni za TFF. Kanuni ambazo zina ukakasi wa utekelezaji na tafsiri zake.

4. Haji Manara (Msemaji wa Yanga SC)
Kosa:
Kudaiwa kumtishia na kumdharau rais wa TFF, Wallace Karia.

Adhabu: Kifungo miaka 2 kutojihusisha na Soka na faini Tsh. Milioni 20.

Mambo muhimu ya kubadilisha haraka ili soka letu lisalimike.
  1. Kwanza kabisa, natamani kuona uongozi wa TFF ukifumuliwa juu chini, donda la TFF limeoza sana, dawa ni kukata zimazima ili kansa ya Karia isiendelee kutafuna maendeleo ya soka nchini.​
  2. Karia ana kundi linalompa jeuri wakiwemo viongozi waandamizi wa Serikali. Huu uonevu wote unaofanyika una jicho la mtu ndani ya Serikali ambao wao ndio wanafanya maamuzi kupitia Karia, sasa Shirikisho la Mpira haliwezi kuendeshwa kwa u-chawa wa Karia kwa mtu fulani Serikalini au kuwa remote controlled.​
  3. Karia anatumia ubabe na undava kuumiza watu wengine katika soka kwa maslahi na maelekezo kutoka nje ya Taasisi ya TFF, hii sio sawa hata kidogo.​
  4. Kamati za Maadili na Sekratarieti zote hazina meno dhidi ya matakwa ya KARIA NA GENGE LAKE, Kamati hizi zijitafakari sana kuwakosea kwa makusudi watanzania kwa kiasi hiki, hii haikubaliki popote duniani.​
  5. Karia anajinasibu kuwa TFF haiingiliwi na Serikali, lakini TFF ni shirikisho la UMMA, sio taasisi binafsi, Serikali inawajibika kuhakikisha TFF inaendana na taratibu zote za kisheria katika utendaji na utoaji wake wa huduma zake kwa wahusika nchini. Haiwezekani TFF ionee watu halafu Serikali ikae kimya, Serikali inapaswa kulitazama hili vizurii, mpira ni ajira na biashara kubwa sana duniani kwa sasa, na ni burudani pia sio manyanyaso kwa wanamichezo nchini sababu BABA MWENYE NYUMBA KARIA KASEMA.​
  6. Wakati Kamati ya maadili inatoa hukumu dhidi ya HAJI MANARA, ilimsikiliza mlalamikaji? Au hukumu ilitoka kwa maelekezo ya nje kama kawaida?​
  7. Watanzania tunatamani iundwe Kamati Maalum ya kuchunguza adhabu zote za watu wote waliofungiwa katika awamu ya Rais Karia madarakani kwa kuzingatia haki, sheria, kanuni na ustawi wa soka nchini, hatuwezi kufikia maendeleo kwa mkono wa chuma.​
  8. Kamati na Sekratarieti za maadili zichunguzwe upya kimuundo na kimfumo kuondoa migongano ya kimaslahi na Rais wa Shirikisho TFF sababu kimsingi sekretarieti imekua mkono wa adhabu wa Rais wake.​
  9. Kanuni za ligi ziangaliwe upya, tafsiri ya kanuni zote ziwekwe wazi na zitambulike kwa wadau wote pamoja na watu wote ambao wamefungiwa kinyume na kanuni zilizopo watambulike kama watu huru.​
  10. Kauli, maoni au sapoti ya viongozi wa serikali yanaathiri matokeo ya hukumu za kimichezo na maendeleo yake kiujumla. Kiongozi wa TFF anapata nguvu sababu hata serikali inatoa muelekeo dhidi ya mtu/watu fulani, hii inatoa mianya ya hukumu zisizo na uhalisia kutolewa na viongozi kuingilia maamuzi ya TFF kwa mlango wa uani.​
  11. Ni Tanzania pekee ndipo kila uchwao watu wanafungiwa kujihusisha na soka, adhabu kubwa kama hizi hazitolewi mara kwa mara katika mashirikisho ya soka kote duniani, hivyo ziangaliwe adhabu mbadala zenye afya kwa maendeleo ya soka letu kama faini, kutoenda viwanjani kutazama mechi, kutofanya matangazo ya timu n.K​

SWALI LA MSINGI LA KUJIULIZA
Ikiwa TFF inatoa adhabu zote hizi kwa mujibu wa kanuni. Je, kanuni hizi zimesajiliwa wapi na lini?

Ikishindwa kuuambia umma juu ya hilo, maana yake TFF inatoa adhabu batili kwa wanamichezo nchini kupitia kikundi kidogo cha watu walio nje ya TFF na ndani ya Serikali dhidi ya raia wengine walio katika tasnia ya soka nchini.

Hii ina maana vifungo ambavyo TFF inatoa kwa wanamichezo ni vifungo batili na havina uhalali wowote wa kutumikiwa hivyo wawatangazie uhuru wote waliowafungia kwa kanuni ambazo ni batili na hazijahalalishwa na mamlaka za nchi kutumika nchini bali ni adhabu za watu fulani nje ya TFF.

MWISHO KABISA:

TFF na Rais Karia mmeshindwa kusimamia weledi katika utekelezaji majukumu yenu, tuachieni TFF tupate kiongozi mpya, maana Karia amekua chawa wa kikundi kidogo cha watu ndani ya serikali na kutumika kama fimbo ya watu hao, Karia kamwe hawezi kuifikisha Tanzania nchi ya ahadi kwa maendeleo ya soka, Karia ni "Puppet-Leader" kama wa enzi wa Ukoloni anaesaliti soka letu kwa kujali tumbo, ni mbabe na anatumia vifungo kumuondoa yeyote anaeuliza utendaji wake.

KARIA MUST GO! KARIA HAFAI​
 
Nasikia sikia anandoto ya kigombea awamu ya tatu na tayari ameanza kujenga mazingira
 
Tukiongea tunaonekana mashabiki wa upande Fulani. Hata kwa hili bandiko lako usishangae ukaitwa Manara, Zeruzeru, shabiki wa Yanga nk.

Lakini wakati Barbara Gonzalez ananyanyaswa kisa kuingia na watoto, tuliuliza, Hivi wale watoto hata kama kanuni za FIFA (sijui kama ni kweli) zinakataza, kuna madhara gani kiongozi mwenye kuheshimika na Watanzania zaidi ya mil.10 wanaoshabikia klabu ya Simba, kuruhusiwa kuingia nao kisha akafuatwa na kuambiwa kistaarabu kuwa alichofanya ni kinyume cha kanuni? Kwa nini tunataka ubabe hata sehemu inayostahili busara? Hawakutuelewa, na wakapata waungaji mkono Gonzalez afungiwe.

Tukio ambalo mpaka kesho Roho yangu imekataa kuwasamehe TFF na wanasheria wao wasio na hekima wanaojiita Kamati ya Maadili ni tukio la Makata na Naftali wa Mbeya Kwanza. Nikiwa uwanjani niliwalaumu kwa nini Mbeya kwanza hawakucheza mechi ile maana walikuwa wanawaadhibu mashabiki ambao si sehemu ya mapungufu ya TFF hasa mwakilishi wao Chama cha soka mkoa wa Lindi ambao hawakuweka Mazingira sahihi ya mechi Salama.

Lakini baada ya wao kukosea, kilichofuata ni kufungiwa miaka 5 kutojihusisha na soka. Yaani mtaalamu/Mwalimu anayetakiwa kuzalisha vipaji vya soka mnamfungia miaka 5 kwa kosa ambalo na nyie ni wahusika, ila mnatoa adhabu kuficha makosa yenu. Maana sikusikia hatua waliyochukuliwa maafisa waliosababisha kuchelewa kwa Ambulance Lindi. Unamuadhibu miaka 5 Mtu ambaye timu imepoteza hela ya nauli Mbeya to Lindi na point 3 za mezani?

Suala la Manara wengi wamelisema, tumeliongelea na kwangu mtazamo ni ule ule, Karia akikosewa inakuwa imekosewa TFF? Maana chanzo ni utani uliozaa makasiriko na kisha kufukuzana kwenye jukwaa.

Hili linafanywaje suala la kitaifa zaidi ya kuombana radhi waliokoseana? Hata yakifunguliwa mashitaka miaka 2 mil.20 kwa kosa la kuhiyilafiana kauli na Rais wa TFF? Hii adhabu au mauaji?
 
Muache uhuni uhuni kwenye mpira, hizo adhabu zinakuja kwa kufanya mambo ya hovyo kwenye mpira mnataka mchekewe chekewe Tumbafu kabisa
 
Hivi karibuni sakata la kufungiwa kwa Msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Sande Manara "Bugati" limeshika kasi katika tasnia ya michezo nchini, lakini mtiriko wa matukio ya kuichafua tasnia ya soka kutoka kwa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) na Rais wake, Wallace Karia umeongezeka kwa kasi.

Hebu tuyatazame matukio yenye kulitia DOA CHAFU TFF tangu Rais Karia aingie madarakani;​
  • KARIA NA MKATABA MBOVU WA GSM KWA KLABU ZA HAPA NCHINI.
Ni Karia ndie aliyeingia mazungumzo na makubaliano na Kampuni ya GSM kudhamini Klabu za nchini kwa miaka miwili kwa thamani ya Tshs. Bilioni 2.1

Mkataba huu uliibua mzozo mkubwa mwanzoni, katikati, na mwishoni ambapo ulikufa.

TFF haikushirikisha Klabu hizi wala kuzipa taarifa, bali Karia na genge lake walijadili peke yao na mdhamini. Walisaini mkataba na kuamuru Klabu zivae nembo za mdhamini kama AMRI, wakidai hayo ni makubaliano ya mdhamini na TFF pekee. Hii inaacha harufu ya ubadhilifu na rushwa kutamalaki lakini pia ubabe wa Karia kwa Klabu za hapa nchini hadi kuingilia afya ya kibiashara kwa Klabu hizo

Karia ameshindwa kulipa fidia ya matangazo Klabu zilizovaa nembo ya GSM (kwa kuogopa vitisho na kupewa adhabu na TFF) kwa miezi mitatu kabla mkataba huo haujavunjika kwa kuonekana ni batili na Klabu zilikua na haki.

Soma: GSM yatangaza kujiondoa kwenye udhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara
  • KARIA NA SAKATA LA BARBARA GONZALEZ
Mara baada ya C.E.O wa Simba SC, Barbara Gonzalez kuugomea hadharani mkataba wa TFF na GSM, yakafuatia matukio mfululizo ya kuitwa na Sekretarieti ya TFF pamoja na Kamati ya maadili kujadili kauli zake mbalimbali.

Tukio kubwa lilikuwa ni C.E.O wa Klabu ya Simba iliyokuwa mwenyeji wa mchezo dhidi ya Yanga SC, kuzuiwa kuingia uwanjani na maafisa wa TFF wakidai hawaruhusu watoto ambao walikuja na C.E.O Barbara kuingia VVIP ilihali wote wana tiketi husika. Hii ni namna ambavyo Karia ambaye alitakiwa kuwa mlezi wa soka ila ameamua kumshughulikia C.E.O wa Klabu Barbara Gonzalez kibabe.
  • KARIA NA FUNUNU ZA KUMFUNGIA BARBARA MIAKA 10
Karia anahusishwa na maneno yaliyotapakaa kwenye jamii kuwa waliketi kikao cha siri nyumbani, jinsi ya kumdhibiti Barbara Gonzalez na kumfungia kwa miaka 10 kutojihusisha na soka nchini.

Taarifa hii ilikanushwa na TFF lakini mtiririko wa matumizi ya vifungo kwa wanafamilia ya soka kama silaha unajionyesha wazi katika awamu ya Karia kama Rais wa TFF.

Wafuatao ni wanamichezo ambao wamefungiwa kujihusisha na soka chini ya Rais Karia

1. Shaffih Dauda
Kosa:
Kuchapisha mtandaoni maudhui yanayodaiwa hayakuwa na utii kwa TFF.

Adhabu: Kifungo miaka mitano kutojihusisha na soka pamoja na faini Tsh. Milioni 2.

Shida za Shaffih zilizidi alipomkosoa sana Karia na maamuzi ya TFF, Shaffih Dauda ambaye alishawahi kugombea nafasi ya u-rais wa TFF amefungiwa miaka mitano kutojihusisha na soka, adhabu zinazotokana na kanuni za kuchomekea, kanuni zisizo na tafsiri inayokubalika kwa wote na kanuni batili ambazo hazijasajiliwa popote na mamlaka za nchi kutumika nchini.

Adhabu ya miaka mitano kwenye familia ya wanamichezo wachache ambao nchi bado inajitafuta kujipambanua kimichezo haina uhalisia wala kuonyesha dhamira ya kukuza soka nchini.

Tathmini inaonyesha miaka mitano ni kifungo cha kuhakikisha Rais Karia anamaliza muhula mmoja madarakani bila kukosolewa na Shaffih Dauda na si kumfundisha mkosaji.

Pili, ni ubabe juu ya kanuni zipi zinatumika kutambua makosa ya machapisho ya kimtandao kupitia akaunti binafsi ya mwanamichezo mwenye maoni na uhuru binafsi.

Tatu, iwapo chombo cha kimtandao (media) cha Shaffih ndicho kilitumika kuweka maudhui mtandaoni, basi kilipaswa kifungiwe chombo chenyewe cha habari (online media) na mamlaka ya TCRA na si TFF kumfungia mtu binafsi kujihusisha na soka nchini.

Hii inadhihirisha Karia anatumia mabavu kuwinda watu asiowataka, na si vinginevyo.

2. Mbwana Makata & David Naftali (Kocha & Meneja Mbeya Kwanza).
Kosa:
Kushawishi wachezaji wasiingie uwanjani dhidi ya Namungo FC.

Adhabu: Kifungo miaka mitano kutojihusisha na soka.

Kocha na Meneja wa Mbeya Kwanza wamefungiwa miaka mitano na Karia, TFF wakidai wamekiuka sheria za FIFA na Kanuni, ilihali hoja ya Mbeya kwanza ni mchezo kutoanza bila kuwepo gari ya wagonjwa ambayo timu ya maandalizi ya mechi ilishindwa kutimiza takwa hilo kwa wakati.

Wakati huohuo, klabu ya Yanga SC iligoma kuingia uwanjani kucheza na Simba SC kwa kile kilichodai ratiba kubadilishwa kinyume na kanuni za ligi, TFF wakaisuluhisha kupitia waziri Bashungwa na Serikali bila kumfungia wala kutoa adhabu kwa mtu yeyote, ila Mbeya Kwanza wako kwa tuhuma hizohizo, japo kutoandaa Ambulance ni makosa ya kimaandalizi ya TFF.

3. Hawaiju Gantala (Biashara United - Mara)
Kosa:
Kupinga uchaguzi Mahakama ya kawaida.

Adhabu: Kifungo cha maisha kutojihusisha na soka.

Gantala amefungiwa maisha kwa sheria za FIFA jumlisha Kanuni za TFF. Kanuni ambazo zina ukakasi wa utekelezaji na tafsiri zake.

4. Haji Manara (Msemaji wa Yanga SC)
Kosa:
Kudaiwa kumtishia na kumdharau rais wa TFF, Wallace Karia.

Adhabu: Kifungo miaka 2 kutojihusisha na Soka na faini Tsh. Milioni 20.

Mambo muhimu ya kubadilisha haraka ili soka letu lisalimike.
  1. Kwanza kabisa, natamani kuona uongozi wa TFF ukifumuliwa juu chini, donda la TFF limeoza sana, dawa ni kukata zimazima ili kansa ya Karia isiendelee kutafuna maendeleo ya soka nchini.​
  2. Karia ana kundi linalompa jeuri wakiwemo viongozi waandamizi wa Serikali. Huu uonevu wote unaofanyika una jicho la mtu ndani ya Serikali ambao wao ndio wanafanya maamuzi kupitia Karia, sasa Shirikisho la Mpira haliwezi kuendeshwa kwa u-chawa wa Karia kwa mtu fulani Serikalini au kuwa remote controlled.​
  3. Karia anatumia ubabe na undava kuumiza watu wengine katika soka kwa maslahi na maelekezo kutoka nje ya Taasisi ya TFF, hii sio sawa hata kidogo.​
  4. Kamati za Maadili na Sekratarieti zote hazina meno dhidi ya matakwa ya KARIA NA GENGE LAKE, Kamati hizi zijitafakari sana kuwakosea kwa makusudi watanzania kwa kiasi hiki, hii haikubaliki popote duniani.​
  5. Karia anajinasibu kuwa TFF haiingiliwi na Serikali, lakini TFF ni shirikisho la UMMA, sio taasisi binafsi, Serikali inawajibika kuhakikisha TFF inaendana na taratibu zote za kisheria katika utendaji na utoaji wake wa huduma zake kwa wahusika nchini. Haiwezekani TFF ionee watu halafu Serikali ikae kimya, Serikali inapaswa kulitazama hili vizurii, mpira ni ajira na biashara kubwa sana duniani kwa sasa, na ni burudani pia sio manyanyaso kwa wanamichezo nchini sababu BABA MWENYE NYUMBA KARIA KASEMA.​
  6. Wakati Kamati ya maadili inatoa hukumu dhidi ya HAJI MANARA, ilimsikiliza mlalamikaji? Au hukumu ilitoka kwa maelekezo ya nje kama kawaida?​
  7. Watanzania tunatamani iundwe Kamati Maalum ya kuchunguza adhabu zote za watu wote waliofungiwa katika awamu ya Rais Karia madarakani kwa kuzingatia haki, sheria, kanuni na ustawi wa soka nchini, hatuwezi kufikia maendeleo kwa mkono wa chuma.​
  8. Kamati na Sekratarieti za maadili zichunguzwe upya kimuundo na kimfumo kuondoa migongano ya kimaslahi na Rais wa Shirikisho TFF sababu kimsingi sekretarieti imekua mkono wa adhabu wa Rais wake.​
  9. Kanuni za ligi ziangaliwe upya, tafsiri ya kanuni zote ziwekwe wazi na zitambulike kwa wadau wote pamoja na watu wote ambao wamefungiwa kinyume na kanuni zilizopo watambulike kama watu huru.​
  10. Kauli, maoni au sapoti ya viongozi wa serikali yanaathiri matokeo ya hukumu za kimichezo na maendeleo yake kiujumla. Kiongozi wa TFF anapata nguvu sababu hata serikali inatoa muelekeo dhidi ya mtu/watu fulani, hii inatoa mianya ya hukumu zisizo na uhalisia kutolewa na viongozi kuingilia maamuzi ya TFF kwa mlango wa uani.​
  11. Ni Tanzania pekee ndipo kila uchwao watu wanafungiwa kujihusisha na soka, adhabu kubwa kama hizi hazitolewi mara kwa mara katika mashirikisho ya soka kote duniani, hivyo ziangaliwe adhabu mbadala zenye afya kwa maendeleo ya soka letu kama faini, kutoenda viwanjani kutazama mechi, kutofanya matangazo ya timu n.K​

SWALI LA MSINGI LA KUJIULIZA
Ikiwa TFF inatoa adhabu zote hizi kwa mujibu wa kanuni. Je, kanuni hizi zimesajiliwa wapi na lini?

Ikishindwa kuuambia umma juu ya hilo, maana yake TFF inatoa adhabu batili kwa wanamichezo nchini kupitia kikundi kidogo cha watu walio nje ya TFF na ndani ya Serikali dhidi ya raia wengine walio katika tasnia ya soka nchini.

Hii ina maana vifungo ambavyo TFF inatoa kwa wanamichezo ni vifungo batili na havina uhalali wowote wa kutumikiwa hivyo wawatangazie uhuru wote waliowafungia kwa kanuni ambazo ni batili na hazijahalalishwa na mamlaka za nchi kutumika nchini bali ni adhabu za watu fulani nje ya TFF.

MWISHO KABISA:

TFF na Rais Karia mmeshindwa kusimamia weledi katika utekelezaji majukumu yenu, tuachieni TFF tupate kiongozi mpya, maana Karia amekua chawa wa kikundi kidogo cha watu ndani ya serikali na kutumika kama fimbo ya watu hao, Karia kamwe hawezi kuifikisha Tanzania nchi ya ahadi kwa maendeleo ya soka, Karia ni "Puppet-Leader" kama wa enzi wa Ukoloni anaesaliti soka letu kwa kujali tumbo, ni mbabe na anatumia vifungo kumuondoa yeyote anaeuliza utendaji wake.

KARIA MUST GO! KARIA HAFAI​
Rais wa FIFA amesema Karia is the best. Nenda kajinyonge
 
Manara udumu huko ulipo kwa hii kauli hii sikuwahi kukuelewa ila now days naanza kukuelewa ukimtoa kikwete na baba ako mashabiki wote wa Yanga waliobaki hawana akili
Yaan ufanye kosa uachwe ukitaka ufanye kosa na uachwe kaongoze ukoo wako ndio watakuacha
 
Msiyempenda kaja na anazidi kuwatesa weraaaaaah
FB_IMG_16601598506348710.jpg
 
Hiyo campaign yako ya kijinga haiwezi fanikiwa. Tunahitaji nidhamu kwenye soka.
 
Mpira hauhitaji masela unahitaji watu professional.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom