Wall Street Journal Nov-2018: Top 10 riskiest countries to invest in mines, Tanzania rank 3rd.

Tunaweza kusema ni habari njema kwetu lkn kwa upande mwingine tuna sera ya viwanda, tutakimbiwa na wawekezaji, swali la kujiuliza je tupo tayari ku sustain hilo kwa muda gani.
Labda wawekezaji kanjanja/Feki. Unajua kuna wawekezaji wapiga deal tu, na kuna wawekezaji hasa. Wale wapiga deal ndio huwa wanatuchungulia kwanza kuangalia weakness zetu kabla hawajaja, wanatumia mapungufu yetu kutengeneza faida. Siku ukushtuka utasikia ohoo ulisaini mwenyewe na blabla, yeye aliingia akijua hujui kitu fulani na aliwekeza hapo, lakini muwekezaji makini ambaye anaijua biashara yake hafanyi uhuni kama huo. Wenzetu huko wanasainishana mikataba huko WTO, mikataba imepimwa haina ujanjaujanja, haki na maslahi ya wahusika yanazingatiwa na kulindwa kisheria.
Hawa wakwetu wanatuvizia, wanatupiga. Tukishtuka wanaanza kututisha mara nitakushitaki unilipe fidia, mara twende kwa arbitrator, ilimradi fujo tu.
Mkuu sasa ulevi na ujinga umeanza kututoka, yale ma hang over yanaishia hivyo tumeanza kujua jua tuko wapi, na tunafanya nini. Tunataka waje tukiwa sober, wasituibie.
Kabla hawajaja tuli stustain vipi mkuu?! Tutastastain for as long as anapatikana muwekezaji atakaye kubali masharti tuliyojiwekea. Tusikubali kubend kwa kila ajae, tuwe na msimamo wenye kulinda maslahi yetu. Nimesema huko juu tunaweza kuwa wamwisho sokoni au wa mwisho kuuza lakini tuuze kwa faida.
 
Mimi hii habari bado sijamini na kma ni kweli serkali kuu yote ilitakiwa ijiuluku kwa afya na ustawi wa nchi yetu. Yan kuanzia wazir mkuu had Rais MAGUFULI.

ingekuwa nch nyingine zilizoendelea ujinga kma huu wasingeutorelate
 
Aliyechangia hii report anaweza kuwa mganda au mkenya( Nick bariyo) . Hivi ni vita vya kiuchumi . Majirani kupitia waandishi Wao wanajaribu kupeleka ripoti mbaya kuhusu Tanzania ili wao majirani wanufaike kwa uwekezaji kuhamia Kwao au Tanzania kuporomoka kiuchumi ili iwe faida kwao.
Ni Kama yule aliyeandika benki ya Dunia imeinyima msaada Tanzania .
Kwan ni uongo?
 
Na hii hbar kma vle waliijua before ndyo wakaleta habari ya mengi kujenga kiwanda cha magar ya kolea???
 
Hahaha cha mtu mavi, wawekeze huko kwao. Mbona sijawahi kusikia wanataka kujenga viwanda hapa kwetu, wao kuchimba madini tu, kwani kwao hakuna ardhi. Nasi tunataka iphone zitengenezwe Tanzania, madini tuchimbe huko USA na Ulaya.
Wajenge viwanda hata hakuna umeme wala miundombinu yakutosha , Sera nzuri hakuna ,
 
Wajenge viwanda hata hakuna umeme wala miundombinu yakutosha , Sera nzuri hakuna ,
Hahaha umeme ndio huo tunataka kujenga Stiglers gorge wao wanatukataza, eti athari za kuharibu mazingira, na blabla. Watuache tuwawekee umeme wa uhakika. Miundo mbinu gani wanataka, kutosha ni kiasi gani?!
 
tuongoze hata kwenye hili jamani
Ni bora tuongozepo jamani sio kila ranking ikitoka tupo chini huko.

Zimbabwe awe makini soon tunachukua kiti hapo,sie si watu wa mchezomchezo.

Kama hili ni kweli basi naipongeza serikali yangu kwa uthubutu na umakini huu.
 
Sawa alisema, kwani kawapiga? Ni maneno tu, mbona trump anasema mengi hatimizi and he's performing.
Mnatakiwa kuelewa huyu bwana anabonga sana lkn si kila kitu anafanya kama alivyosema a certain type of persona u got to be used to, because people luv him they know and see he's there for the majority poor people.
Unasema "katutia kidole tu, hakutubaka".

Umefuraaaahi kakutia kidole tu, hakukubaka.

Nani kasema Trump ni standard?
 
Kwan ni uongo?
Watu wanawalalamikia majirani kwa mambo ambayo hata Wwatanzania tunayaona?

Na sisi Watanzania tunaoona Jiwe anavyoharibu uchumi wa nchi ni majirani?

Rais ananunua korosho juu ya bei ya soko la dunia, bila strategy ya kupata faida, kwa hela ambazo hazijapitishwa na bunge, halafu watu wanashangilia.

Yani sasa hivi wakulima wa korosho wa Msumbiji wanaweza kuingiza korosho Tanzania, tukanunua kwa bei iliyo zaidi ya soko la dunia, halafu tukose pa kuiuza kwa faida!

Watu wanashangilia.
 
Back
Top Bottom