waliowekwa ndani kwa ajili ya sensa waachiwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

waliowekwa ndani kwa ajili ya sensa waachiwe

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nkisumuno, Aug 31, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ushauri wangu wale wote waliowekwa ndani kwa sababu ya sensa naomba waachiwe huru kwani hata wangekuwepo mtaani wasingehesabiwa kwani vifaa vimeisha. wale wote waliohusika kukwamisha zoezi la sensa kwa kuchakachua vifaa hao ndo wawekwe ndani tukianzia na kamishna kwani haiwezekani maandalizi ya miaka mingi halafu ionekane kama ni ya siku moja.

  Iundwe tume ya uchunguzi ikishirikisha vyombo huru itabainika uovo na ufisadi uliotumika. makarani tumekosa hata tshirt, kofia na hata ukiona vitambulisho hutaamini, mabegi ya kichina, kazi ngumu lakini malipo yake kidogo. Kwa vile muda Unaelekea ukingoni makarani tusikubali kuendelea na kazi muda utakavyoisha labda iwe kwa makubaliano mengine maana serikali ndiyo chanzo cha yote hayo.

  Inakuwaje serikali inakosa madodoso imekuwaje? nani alipewa tenda hiyo? Mbona wanakula na kuiba pesa bila hata kufikiri nchi gani hii? Kujitapa eti kuna mafanikio sana. Labda mafanikio ninayoyaona nimwitikio wa wananchi lakini makarani tumekosa vifaa hizo ndo changamoto ndogo kama tunavyoaminishwa?
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hao waliokataa kuhesabiwa wakamatwe wote, wakaheshabiwe wakiwa mahabusu!
   
 3. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Hamna haja ya kuwaachia kwasababu wamefanya makosa chini ya sheria za sensa za mwaka 2002! Wawe fundisho kwa wengine katika sensa zijazo.
   
 4. Pelham 1

  Pelham 1 JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 521
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ebwana nakuunga Mkono mi mwenyewe nimeyaona hayo: Serikali hakujipanga flesh swala hili maana kama inauwezo wa kusimia mambo mengine kama Vitambulisho kura n.k kwann hili lishindikane!!!? Makarani wanateseka pesa imechakachuliwa kuanzia ngazi juu mpaka kwa Watendaji!!
   
Loading...