Waliowekeza hapa Tanzania kwa mapana na marefu yake sio wawekezaji bali ni wasanzuaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliowekeza hapa Tanzania kwa mapana na marefu yake sio wawekezaji bali ni wasanzuaji

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mbunge, Jun 14, 2011.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dalili za kubaini kwamba mwekezaji si mwekezaji bali ni msanzuaji ni hizi hapa:1. Hutumia mabilioni kujisafisha na kujitakasa kwa sabuni na marashi kwa nje, lakini kwa ndani ananuka uharo na matapishi kabakaba;2. Huwafundisha hata korokoroni wao kudharau sio wananchi tu hata viongozi wao;3. Ahadi zao nyingi ni hewa na hata wakiwa na ziada ya kitu ni bora kioze kuliko mzawa akipate;4. Huhonga vyombo vya habari ikiwemo wahariri wa magazeti, redio na televisheni wasitoe habari zao chafu;5. Huwaabudu viongozi wa juu (waliosafishia njia) na kuwadharau viongozi wa nchi.6. Kwa kuwa wana kiwanja cha ndege kwenye mgodi huko bushi hawasumbuki kutengeneza barabara kwani mwananchi wa kawaida atapita.7. Hujenga ubaguzi kati ya wafanyakazi wa juu, wa kati na wale wa chini ambao hauna tofatuti na zile sera alizozipangua Madiba huko Afrika Kusini;8. Wakishaweka korokoroni wao ambao ni 'wazawa' wenye njaa kali zaidi, hawaulizi pale mauaji, dhuluma au uonevu unaporipotiwa kwao. Wanaamini, mzawa kufa au kuathirika kwa hili au lile ni kitu wanachokistahili kutokana na umaskini wao.9. Pamoja na watafiti huko kwao kuonesha kuwa ardhi, makazi ya watu, utamaduni wao, mazingira yao yanastahili kupewa THAMANI KUBWA zaidi kuliko ilivyo sasa ili kuwe na maendeleo endelevu wao husepa, na kwa kuwa viongozi hawajajua juu ya ukweli huu basi wapo wapo tu, lakini hawana msaada kwetu.10. Huizaini serikali ikaingilia kwa mabavu na maguvu matatizo kati yao na wananchi na kusahau kwamba serikali haishi nao bali ni wananchi wanaoishi walikosogezwa kibabe na kiharamu na hadi haki itendeke matatizo yataendelea kati yao;11. Hudanganya viongozi Ulaya, Canada, Ghana, Afrika Kusini kwamba kila kitu nchini kwa upande wao kinakwenda vizuri na hawana matatizo na wananchi, kitu ambacho si kweli;12. Hujenga mifumo ya kulaghai na kuzika ukweli wanapokiuka haki za binadamu na sheria nyingine. Serikali kuu inachoshindwa kuelewa ni kwamba leo mwananchi mkazi wa eneo husika akidharauliwa au kuuawa, kesho atakayedharauliwa ni mfanyakazi wao, kesho kutwa ni kiongozi wa chini wa serikali na mtondogoo ni kiongozi mkubwa wa serikali.13. Pamoja na ukweli kuwa baadhi ya wawekezaji hawa wanajifanya ni wacha Mungu na wanashirikiana na baadhi ya madhehebu ya dini nchini lakini wana mengi pia mabaya wanayoyaendesha kwa pamoja na mengi katika uficho mkubwa kutokana na haki, misamaha na ruhusa za kiajabu ajabu wanazopewa wawekezaji wetu;13. LAANA ya kupora rasilimali ya wakazi wa maeneo mbalimbali nchini sio laana ya kudharauliwa. Laana hiyo itatoka chini hadi juu na kizazi hadi kizazi, na Mungu atupe umri tutaiona tu!
   
Loading...