Waliowasindikiza Esther Matiko na Bulaya bungeni wafutwa uanachama wa CHADEMA

Wamewaonea tu, siku hiyohiyo bungeni alionekana Elizabeth Mwakipesile akiwa kamsindikiza Mbunnge Sofia Mwakagenda. Mbona yeye hajafukuzwa?!
Vijana wa UVCCM muwe mnajitahidi kusoma jambo na kulielewa, umeambiwa CHADEMA mkoa wa mara ndio wamewafukuza wanachama wake, wewe unahoji kwanini wa mbeya hajafukuzwa?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoa wa Mara kimewavua uongozi na kuwafuta uanachama wanachama wake nane akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Tarime kwa kosa la kuwasindikiza waliokuwa viongozi na wanachama wa chama hicho Ester Bulaya na Esther Matiko bungeni Dodoma pamoja na kukiuka sheria za chama.

=====

Uongozi wa CHADEMA mkoani Mara umewafuta uanachama na kuwavua nyadhifa za uongozi watu nane akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wilaya ya Tarime.

CHADEMA kimefikia maamuzi hayo baada ya wanachama hao kuwasindikiza bungeni, Ester Bulaya na Esther Matiko ambao ni wabunge wa viti maalum ambao waliwahi kuwa wanaCHADEMA.

Aidha Peter Makwi ambaye alikuwa Katibu wa CHADEMA Jimbo la Tarime Mjini ametuhumiwa kuwa anajitangaza kuwa ni Katibu wa Esther Matiko ambaye hatambuliki na Chama.

CHADEMA kiliwafukuzwa uanachama wabunge 19 walioapishwa kuwa viti maalum, kwa sasa bado rufaa yao haijatolewa majibu kama wanaendelea kutambulika kama wanachama wa CHADEMA.

View attachment 1722853

ITV
Halafu mnadai hii SACCOSS ia demokrasia,
 
Back
Top Bottom