Waliowashawishi kuhamia CCM wanaondoka bila ahadi ya vyeo kutimia. Nani alaumiwe?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,343
217,371
Humphrey Polepole ambaye ndiye aliyekuwa ofisa mazungumzo (manunuzi) siku yoyote ataachia kiti cha uenezi kwa vile kishaingia bungeni. Huku mlipaji mkuu wa chama ambaye ni Katibu Mkuu Mh Bashiru Ally akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu kiongozi wa Ikulu, na bila shaka ataondoka kwenye Ukatibu Mkuu wa CCM

Watakuja wengine wenye mipango mipya, hofu yangu ni kwa vijana walioshawishiwa watukane walikotoka. Je, ni nani atawakumbuka ikiwa ahadi ya kupewa vyeo haikuandikwa popote?

2007280_17_Tanzanian_opposition_legislators_face_various_politically_motivated_offenses_.jpg
 
Inasemekana aliachwa makusudi ili aje kujaza nafasi ya Bashiru
Nafasi ya Bashiru kwio😂😂😂

Kwani Kijazi kafa kwa makusudi??? Ile nafasi ina wenyewe na sio mashinji

Kama Ukatibu wa Upinzani ulimshinda akajawa na tamaa unahisi CCM atatosha? Aendee kuomba Mungu Changamoto ya kupumua ishike kasi pengine anaweza kuibukia mbele ya safari😂😂😂
 
Sijaelewa kwamba hao walishawishiwa ahadi ya kuwa viongozi kwenye chama au serikali?
Sasa kama Bashiru anakua katibu mkuu kiongozi atashindwa vipi kuwapigia chapuo wapate vyeo hao walioahidiwa?
Ingawa pia kama waliondoka kwenye vyama vyao wakiahidiwa vyeo basi niwanasiasa wasiofaa.
 
Sijaelewa kwamba hao walishawishiwa ahadi ya kuwa viongozi kwenye chama au serikali?
Sasa kama Bashiru anakua katibu mkuu kiongozi atashindwa vipi kuwapigia chapuo wapate vyeo hao walioahidiwa?
Ingawa pia kama waliondoka kwenye vyama vyao wakiahidiwa vyeo basi niwanasiasa wasiofaa.
Shetani hana rafiki, Katibu mkuu kiongozi hana uwezo wa kuteua yeyote, yeye anatoa maoni tu kwa majina yaliyoletwa, lakini katibu mkuu wa CCM ana uwezo wa kuteua watu wake wawe Ma DC au Ma RC au hata mawaziri, ninao ushahidi wa baadhi ya watu wa Katibu mkuu kuukwaa uongozi akiwemo naibu waziri anayetokea kaskazini.
 
Back
Top Bottom