Waliowashawishi kuhamia CCM wanaondoka bila ahadi ya vyeo kutimia. Nani alaumiwe?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,137
2,000
Humphrey Polepole ambaye ndiye aliyekuwa ofisa mazungumzo (manunuzi) siku yoyote ataachia kiti cha uenezi kwa vile kishaingia bungeni. Huku mlipaji mkuu wa chama ambaye ni Katibu Mkuu Mh Bashiru Ally akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu kiongozi wa Ikulu, na bila shaka ataondoka kwenye Ukatibu Mkuu wa CCM

Watakuja wengine wenye mipango mipya, hofu yangu ni kwa vijana walioshawishiwa watukane walikotoka. Je, ni nani atawakumbuka ikiwa ahadi ya kupewa vyeo haikuandikwa popote?

2007280_17_Tanzanian_opposition_legislators_face_various_politically_motivated_offenses_.jpg
 

dindilichuma

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
1,371
2,000
Sijaelewa kwamba hao walishawishiwa ahadi ya kuwa viongozi kwenye chama au serikali?
Sasa kama Bashiru anakua katibu mkuu kiongozi atashindwa vipi kuwapigia chapuo wapate vyeo hao walioahidiwa?
Ingawa pia kama waliondoka kwenye vyama vyao wakiahidiwa vyeo basi niwanasiasa wasiofaa.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,137
2,000
Sijaelewa kwamba hao walishawishiwa ahadi ya kuwa viongozi kwenye chama au serikali?
Sasa kama Bashiru anakua katibu mkuu kiongozi atashindwa vipi kuwapigia chapuo wapate vyeo hao walioahidiwa?
Ingawa pia kama waliondoka kwenye vyama vyao wakiahidiwa vyeo basi niwanasiasa wasiofaa.
Shetani hana rafiki, Katibu mkuu kiongozi hana uwezo wa kuteua yeyote, yeye anatoa maoni tu kwa majina yaliyoletwa, lakini katibu mkuu wa CCM ana uwezo wa kuteua watu wake wawe Ma DC au Ma RC au hata mawaziri, ninao ushahidi wa baadhi ya watu wa Katibu mkuu kuukwaa uongozi akiwemo naibu waziri anayetokea kaskazini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom