Waliowahi kupitia dharau, manyanyaso na kusengenywa kipindi wamepigika tukutane hapa

Simbamteme

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
561
1,000
Kwa tamaduni zetu hizi za Kitanzania mtu usipokuwa na uwezo mzuri wa kiuchumi na umeshafikisha umri wa KUTAFUTA, unapitia mengi sana kutoka kwa ndugu, rafiki pamoja na majirani zako.

Mimi nakumbuka kipindi namaliza chuo 2010 baada ya kurudi mtaani nilipitia tabu nyingi sana kutoka kwa majirani zangu (unfortunately 4 me wazee wangu walishafariki kitambo sana) na tupo wawili tu mm na mdogo wangu wa kike ambae ashaolewa na ana mishe zake huko mkoani.

Nakumbuka nilisota mtaani kwa miezi 4 bila inshu ya msingi ya kufanya,nipo tu kijiweni kazi ni kuamka kupiga stori na washkaji kula na kulala (masalio ya boom yalikuwa yananibeba sana kipindi hiko)

Sasa hela ilipokuwa inakaribia kukata ndo nikapata akili ya kutengeneza mkokoteni wa kubebea maji ambao ulikuwa na uwezo wa kubeba madumu 10 hivi.

Nikawa nanunua maji kwa sh 100(kipindi hicho) na kutembea kilometa zaidi ya 8 kutoka pale nnapoishi na kuuza kwa sh 400-500..Hii kazi ilinisaidia sana kupata hela ya ku-sustain maisha kipindi kile..Maana nilikuwa sikosi 5000-7000+ kwa siku.

Hii kazi ilikuwa ni ngumu sana. Pata picha mtaani watu wanajua umesoma halafu unasukuma mkokoteni wa kuuzia maji hapo hapo mtaani na wanakuona kila siku. Nilipata dharau sana kutoka kwa watu wa pale mtaani ILA dharau moja ambayo siwezi kuisahau na nilikuja KUILIPIZA ni ya demu mmoja hivi ambae alihamia hapo mtaani kipindi hicho(nyumba ya 4 kutoka nnapoishi) na alikuwa mzuri kweli. Pilika pilika za ujana nikamtokea yule manzi. Nilichokipata ndo kimenisukuma kuandika huu uzi. Yule manzi alinijibu SHOMBO za hatari na majibu ya DHARAU sana. NILIUMIA sana siku hiyo na nilijiapiza sintakaa nije niumie kiasi hicho kwa sababu ya Mapenzi

Miaka 2 baadae nilipata CHANCE moja Taasisi flani hivi MKOANI. Hiyo kazi ilinifanya nizunguke sana na nilipata pesa nzuri sana(kwa maisha haya ya kitanzania).Nilipotea mtaani Takribani miaka 5 na kitu
 

Simbamteme

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
561
1,000
Hivi ushawahi kutolewa SHOMBO ww na mdada wkt hujamfanyia baya zaidi ya kumtongoza tu?
Inabidi umpe shukrani huyo mdada maana bila yeye ile hali ya kupambana kabisa na maisha usingekuwa nayo kama ulivyofanya sasa. kama angekukubali toka mwanzo yamkini ungebweteka na kujisahau na kubaki kwenye dimbwi la umaskini.

NB; Ona jema katika baya ulilotendewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom