Waliowahi kujiuzulu; Ulikuwa mwisho wao?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
KUna baadhi ya viongozi ambao waliwahi kujiuzulu kwa sababu mbalimbali na baadaye waliweza kujiokoa walipopewa nafasi nyingine. Kuna waliojiuzulu ili kupisha wengine ili wao wafanye mambo mengine na kuna waliojiuzulu kwa sababu walifikia ukingoni... Majina yanayonijia kwa haraka ni:

Mwalimu Nyerere - Alijiuzulu Uwaziri Mkuu na kumwachia Kawawa
Ally Hassan Mwinyi- alijiuzulu Uwaziri wa Mambo ya Ndani kufuatia mauaji ya Shinyanga
Idi Simba - Alijiuzulu Uwaziri wa Viwanda na Biashara kufuatia Kamati Teule kuundwa kuhusu misamaha ya kodi ya Sukari
Kighoma Malima - Sikumbuki vizuri alijiuzulu katika mazingira yapi na kama alijiuzulu kabisa au alitishia kujiuzulu...

Wengine kina nani waliowahi kujiuzulu na kwanini walijiuluzu; na je waliishia wapi?
 
Aboud Jumbe Mwinyi. Machafuko ya hali ya hewa & kisiasa huko Zanzibar. Alimwachia kiti cha uraisi, Alhaji Ali Hassani Mwinyi
 
Prof Joseph Mbilinyi... kwa shingo upande zile sekeseke za Lyatonga Mrema!
Nafikri na Mrema mwenyewe ni kama aliipiga chini ile post ya Waziri wa mambo ya ndani na Naibu waziri mkuu; SIJUI NAYO ILE ILIKUWA NI KWA MANUFAA YA TAIFA!?
 
Prof. Mwandosya, sina uhakika, lakini si naye aliwahi kujiuzulu na kurudi Mlimani..au...

SteveD.
 
Prof Joseph Mbilinyi... kwa shingo upande zile sekeseke za Lyatonga Mrema!
Nafikri na Mrema mwenyewe ni kama aliipiga chini ile post ya Waziri wa mambo ya ndani na Naibu waziri mkuu; SIJUI NAYO ILE ILIKUWA NI KWA MANUFAA YA TAIFA!?

Green29, polepole bro!
Huyo Joseph Mbilinyi ni mwanamuziki wa bongo flava(Mr II) aka "SUSU".
Aliyejiuzulu uwaziri ni Profesa Simon Mbilinyi, aliyekuwa mbunge wa Peramiho. Kwenye hili sakata kulikuwa na wahusika kama Idd Mohamed Simba (alikuwa mbunge wa jimbo la Ilala), Juma Ngasongwa (Ulanga) na Mbilinyi, katika sakata la misamaha katika kuingiza sukari nchini.
 
Huyo Mbilinyi mke wake si bado Mhadhiri Chuo Kikuu.. yeye mwenye hivi bado yuko hai? nadhani alishaaga dunia; sina uhakika. Hivi baada ya kujiuzulu ulikuwa ndio mwisho wake? Halafu Malima alijiuzulu au alikaribia kujiuzulu..?
 
ooh kweli mkuu, nimechanganya na Mr Sugu!! profesa Mbilinyi yupo hai, Nilimuona kwa mbali kwenye zile picha za msiba wa mheshimiwa Salome Mbatia
 
Mke wake ni Marjorie Mbilinyi, mwanaharakati wa masuala ya jinsia plae TGNP. Mbilinyi mwenyewe sasa hivi ni mwenyekiti bodi ya TIC. Alipokuwepo Sitta kabla ya kuingia siasa
 
asante, hawa ndio watu wa kuwauliza kwanini walijiuzulu? Nurujamii nashukuru kwa sababu inanisaidia kuandika makala yangu ya Jumatano. Hivi ni hawa tu ambao waliwahi kujiuzulu? Aboud Jumbe alijiuzulu au alilazimishwa kustaafu?
 
mkjj...

ABOUD JUMBE alilazimishwa kujiuzulu baada ya sekeseke kati yake na mwalimu na MWALIMU NYERERE kuhusu issue ya znz.
 
Huyo Mbilinyi mke wake si bado Mhadhiri Chuo Kikuu.. yeye mwenye hivi bado yuko hai? nadhani alishaaga dunia; sina uhakika. Hivi baada ya kujiuzulu ulikuwa ndio mwisho wake? Halafu Malima alijiuzulu au alikaribia kujiuzulu..?

Mbilinyi yupo, jimbo lake lilichukuliwa na Mwalimu Jenista Mhagama. Mbilinyi aliachana na siasa. Mke wake, bibi Marjorie Mbilinyi alikuwa ni mhadhiri pale Udsm wakati nikiwa pale, sijajua kwa sasa.
Profesa Kighoma Alli Malima, alijivua uanachama wa sisiemu baada ya kutoelewana na raisi Mwinyi, alijiunga na chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), na walitaka kumweka mgombea wa uraisi mwaka huo kwa tiketi ya chama hicho. Bahati mbaya aliitwa mbele ya haki na Muumba kabla ya yote
 
Hivi Marehemu Sokoine Alijiuzulu uwaziri mkuu ili aende kusoma? sikumbuki vizuri tusahihishane. nadhani ilikuwa 1980. akarudi 1983 na kuteuliwa tena kuwa Waziri mkuu.
 
mkjj...

ABOUD JUMBE alilazimishwa kujiuzulu baada ya sekeseke kati yake na mwalimu na MWALIMU NYERERE kuhusu issue ya znz.

Uko sahihi kabisa Ndg Mohamed.
Huyu Jumbe alimuuliza Mwalimu kuhusu hadidu za rejea za muungano pamoja na mambo mengine ambayo yanafanywa siri katika muungano. Suala hili ndilo lililomuudhi Mwalimu, ndipo mkuu Jumbe "akaadhibiwa" katika vikao vya chama.
Sisiemu wanalifahamu hili kwa undani, ila huwa haliongelewi hadharani.
Labda tumuulize Field Marshall undani wake, yeye ana upeo mzuri wa siasa za ndani za sisiemu.
 
hivi hii listi haiwezi kwenda as far as miaka ya kina Oscar Kambona? Hivi Kasanga Tumbo hakujiuzulu Ubalozi UK?

Ninaokumbuka kuwa walijiuzulu ni wafuatao:

1.Edwin Mtei 2.Edward Sokoine 3.Venance Ngula 4.Alli Mwinyi
5.Kighoma Malima 6.Juma Ngasongwa 7.Simon Mbilinyi 8.Hassy Kitine

pia wapo "walioshauriwa kujiuzulu." wengine walitofautiana na wakubwa wao, na walipoacha/walipojiuzulu kazi vyombo vya habari havikutangaza.

the most interesting ones ni wale walioteuliwa na Raisi lakini wakakataa uteuzi huo!! hao nawaheshimu kwani wana msimamo.

NB:
ilitangazwa kwamba Sokoine amejiuzulu kwasababu za kiafya. pia walisema alipelekwa Yugoslavia kwa matibabu. nadhani alikitumia kipindi hicho kutibiwa na kujiendeleza kimasomo.

...OOPS!! kwa hiyo wakubwa wameanza kutibiwa nje muda mrefu tu!!!
 
Nimeona Mmeandika Waliojuzuru Binfsi Jamani,naomba Na Mie List Ya Waliojuzuru Kwa Barua Wakaomba Kurejea Tena The Same Post,,nataka Niandike Makala Zangu Tathmini Inaonyesha Bwana Idrissa Ndie Wa Kwanza ,,labda Na Sababu Zinazoweza Kumfanya Mtu Kujirudi Haraka Kabla Ya Masaa 24
Pdidy
 
Uko sahihi kabisa Ndg Mohamed.
Huyu Jumbe alimuuliza Mwalimu kuhusu hadidu za rejea za muungano pamoja na mambo mengine ambayo yanafanywa siri katika muungano. Suala hili ndilo lililomuudhi Mwalimu, ndipo mkuu Jumbe "akaadhibiwa" katika vikao vya chama.
Sisiemu wanalifahamu hili kwa undani, ila huwa haliongelewi hadharani.
Labda tumuulize Field Marshall undani wake, yeye ana upeo mzuri wa siasa za ndani za sisiemu.

sidhani kama kweli aboud jumbe alijiuzulu kwa sababu ya kuhoji muungano. kwa taarifa fulani ni kuwa maalimu seif alitaka kugombea urais kwa kufikiri zamu ya pemba kutoa rais kwa hiyo akampikia fitina mzee jumbe!!

nitafanya utafiti kwenye makabrasha yangu kucheki nilisoam wapi hii kitu!!
 
Ningependa kujua zaidi kuhusu kujiuzulu kwa A.H Mwinyi, kweli kulitokana na mauaji ya Shinyanga au kulikuwa na sababu nyingine za kisiasa?

Maana kama alivyosema Karume (rais wa sasa wa ZNZ) viongozi Tanzania hawana utamaduni wa kukubali makosa seuze kujiuzulu, sasa kama mzee Mwinyi alikuwa na humility ya kujiuzulu siku hizo more power to him.Lakini kwa nini alirudishwa kwenye serikali? Au ndiyo dynamics za "chafuko wa hali ya hewa ya kisiasa" Zanzibar ulimfanya apande ngazi kutoka Spika wa Baraza la Wawakilishi mpaka "Rais wa muda" Zanzibar?
 
nadhani wengi wa waliojiuzulu bila shinikizo walipata mwisho mzuri ila naona kaka yangu idrisa alishinikizwa kurudi na ninapata shaka na huyo aliyemshinikiza kwamba labda yeye ndiye anayepaswa kuachia ngazi kwa uongozi mbovu
 
Kina Pinda wanapaswa kujifunza kuwa hata ukijiuzulu kama wananchi wanakupenda watakuchagua tena. But Bado wazee wanautamani ukuu. Shame on zem.
 
Back
Top Bottom