Waliowahi ku-order bidhaa online kupitia mtandao wa alibaba naombeni uzoefu wenu

Fundi_Mjasiriamali

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
748
1,329
Habarini za asubuhi wanajamvi,

Kuna bidhaa nataka ku-order online kupitia mtandao wa alibaba, je nitaratibu gani za kufuata ili niweze kuipta bidhaa hiyo kwanzia kufanya malipo mpaka kuweza kuitia mikononi..

napia naomba uzoefu kwa wale walioshawahi kufanya na kufanikiwa mpaka bidhaa kuwafikia ili wachukua siku ngapi, na je kuna utapeli wowote huko.

Je zile bei zinazoandikwa shilingi ya kitanzania ni fixed au ndi inabadilika kulingana na dollar inavyobadilika.

nawasililisha kwa msaada zaidi
 
Kwanza lazima uwe una namba zile za posta zile S.L.P,za barua..maana agents wao ni posta tanzania..baada ya hapo easy tu,unajisajili kupitia app yao..kuhusu bei kuwa in Tsh ni wao wenyewe ndio wanabadilisha kutokana na dollar inavyobadilika kwenye soko..ukiandikiwa bei ndio hiyo hiyo inakuwa fixed..kuhusu utapeli hakuna,mzigo utakufikia tu,ingawa sometimes huwaga kuna changamoto za uchelewashaji wa mzigo,na ukifika tu posta watakutaarifu kwa meseji ukachukue mzigo wako..jamaa wapo vizuri!
 
asantee sana mkuu, vp kufungua sanduku la posta
Una hata haja ya kufungua sanduku la Posta... Wewe andika address na jina la Posta unayoenda kupokelea mzigo then wao watautuma kwenye Posta husika then wewe mhusika utafuata mzigo wako kwenye Posta uliyoiandika.

Sio lazma uwe na sanduku la Posta ndio upate item yako toka AliExpress.

Nilishanunua bidhaa nyingi tu na zinanifikia bila shida pasipo kutumia private postal address.

Asante.
 
Una hata haja ya kufungua sanduku la Posta... Wewe andika address na jina la Posta unayoenda kupokelea mzigo then wao watautuma kwenye Posta husika then wewe mhusika utafuata mzigo wako kwenye Posta uliyoiandika.

Sio lazma uwe na sanduku la Posta ndio upate item yako toka AliExpress. Nilishanunua bidhaa nyingi tu na zinanifikia bila shida pasipo kutumia private postal address.

Asante.
malipo huwa unafanya kwa njia gani!??
 
Mimi nataka kuagiza package ya soral yenye Watt 120, charge controller,tv 32,taa 6 na battery nafanyaje wakuu
 
Mimi nimefanya manunuzi juzi bila hizo address za posta, nimeweka number yangu ya simu na residence address.
Mzigo ukifika Posta inabidi wakujulishe kwa sms sema wengi wavivu kufanya hivyo mzigo unakaa Hadi wiki ndio wanakutumia sms au kukupigia simu.
 
Kwanza lazima uwe una namba zile za posta zile S.L.P,za barua..maana agents wao ni posta tanzania..baada ya hapo easy tu,unajisajili kupitia app yao..kuhusu bei kuwa in Tsh ni wao wenyewe ndio wanabadilisha kutokana na dollar inavyobadilika kwenye soko..ukiandikiwa bei ndio hiyo hiyo inakuwa fixed..kuhusu utapeli hakuna,mzigo utakufikia tu,ingawa sometimes huwaga kuna changamoto za uchelewashaji wa mzigo,na ukifika tu posta watakutaarifu kwa meseji ukachukue mzigo wako..jamaa wapo vizuri!
Una uhakika brother...?? Mimi nimeorder mzigo mwezi wa saba mwaka jana direct kwa dealer wa alibaba..umefika mwezi december baada ya kuomba kampuni ya Agiza wakanichukulie kiwandani nilipoorder ambapo imenigharimu pesa mara mbili yaani jumla yote nimelipa 1.83M

Bora utumie makampuni yaani madalali, wapo wengi hapa Tz.
 
Mzigo ukifika Posta inabidi wakujulishe kwa sms sema wengi wavivu kufanya hivyo mzigo unakaa Hadi wiki ndio wanakutumia sms au kukupigia simu.
Naona kwenye akaunti yangu pale alixpress Kuna procedure wanaonyesha toka order iwe confirmed Hadi kuwa shiped Hadi kufika.

I know kikuu wako fast wanakujilisha instantly..Je naweza kwenda wakati gani posta kuuliza if mzigo umefika?

Maana mzigo nauhitaji ndani ya siku 30 toka nilipie.
 
Msaada kwenye tuta Kwa anayefahamu jinsi ya kuagiza bidhaa Kwa hao jamaa mpaka inakufikia bongo unafuata taratibu zipi na je sio wababaishaji au wapigaji.

Screenshot_20220712-065839.jpg
 
Msaada kwenye tuta Kwa anayefahamu jinsi ya kuagiza bidhaa Kwa hao jamaa mpaka inakufikia bongo unafuata taratibu zipi na je sio wababaishaji au wapigaji.

View attachment 2287645
Msaada kwenye tuta Kwa anayefahamu jinsi ya kuagiza bidhaa Kwa hao jamaa mpaka inakufikia bongo unafuata taratibu zipi na je sio wababaishaji au wapigaji.
Alibaba ni maalum kwa wafanya biashara, orders toka kiwandani,

Ila kwa wateja wa kawaida site yao ni aliexpress ndio web sahihi
==
Rejea
#1. Special thread: Kununua bidhaa Aliexpress na Alibaba
#2. Msaada wakuu namna gani Alibaba wanaship product kwa mteja
#3. Jinsi ya Kununua Bidhaa Kupitia AliExpress Ukiwa Tanzania
==
Zaidi > Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa
 
Back
Top Bottom