Waliovunjiwa mabanda watoa wiki mbili kwa Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliovunjiwa mabanda watoa wiki mbili kwa Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by saragossa, Mar 7, 2011.

 1. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  WAFANYABIASHARA katika soko la Mabibo, Big Brother, jijini Dar es Salaam, waliovunjiwa mabanda ya biashara ili kupisha upanuzi wa barabara ya magari yaendayo kasi, wametoa wiki mbili kwa Serikali kuwalipa bidhaa zao zilizopotea.

  Wafanyabiashara hao wameingia siku ya nne wakiwa katika wakati mgumu baada ya mabanda yao kuvunjwa na serikali, February 28, mwaka huu.
  Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara waliitaka serikali iwalipe kwa sababu walivunja mabanda yao, kinyume na sheria.

  “ Tukio la kuvunjwa kwa sehemu zetu, limefanywa kimakosa kwa sababu tupo kwa amri ya seriakali baada ya kutuamisha kutoka Tandale tukiwa katika usimamizi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Makamba,”alisema Kalega Rajabu


  Naye Hamis Meli alisema kama kiongozi yoyote wa Serikali hatoweza kutokea kwaajili ya kuongea nao, wataanza maandamano kudai haki zao.

  “Tumechoka kwani kama Dk Slaa ana andamana huko mikoani sisi tutaandamana hapa jijini Dar es Salaam,”alisema Meli
  Meli alisema uamuzi wa serikali kuvunja mabanda ya biashara , umewaathiri kuliko waadhirika wa mabomu ya Mbagala.Meli alitoa wito kwa wafanyabiashara wengine kuunga mkono siku ambayo wataanza maandamano.
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kwamba huyu bwana Meli hajui kuwa Dr. Slaa anaandamana mikoaani kwa ajili ya watu kama yeye!!
   
Loading...