Waliovuja Muungano ni Zanzibar or Tanganyika kuvaa koti la Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliovuja Muungano ni Zanzibar or Tanganyika kuvaa koti la Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakke, Jul 19, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1]Wanaosema Muungano hawautaki ni Wz’bar kudai haki yao au ni Wtanganyika kufuja makubaliano ya Muungano na kuendeleza Ubabe na Zarau?[/h]Written by amini // 18/07/2011 // Habari // 2 Comments

  [​IMG]Mh Karume akikabizi nchi ,nembo ya taifa la Tanganyika ni ile ile. Wz'bar we are blind?

  Tanganyika kuwa Tanzania , Nembo ni ile ile ya Taifa la Tanganyika [​IMG]


  Ndugu wana Mzalendo hakuna shaka kuwa tumeona mengi na tumesoma mengi kuwa wasio taka Muungano ni Wtanganyika na Serekali yao ya Tanganyika ijitayo Tanzania.
  Lengo na zamira ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wasisi wawili wa Tanu na ASP yani Mwalim Juliasi Kambarage Nyerere na Mh Abedi Amani Karume kuunganisha nchi mbili zilizo kuwa huru yani Serekali ya Tanganyika na Serekali ya watu wa Zanzibar.
  Kwa lengo la kushirikiana na kuimarisha umoja, lakini juya zamira zote hizo inaonekana wenzetu wa Tanganyika zamira yao ilikuwa sio hio.
  Zamira ya Wtanganyika na Serekali yao ijitayo Tanzania imekuwa ni kuvinyakuwa visiwa vya Zanzibar na kuvizoficha ili vitambulikane kuwa ni sawa na samani ya mikowa midogo ya Pwani ya Tanganyika ijitayo tanzania.
  Hakuna shaka kuwa wenzetu Muungano hawautaki na kuna sababu nyingi tu zakuwa wao ndio wasio utaka Muungano, a.) kwanza ni kuvunja makubaliano ya mkataba mama(Artcle of Union).
  Nikipindi kifupi tu baada ya Zanzibar kuingia ktk Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wenzetu waliaza hapo ku-play game, nipale walipo itisha Bunge lao la Tanganyika bila ushauri wa upande moja wa mshirika wa Muungano kumshauri waka vunja katiba ya Tanganyika na ikawa katiba ya Tanzania kwa kupadiliswa kidogo, na kufutwa kwa Tanganyika na kila palipo andikwa Tanganyika ikabidi patamkwe Tanzan
  l
  Na sihivyo tu ikashukuliwa Bendera ya Tanganyika na nembo ya Tanganyika zote hizo zikafanjwa ndio nembo za taifa la Tanganyika iliovaa koti la Tanganyika.
  Sasa wanao sema Muungano hawautaki ni Wzanzibar kupiga kelele au Wtanganyika kufuja makubaliano ya Muungano?
  Kutokana na hali hii Wzanzibar tulio kwenda nayo na kuvumilia Muungano kwa Zarau na kebehi za wenzetu kipindi chote hishi cha miaka 47, tuna haki na sababu za kimsingi Wzanzibar kukataa kuvunja Muungano na sio marekebicho ya kuchangia katiba ya Tanganyika.
  kuna kila dalili na uchahidi kuwa Tanganyika imevaa koti la Tanzania na kujifanya Super power mbele ya Zanzibar.
  Hii ni kutuzarau na kutu kebehi wenzetu kutokana na sisi Wzanzibar viongozi wetu wa ngazi za juu wa smz kushindwa kuwa makini na kuwashtukizia Wtanganyika kuwa wanasheza foul na haikubaliki ni hatari kwa Zanzibar kumezwa.
  Hivi sasa kelele za Muungano ziko Zanzibar kwa sababu kwa kipindi kirefu wananchi wa Zanzibar walifungwa midomo na ikawa wanashindwa kutowa joto lao kwa kubanwa na sio Serekali ya Tanganyika tu, hata Serekali ya smz imeshiriki kikamilifu kuwazalilisha Wzanzibar ktk harakati za kujinasua ktk Jindamizi la Muungano.
  Leo ndio Wtanganyika wamesha ifikisha pakuifikisha Zanzibar ndio viongozi wetu wa ccm/smz ndio wanajitowa kimasomaso ili kujipapatuwa kuwa wao hawamo?.
  ikiwa wao sio walio tufikisha hapa ni nani Wzanzibar walio tufikisha hapa tunapo papapatua?
  Mimi nasema %75 ya hapa tulipo fika basi viongozi wa ccm/smz zima na jukumu mbele ya Allah wanalo na watakwenda kusimamishwa kila moja na kujibu mabaya yake zidi ya wananchi mazulumu wa Zanzibar.
  Ikiwa wao wakijali,masla au chama mbele au matamanio ya Dunia basi kesi yetu Wzanzibar iko ktk Mahkama ya M/Mungu na kila alofanya ubaya wake siku itafika.
  Chanzo cha ugonjwa huu tulio nao leo ni wao na kwa vile walikuwa na nguvu ya uongozi na wanacho kiongoza basi M/mungu yupo na anawasubiri.
  Kuna waliokuwa na sifa na fahari akina Adof Hitla Juliasi na wenzake wako wapi leo,hatuko nao miongoni kwetu na wameasha kila walichokuwa nacho hapa.
  Kwa hio zulma na mateso walio fanyiwa Wzanzibar M/mungu ndie mwenye kuhukumu na hasahau wala hapotezi, huwezi kumbabaisha wala kumdanganya.
  Mungu kibariki kizazi cha Zanzibar na Wzanzibar wote.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  tatizo ni moja hapo
   
Loading...